Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif atua Zanzibar kumalizana na Lipumba

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,935
5,558
Wana JF,

Katibu Mkuu wa Chama wa Wananchi (CUF) Maalim Seif ameshatua Zanzibar tayari kwa ajili ya Kikao cha Baraza Kuu la CUF kinachofanyika leo huko Zanzibar kumjadili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Lipumba.

Kikao hicho kimeitishwa kwa dharura kumjadili [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] baada ya [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] akishirikiana na wafuasi pamoja na Jeshi la Polisi kuvamia Ofisi za Makao Mkuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam kwa kile wanachodai wamepokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi ikimtambua Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF baada ya kujiuzulu uenyekiti wa CUF mwenyewe Agosti 6 mwaka jana akipinga uamuzi wa UMOJA wa [HASHTAG]#UKAWA[/HASHTAG] kumsimamisha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kugombea urais.
Screenshot_2016-09-27-10-40-41.png

Prof.Lipumba kung'oka leo?

#My take: Baada ya kutolewa taarifa kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kumtambua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF kumetokea sintofahamu kubwa sana kuhusu jambo hilo.

Nilisoma kazi na majukumu ya Msajili vya Vyama lakini sijaona kifungu ambacho kinampa mamlaka Msajili wa Vyama kupingana na Maamuzi ya Vikao Vya Kamati Kuu au Baraza Kuu ya Vyama vya Siasa nchini kama alivyofanya kwa CUF, kwa kutoa barua ya kumtambua Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF wakati alishajiuzulu mwenyewe.

Baada ya hapo Baraza Kuu lilipokutana kwenye Mkutano wake wa ndani kujaza nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CUF ndipo Lipumba alivamia Mkutano huo na kuandaa vijana kufanya vurugu na kuvunja Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu uliokuwa unafanyika ambapo ilimpelekea kuchukuliwa hatua za kufukuzwa uanachama.

Nawatakia kila la heri CUF kwenye Mkuu wa Baraza Kuu unafanyika leo naamini watatoa maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya nchi. Migogoro ndani ya chama huleta mgawanyiko mkubwa sana kwa wafuasi wao. Naamini [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] ataheshimu maamuzi ambayo yatatolewa baada ya Mkutano huo.
 
Wana JF.
Katibu Mkuu wa Chama wa Wananchi (CUF)Maalim Seif ameshatua Zanzibar tayari kwa ajili ya Kikao cha Baraza Kuu la CUF kinachofanyika leo huko Zanzibar kumjadili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Lipumba.
Kikao hicho kimeitishwa kwa dharura kumjadili [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] baada ya [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] akishirikiana na wafuasi pamoja na Jeshi la Polisi kuvamia Ofisi za Makao Mkuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam kwa kile wanachodai wamempokea barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi ikimtambua Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF baada ya kujiuluzu mwenyewe novemba 6 mwaka jana akipinga uamuzi wa UMOJA wa [HASHTAG]#UKAWA[/HASHTAG] kumsimamisha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa kugombea uraisi.
Prof.Lipumba kung'oka leo? ???

Ajiuzulu August 6, 2015 na sio Novemba 6
 
1.msomi anajitutumua kwa hisani ya mkoba!
2.kwanini asianzishe chama chake kama kijana alipofukuzwa alianzisha chama...
3.msomi rudi kwenye makaratasi (kushauri) utapata heshima zaidi kuliko kwenye siasa
4.miaka zaidi ya 20, msomi huyohuyo tu!!
5.pumzika msomi wetu. kama zimebaki nenda kwenye barafu kama yuleee...ukale bata.
naota tu...
 
Ajiuzulu August 6, 2015 na sio Novemba 6
Mwaka mmoja na Mwezi mmoja ndio anarudi?
Hii na sawa na mke anaandika talaka na kuondoka kabla ya talaka kukadiliwa na anaonekana akipuyanga huku na kule na mabwana na huku nyuma mume anajiandaa kuoa tena.
Mabwana wanamtosa baada ya kugundua ni malaya eti baada ya mwaka na mwezi anarudi na kuvunja mlango na kusema yeye ndie mke halali kwani hakimu kasema mume hajaijibu ile talaka hivyo mahakama haijaidhinisha.
[HASHTAG]#sipendiubwegemie[/HASHTAG]
 
Mkuu umenifanya nimecheka asbh hii mpaka watu wameshituka.
 
Mwaka mmoja na Mwezi mmoja ndio anarudi?
Hii na sawa na mke anaandika talaka na kuondoka kabla ya talaka kukadiliwa na anaonekana akipuyanga huku na kule na mabwana na huku nyuma mume anajiandaa kuoa tena.
Mabwana wanamtosa baada ya kugundua ni malaya eti baada ya mwaka na mwezi anarudi na kuvunja mlango na kusema yeye ndie mke halali kwani hakimu kasema mume hajaijibu ile talaka hivyo mahakama haijaidhinisha.
[HASHTAG]#sipendiubwegemie[/HASHTAG]
Mkuu umenichekesha sana ujumbe mzuri sana watu wengi hawaelewi kwa nini [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] ameamua kujithalilisha hivyo yote yanatokana na kitu kinaitwa mpango kutumiwa kutaka kuivuruga CUF baada ya hatua ya kwanza kusindwa mwaka jana.Njaa mbaya sana sijui familia ya [HASHTAG]#Lipumba[/HASHTAG] iko wapi inashindwa hata kumshauri?
 
1.msomi anajitutumua kwa hisani ya mkoba!
2.kwanini asianzishe chama chake kama kijana alipofukuzwa alianzisha chama...
3.msomi rudi kwenye makaratasi (kushauri) utapata heshima zaidi kuliko kwenye siasa
4.miaka zaidi ya 20, msomi huyohuyo tu!!
5.pumzika msomi wetu. kama zimebaki nenda kwenye barafu kama yuleee...ukale bata.
naota tu...
Ni Profeselii wa olijino comedy kichwani kasahau alichosomea ndiyo maana hawezi kufanya kazi akihofia watamshitukia ni msomi feki, kwa sasa anashinda kwa Sangoma na yy usiku anapaa na Ungo anaamimini kamati za ufundi alizopewa na February zitamsaidia kupambana na upepo wote CUF. Kwa sasa mzee Pumba si Msomi tena kichwani kasalia na upeo wa kujali pesa si Akili yy hahitaji Akili tena kajitoa fahamu kwa ajili ya kuwafurahisha madalali wa Siasa ambao huambulia 10% kwe pesa anazopewa na akina membe na CCM.
 
Hivi [HASHTAG]#lipumba[/HASHTAG] anawatoto (familia)?

Kama anayo Tafadhali nipatieni namba ya mke wake au mwanae ili niongee nao machache wamshahuri mzee wao.

Tafadhali mwenye namba ani-pm
 
Mwaka mmoja na Mwezi mmoja ndio anarudi?
Hii na sawa na mke anaandika talaka na kuondoka kabla ya talaka kukadiliwa na anaonekana akipuyanga huku na kule na mabwana na huku nyuma mume anajiandaa kuoa tena.
Mabwana wanamtosa baada ya kugundua ni malaya eti baada ya mwaka na mwezi anarudi na kuvunja mlango na kusema yeye ndie mke halali kwani hakimu kasema mume hajaijibu ile talaka hivyo mahakama haijaidhinisha.
[HASHTAG]#sipendiubwegemie[/HASHTAG]
Lipumba alinunuliwa kwa pesa haramu ya marehemu Gadafi toka kwa Membe akatoroka akaenda Rwanda ambapo alifanya uzinzi usiku na mchana huku akiunda vikundi haramu, ile pesa haramu ikamalizikia kwenye vitendo haramu na mpaka leo kashindwa kuoa anaishi na michepuko kibao, hana familia ya kamshauri Akili yake ni sawa na ya darasa la nne tu uwezo wa kufikiri umekamatwa na akina Ole sendeka std 7 hata profesa maji marefu ni mjanja kuliko Huyo single mzee Pumba, alichosomea kasahau ndiyo maana Anyang'ang'ania siasa ili afiche mapungufu yake, ebu jiulize mtu kashindwa kuongoza familia ataweza kuongoza taasisi kubwa Kama CUF?
 
Nakushukuru Mtoa Mada,na Mie Kama TeamLowasa,Ningependa Kuwaomba CUF:
Watupe Msimamo Wao Juu Ya Uchaguzi wa Mameya wa Ubungo na Kinondoni!
Watuambie Hao Madiwani Wanapaswa Kuwa Alligned kwa Nani?Lipumba au Mtatiro!
Watuambie Pia Wao Kama Chama Kilicho Ndani ya Ukawa,je Wanaendelea Kuiunga Mkono Ukawa?na Pia Wana Ukawa Wenza CHADEMA,NLD na NCCR Waiitii Kauli ya Lipumba au Maalim Seif!?
Na Mwisho Watupe Msimamo Kuhusu Wabunge wa CUF,Hasa Wale Ambao Wapo Ndani ya Halmashauri ya Iliyokuwa Wilaya ya Kinondöni!je Hawa Wabunge Wako Alligned na Nani?Lipumba au Mtatiro!
Na Nini Msimamo wa Seif Katika Uchaguzi wa Mameya wa Kinondoni na Ubungo!
 
Back
Top Bottom