Katibu Mwenezi wa CHADEMA atekwa, apigwa

tata mura

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
275
170
Katibu Mwenezi anavuka kwenda ng'ambo anakoishi huku wenzake wakiendelea na mkutano. Au ndo na yeye anaandaliwa kama wa Mwingulu?
 
mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,508
0
Na Christopher Nyenyembe, Mbeya

MADAI kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya kinaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake, yamedhihirika baada ya kundi la vijana wa chama hicho kumteka, kumpiga na kumsababishia maumivu makali Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Mwakibete, Fadhil Mwakosya (35).

Wakati CHADEMA wakiituhumu CCM kuwa imeweka kambi na inaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake, wao walijitetea kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya kuwajengea ukakamavu ili wawe na uwezo wa kuimarisha ulinzi kwa viongozi na wanachama wao.

Mvutano huo uliingia hatua mpya juzi baada ya kundi la vijana wa CCM waliokuwa kwenye kambi ya mafunzo ya Ivumwe kumteka, kumpiga na kumshambulia Mwakosya aliyeumizwa na kukimbizwa kwenye hospitali ya Dar Group alikopatiwa matibabu.

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, Christopher Mwamsiku akisimulia mkasa huo, alisema kuwa wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Sekondari Samora, walipigiwa simu wakitaarifiwa kuwa vijana wa CCM waliokuwa kwenye mazoezi wamemteka katibu wao mwenezi ndipo alipokwenda kuomba wamwachie.

“Hali hii inasikitisha sana nilipofika nilimkuta ameshapigwa na hawezi kusimama na mimi hawakunifanya chochote, baadaye nilimpigia simu Kamanda Diwani na kumweleza kilichotokea,” alisema.

Alisema Mwakosya alikuwa akivuka uwanja kwenda ng’ambo ya pili anakoishi jirani na eneo vijana hao walipokuwa wameweka kambi kwenye Shule ya Ivumwe inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM.

Alibainisha kuwa katibu huyo mwenezi alipotekwa alipewa maelekezo ya kuwaita viongozi wenzake.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete ameielezea hali ya mwenezi wa kata yake kuwa si ya kuridhisha ambapo licha ya kutolewa hospitalini alikolazwa, bado hana uwezo wa kutembea.

“Huu ni unyama, tumewaomba wenzetu wa CCM wafanye siasa za ustaarabu. Tulijua madhara ya mafunzo hayo tangu mwanzo ndiyo maana nililalamika mapema. Unaona sasa tayari wameanza kuumiza watu kabla ya uchaguzi wa udiwani Kata ya Iyela kufanyika Juni 16,” alisema Mwampiki.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Julius Msaka juzi alikiri kuwepo kwa kambi ya vijana katika eneo la Ivumwe, lakini alikana kumteka kiongozi wa CHADEMA.

“Sisi hatujamteka kiongozi wa CHADEMA, hizi ni propaganda. Nasema kama mtendaji mkuu wa vijana wa CCM, hatuwezi kukubali kuona wanaCCM wanapigwa. Tutawalinda wanachama wetu na viongozi wetu, mbona wao wanabandua picha za mgombea wetu na kuwavua vilemba kinamama wa CCM,” alisema Msaka.

Wakati uongozi wa vijana wa CCM ukikataa kuhusika kwenye tukio hilo, habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi na kuthibitishwa na Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani zinaeleza kuwa tayari vijana wawili wamenaswa na kushikiliwa kituo kikuu cha kati wakituhumiwa kumteka, kumpiga na kumsababishia maumivu makali kiongozi wa chama hicho cha upinzani.

“Unaponipigia simu nipo kwenye kikao, jambo hili nitalizungumzia baada ya kutoka kwenye kikao au kesho nitakapoitisha kikao na waandishi wa habari, taarifa za kukamatwa kwa watu waliomshambulia kiongozi wa CHADEMA ninazo tayari,” alisema Kamanda Diwani.Bahati yao mliwashtukia mapema wangesema ni cdm wamefanya kitendo hicho!
 
mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,508
0
Bahati yao mliwashtukia mapema wangesema ni cdm wamefanya kitendo hicho! Inatia shaka na kusikitisha
 
Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,730
2,000
Na Christopher Nyenyembe, Mbeya
MADAI kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya kinaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake, yamedhihirika baada ya kundi la vijana wa chama hicho kumteka, kumpiga na kumsababishia maumivu makali Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Mwakibete, Fadhil Mwakosya (35).

Wakati CHADEMA wakiituhumu CCM kuwa imeweka kambi na inaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake, wao walijitetea kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya kuwajengea ukakamavu ili wawe na uwezo wa kuimarisha ulinzi kwa viongozi na wanachama wao.

Mvutano huo uliingia hatua mpya juzi baada ya kundi la vijana wa CCM waliokuwa kwenye kambi ya mafunzo ya Ivumwe kumteka, kumpiga na kumshambulia Mwakosya aliyeumizwa na kukimbizwa kwenye hospitali ya Dar Group alikopatiwa matibabu.

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, Christopher Mwamsiku akisimulia mkasa huo, alisema kuwa wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Sekondari Samora, walipigiwa simu wakitaarifiwa kuwa vijana wa CCM waliokuwa kwenye mazoezi wamemteka katibu wao mwenezi ndipo alipokwenda kuomba wamwachie.

“Hali hii inasikitisha sana nilipofika nilimkuta ameshapigwa na hawezi kusimama na mimi hawakunifanya chochote, baadaye nilimpigia simu Kamanda Diwani na kumweleza kilichotokea,” alisema.

Alisema Mwakosya alikuwa akivuka uwanja kwenda ng’ambo ya pili anakoishi jirani na eneo vijana hao walipokuwa wameweka kambi kwenye Shule ya Ivumwe inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM.

Alibainisha kuwa katibu huyo mwenezi alipotekwa alipewa maelekezo ya kuwaita viongozi wenzake.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete ameielezea hali ya mwenezi wa kata yake kuwa si ya kuridhisha ambapo licha ya kutolewa hospitalini alikolazwa, bado hana uwezo wa kutembea.

“Huu ni unyama, tumewaomba wenzetu wa CCM wafanye siasa za ustaarabu. Tulijua madhara ya mafunzo hayo tangu mwanzo ndiyo maana nililalamika mapema. Unaona sasa tayari wameanza kuumiza watu kabla ya uchaguzi wa udiwani Kata ya Iyela kufanyika Juni 16,” alisema Mwampiki.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Julius Msaka juzi alikiri kuwepo kwa kambi ya vijana katika eneo la Ivumwe, lakini alikana kumteka kiongozi wa CHADEMA.

“Sisi hatujamteka kiongozi wa CHADEMA, hizi ni propaganda. Nasema kama mtendaji mkuu wa vijana wa CCM, hatuwezi kukubali kuona wanaCCM wanapigwa. Tutawalinda wanachama wetu na viongozi wetu, mbona wao wanabandua picha za mgombea wetu na kuwavua vilemba kinamama wa CCM,” alisema Msaka.

Wakati uongozi wa vijana wa CCM ukikataa kuhusika kwenye tukio hilo, habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi na kuthibitishwa na Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani zinaeleza kuwa tayari vijana wawili wamenaswa na kushikiliwa kituo kikuu cha kati wakituhumiwa kumteka, kumpiga na kumsababishia maumivu makali kiongozi wa chama hicho cha upinzani.

“Unaponipigia simu nipo kwenye kikao, jambo hili nitalizungumzia baada ya kutoka kwenye kikao au kesho nitakapoitisha kikao na waandishi wa habari, taarifa za kukamatwa kwa watu waliomshambulia kiongozi wa CHADEMA ninazo tayari,” alisema Kamanda Diwani.Tushukuru Mungu hawajampeleka Mabwepande ya Mbeya yaani Kawetele, wangemuua.
 
Top Bottom