Katibu Mkuu ahimiza ushirikiano baina ya Tanzania na Uchina kupitia michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefungua Mashindano ya mpira wa kikapu ya wafanyakazi wa Kampuni za kichina zinazofanya kazi nchini.

Lengo la kuanzisha mashindano hayo nikuimarisha ushirikiano, mawasiliano na mahusiano baina ya wafanyakazi wa makampuni ya Kichina yanayofanyakazi hapa nchini.

Akifungua mashindano hayo Julai 22, 2023 katika viwanja vya Starlight Arena jijini Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu Bw. Yakubu amehimiza wafanyakazi hao kuendelea kufanya mazoezi kwa kushirikiana ili kuimarisha afya zao hatua itakayowafanya kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kukamilisha miradi ya Serikali wanayoitekeleza huku akiomba Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Michezo.

"Tanzania na China tunaushirikiano Mkubwa sana katika Michezo kuanzia ujenzi wa uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo tumewaomba waendelee kushirikiana na sisi katika uwekezaji kwenye michezo nchini" amesema Katibu Mkuu.

Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu amewaomba katika mashindano yajayo kujumuisha timu za Wanawake na Wanaume kutoka Tanzania kushiriki ili kuendeleza ukuzaji wa vipaji na uhusiano uliopo baina ya nchi hizo.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingjian amemshukuru Katibu Mkuu kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michezo hiyo na ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwenye Sekta ya Michezo.

Makampuni yanayoshiriki mashindano hayo ni yanaongozwa na watumishi wa Ubalozi wa China hapa nchini, Power China Union, Power China, CREC 1, CREC 2 THE GALAXY, CPP, CCCC and CCECC.

IMG-20230722-WA0069.jpg
 
Back
Top Bottom