Katibu Mkuu Wa CHADEMA, Vicent Mashinji atakiwa ofisi ya DCI kwa mahojiano. Baada ya mazungumzo aeleza kilichojiri

Wakati huo huo yuko kimya kabisa kuhusu miili inayookotwa ufukweni.

Tangia mwigulu awe waziri wa mambo ya nadani haya mambo yameongezeka sana haya bana Tanzania yenu ila siku moja mungu atatenda atutoe kwenye minyororo yenu
 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ametakiwa kuripoti ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imeelezwa.

Dk Mashinji anakwenda kuripoti kipindi ambacho Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa chama hicho, Kigaila Benson anaendelea kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Oktoba 25,2017 mwanasheria wa Chadema, Fredrick Kihwelo amesema, “Katibu Mkuu ametakiwa kuripoti kwa DCI na sasa natoka hapa Central kwa Kigaila nakwenda huko."

Amesema suala la Kigaila kupata dhamana au kupelekwa mahakamani litajulikana mchana wa leo baada ya kutakiwa kurudi Kituo Kikuu cha Polisi.

Kihwelo alipoulizwa ni nini sababu ya Dk Mashinji kuitwa kwa DCI, amesema itakuwa ni mwendelezo wa mahojiano na Jeshi la Polisi kuhusu tuhuma za kutoa lugha za uchochezi alipozungumzia hali ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kigaila ambaye ameshafikisha saa 72 akiwa rumande tangu alipojisalimisha kituoni hapo Jumatatu Oktoba 23,2017 na kuhojiwa kwa kutoa lugha za uchochezi katika mkutano na wanahabari Oktoba 12,2017 makao makuu ya Chadema wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

======
Secretary General of the main opposition party, Chadema Dr Vicent Mashinji has been ordered to report to the office of the Director of Criminal Investigation (DCI).

The order comes at the time when Chademas director of operation and training Mr Benson Kigaila is grilled at the central police station since Monday October 23 when he surrendered for questioning.

Speaking to The Citizen on Wednesday, October 25, Chadema advocate, Mr Fredrick Kiwhelo said; “Dr Mashinji has been ordered to report for questioning, right now, I am coming from central police station to see Mr Kigaila and I’m on the way to the DCI office.”

Speaking about reason behind Dr Mashinji’s summons, Mr Kihwelo said it was in connection to the questioning for the allegedly issuance of sedition statement during press conference held recently in the city.

During the press conference, among other things, Dr Mashinji spoke about the attack of the Singida East MP Tundu Lissu in Dodoma in September 7.

On Mr Kigaila, the advocate said his fate would be known later today.

Mr Kigaila is questioned for allegedly issuing sedition statement during the press conference held on October 12 at the Party’s headquarters in Kinondoni District.


Source: Chadema SG directed to report to DCI’s office
Zitto kabwe tumekabizi nchi kwa washamba,na malimbwikeni
 
Badala ya kukamata hao wauaji mapolisi wenzao wasiojulikana wao wanakomaa na viongozi wa chadema.. pambaff kabisa
yote yana mwisho tu lakini
 
Hawa CHADEMA. wanaboa sana, hivi kweli watu waache kufanyakazi wabaki kusikia kauli zao za kijinga kijinga tu.
We una kazi gani?ebu acha iyo kazi yako nenda kawasikilize\kawatazame wale jamaa wanaopenda kujitokeza live kila siku
 
HIVI NI KWANINI HASA VIJANA WENGI WA CCM HUWA WANA IQ NDOGO SANA HASA KTK UCHAMBUZI WA MASUALA YA UCHUMI,SIASA NK.????????????????????


NA WAO MARA NYINGI UBAKIA KUWA WASHUNGILIAJI TU HATA KWA JAMBO WASILOIJUA,IWE MSIBA AU FURAHA WAO HUSHANGILIA TU, IWE MVUA AU JUA WAO HUSHANGILIA TU,IWE MASIKA AU MVUA WAO HUSHANGILIA TU...
 
"Awali nilikuwa na shaka kwamba wameniitia nini lakini kumbe ilikuwa ni majadiliano ya kawaida kati yangu na ofisi ya DCI," amesema Dk Mashinji leo Jumatano Oktoba 25,2017.

Hii ni wazi kwamba sasa jeshi la polisi limeshakosa imani miongoni mwa watanzania. Imefika mahala polisi hata wakikuita tena kwa faida yako unaanza kujiandaa kuwekwa lupango na kufunguliwa kesi.
 
Amesema, "Majadiliano yalilenga kuelezana hiki kinachoendelea cha kamatakamata na je? sisi tunawaonaje na wao wanatuonaje. Pia, mambo mengine mengi."

Kumbe Polisi wamefikia hali ya wasiwasi kutokana na kukamata wanasiasa kwa wingi kupita wakati wowote tangu tupate uhuru!
 
Back
Top Bottom