Katibu Mwenezi wa CHADEMA atekwa, apigwa

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,022
2,000
Na Christopher Nyenyembe, Mbeya
MADAI kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya kinaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake, yamedhihirika baada ya kundi la vijana wa chama hicho kumteka, kumpiga na kumsababishia maumivu makali Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Mwakibete, Fadhil Mwakosya (35).

Wakati CHADEMA wakiituhumu CCM kuwa imeweka kambi na inaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake, wao walijitetea kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya kuwajengea ukakamavu ili wawe na uwezo wa kuimarisha ulinzi kwa viongozi na wanachama wao.

Mvutano huo uliingia hatua mpya juzi baada ya kundi la vijana wa CCM waliokuwa kwenye kambi ya mafunzo ya Ivumwe kumteka, kumpiga na kumshambulia Mwakosya aliyeumizwa na kukimbizwa kwenye hospitali ya Dar Group alikopatiwa matibabu.

Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya, Christopher Mwamsiku akisimulia mkasa huo, alisema kuwa wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Shule ya Sekondari Samora, walipigiwa simu wakitaarifiwa kuwa vijana wa CCM waliokuwa kwenye mazoezi wamemteka katibu wao mwenezi ndipo alipokwenda kuomba wamwachie.

“Hali hii inasikitisha sana nilipofika nilimkuta ameshapigwa na hawezi kusimama na mimi hawakunifanya chochote, baadaye nilimpigia simu Kamanda Diwani na kumweleza kilichotokea,” alisema.

Alisema Mwakosya alikuwa akivuka uwanja kwenda ng’ambo ya pili anakoishi jirani na eneo vijana hao walipokuwa wameweka kambi kwenye Shule ya Ivumwe inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM.

Alibainisha kuwa katibu huyo mwenezi alipotekwa alipewa maelekezo ya kuwaita viongozi wenzake.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete ameielezea hali ya mwenezi wa kata yake kuwa si ya kuridhisha ambapo licha ya kutolewa hospitalini alikolazwa, bado hana uwezo wa kutembea.

“Huu ni unyama, tumewaomba wenzetu wa CCM wafanye siasa za ustaarabu. Tulijua madhara ya mafunzo hayo tangu mwanzo ndiyo maana nililalamika mapema. Unaona sasa tayari wameanza kuumiza watu kabla ya uchaguzi wa udiwani Kata ya Iyela kufanyika Juni 16,” alisema Mwampiki.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Julius Msaka juzi alikiri kuwepo kwa kambi ya vijana katika eneo la Ivumwe, lakini alikana kumteka kiongozi wa CHADEMA.

“Sisi hatujamteka kiongozi wa CHADEMA, hizi ni propaganda. Nasema kama mtendaji mkuu wa vijana wa CCM, hatuwezi kukubali kuona wanaCCM wanapigwa. Tutawalinda wanachama wetu na viongozi wetu, mbona wao wanabandua picha za mgombea wetu na kuwavua vilemba kinamama wa CCM,” alisema Msaka.

Wakati uongozi wa vijana wa CCM ukikataa kuhusika kwenye tukio hilo, habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi na kuthibitishwa na Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani zinaeleza kuwa tayari vijana wawili wamenaswa na kushikiliwa kituo kikuu cha kati wakituhumiwa kumteka, kumpiga na kumsababishia maumivu makali kiongozi wa chama hicho cha upinzani.

“Unaponipigia simu nipo kwenye kikao, jambo hili nitalizungumzia baada ya kutoka kwenye kikao au kesho nitakapoitisha kikao na waandishi wa habari, taarifa za kukamatwa kwa watu waliomshambulia kiongozi wa CHADEMA ninazo tayari,” alisema Kamanda Diwani.

Greda

Member
Apr 20, 2012
95
70
Hakuna cha ujeshi wala usilie lie,huyo kachezea kichapo cha kawaida na hakihusiani na mambo ya jeshi,cha msingi ni kwamba jamaa wapo vizuri wao kama wao,hata cdm kuna kurugenzi ya usalama chini ya Lwakatare ambae pia ni gaidi mkuu hapa nchini,so na yeye afundishe ugaidi vijana wake.
 
Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,637
2,000
Wanasiasa mditupandikizie chuki. Hivi ni lazima kila chama kiwe na walinzi wake wa 'kuwalinfa viongozi wao na wananchama wao'. Kwangu mimi hii ni hatari.
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,726
1,225
Hakuna cha ujeshi wala usilie lie,huyo kachezea kichapo cha kawaida na hakihusiani na mambo ya jeshi,cha msingi ni kwamba jamaa wapo vizuri wao kama wao,hata cdm kuna kurugenzi ya usalama chini ya Lwakatare ambae pia ni gaidi mkuu hapa nchini,so na yeye afundishe ugaidi vijana wake.
Unachoshabikia ni uharifu! Heri wapatanishi maana hao......... ( Mathayo5:1.....)
 
mjasilia

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
595
250
Kwa hasira nataani nimtukane mtu anayejiita kiongozi wa ya hii nchi, sipendi kuogemea upande wowote licha yakwamb ni mfuasi wa itikadi ya chama fulani, si kwakila jambo na ila haya niyaonayo mimi na huku nchi ikiwa na kiongozi nakosa jina la kuyaita, kwa mtu mwenye miaka 18 na kuendela anajua fika kama si kwa kuona ama kusikia au kusoma katika hitoria ya rwanda atakuwa anaelewa kikundi kilichokuw kinaitwa nterahamwe(rwanda 1994) kaziwliyoifanya sasa ni historia ya dunia.

Sitaki niseme sana kwa tanzania, ila vyama vya siasa kuendelea kuwa na kile wanaochokiita vikundi vya ulinzi green guard na red guard na vingievyo mimi kwa akili yangu ndogonaona si sahihi kwa maana tunamajeshi chngu mzima kuanzia polisi, jwtz kushuk mpaka mgambo moja ya shughuli zae ni kulinda usalama wa raia ukijumuisha na viongozi na mali zao;

ishu ya vyama vya siasa kuwa na vikosi vya usalama inatoa wapi ssm mlianziasha haya ila hamkufikilia, cdm wameiga nao hawakuwa makini wameiga kitu kibaya sana, ila inawezekana ni kutokana na mfumo vyombo vya ulinzi kama polisi kushndwa kutokuwa na mlengo wowote wa kivyama haya maeneo yatakuj kutufikisha mabali iku moja nimesema leo mwenye masikio asikie.
 
Fanto

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
208
225
Hivi vyombo rasmi vya usalama kazi yake nini mpaka vyama vya siasa vianzishe vijeshi vyao binafsi kama si kutaka kuanzisha vurugu zisizo za lazima? Tutakuwa na vijeshi vingapi visivyokuwa rasmi na vitawajibika kwa kamanda nani? Ama kweli Tanzania!
 
pius mabula

Senior Member
Jul 2, 2012
196
0
Hakuna cha ujeshi wala usilie lie,huyo kachezea kichapo cha kawaida na hakihusiani na mambo ya jeshi,cha msingi ni kwamba jamaa wapo vizuri wao kama wao,hata cdm kuna kurugenzi ya usalama chini ya Lwakatare ambae pia ni gaidi mkuu hapa nchini,so na yeye afundishe ugaidi vijana wake.
We ni wa kike ama wa kiume?
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,569
2,000
Alitekwa au alivamia kambi ya watu. Alijua hapo kuna kambi ya watu alikuwa anakatisha kwa malengo gani tena eneo la Shule? Hata kama nyumba yake. Habari zako ni za upande mmoja usikute alileta za kuleta vijana wakamuonyesha ukakamavu!!!!
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,453
2,000
uploadfromtaptalk1370881867190.jpg
Hilo ni jeshi la Mwigulu, na yeye ndio kamanda wao.!!
 
Last edited by a moderator:

Kirode

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
3,569
0
Alitekwa au alivamia kambi ya watu. Alijua hapo kuna kambi ya watu alikuwa anakatisha kwa malengo gani tena eneo la Shule? Hata kama nyumba yake. Habari zako ni za upande mmoja usikute alileta za kuleta vijana wakamuonyesha ukakamavu!!!!
tutajibu......subiri...
 
thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,345
1,500
Mkuu katibu wa ccm mkoa unasema amekana kuhusika kwa vijana wake,wewe unaweza kutusaidia kuthibitidha kuwa ni vijana wa ccm umetumia kigezo gani any way pengine kweli tupia picha ya aliyetekwa tukuamini mkuu.
 
Kizotaka

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
561
0
Mkuu katibu wa ccm mkoa unasema amekana kuhusika kwa vijana wake,wewe unaweza kutusaidia kuthibitidha kuwa ni vijana wa ccm umetumia kigezo gani any way pengine kweli tupia picha ya aliyetekwa tukuamini mkuu.
We unadhani atakubali kirahisi mkuu
 
Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Nadhani ni wakati muafaka kwa Mzee Mwambiki kuwatangazia wananchi wa Isengo,Airport,Block T,Soweto,Nzovwe, Mama John,Ilomba,Sai n.k kwamba hawatakiwi kupita eneo la karibu na shule ya Ivumwe vinginevyo watadhuriwa kama Mwangosi,Dr.Ulimboka,Prof.Mwaikusa,Mwakosya n.k Uhuru wa kutembea popote bila kuvunja sheria umefutwa na CCM
 
JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,876
2,000
Hakuna cha ujeshi wala usilie lie,huyo kachezea kichapo cha kawaida na hakihusiani na mambo ya jeshi,cha msingi ni kwamba jamaa wapo vizuri wao kama wao,hata cdm kuna kurugenzi ya usalama chini ya Lwakatare ambae pia ni gaidi mkuu hapa nchini,so na yeye afundishe ugaidi vijana wake.
UMEPOTEZA UWEZO WAKO WA KUFIKIRI!! pole sana. kumbuka vurugu hazina macho,kesho yaweza kuwa zamu yako.
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,567
2,000
Ccm hawawezi siasa za ushindani hata siku moja. Wao wana amini tanzania ni ccm na ccm ndo tanzania! Ccm ni hatari kwa ustawi na mshikamano wa watanzania!
 
Top Bottom