Katibu Mkuu Wa CHADEMA, Vicent Mashinji atakiwa ofisi ya DCI kwa mahojiano. Baada ya mazungumzo aeleza kilichojiri

Hawa CHADEMA. wanaboa sana, hivi kweli watu waache kufanyakazi wabaki kusikia kauli zao za kijinga kijinga tu.
Mwenyezi Mungu wakati wa kuumba alifanya yafatayo.
Alipoumba-
*Mwenye akili akaumba na mjinga
*Kipofu akauba na anaeona
*Mwenye hekima akaumba na mpumbavu
Kila kitu viwili viwili na vinategemeana ukimuondoa mpumbavu hakuna mwenye hekima,kwani hekima hujidhihiri palipo na upumbavu,hali kadharika kwa mwelevu uwepo wa mjinga ndio kudhihirika kwa mwelevu.
Tafiti yagu inaniambia mjinga na mpumbavu wakianza kuchukua hatua kuondokana na hali zao za awali waelevu hugeuka wajinga na wapumbavu kupita kiwango cha mjinga na mpumbavu wa awali,yote haya husababishwa na kupaniki kuchukuliwa kwa nafasi zao.
Mjinga akielevuka mwelevu yu mashakani.
Mmechelewa sana kulitambua hilo hatima yenu iko mashakani,poleni sana nayatambua mashaka yenu lakini hamna jinsi lazima muikubali nafasi yenu mpya.
 
ifike mahali tuachane na siasa za chuki vilevile tusihusishe vyombo vya umma kuwa na maslahi ya chama fulani cha siasa.
 


Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ameeleza kilichojiri kati yake na ofisa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Dk Mashinji amesema alichotarajia kukikuta kimekuwa tofauti.

"Awali nilikuwa na shaka kwamba wameniitia nini lakini kumbe ilikuwa ni majadiliano ya kawaida kati yangu na ofisi ya DCI," amesema Dk Mashinji leo Jumatano Oktoba 25,2017.

Amesema, "Majadiliano yalilenga kuelezana hiki kinachoendelea cha kamatakamata na je? sisi tunawaonaje na wao wanatuonaje. Pia, mambo mengine mengi."

Dk Mashinji amesema wamezungumzia pia kuhusu kuendelea kushikiliwa kwa Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson.

Katibu mkuu Mashinji amesema ofisa huyo ameahidi kulifuatilia suala hilo.

"Mimi nimemweleza alichozungumza Kigaila kiko wazi na wala hakina tatizo lolote," amesema Dk Mashinji.

Mwananchi:
 
Kigaila aliotoa speech mzuri na watanzania tungekuwa na msimamo na kujielewa tungemuunga mkono Kigaila
 
Una kazi wewe!!! Ungekuwa na kazi ungepata muda wa kuandika shudu? Unajua kazi au unazisikia?
Mkuu hata hiyo afanyayo pale Corner Bar nayo ni kazi maana inamuingizia kipato kwani slogan yao ya hapakazituu anaitekeleza!
 
Ninajua ninamwisho ndiyo sababu natenda mema daima,ili mwisho wangu uwe mwema.


Mtenda mema hajisemei, isitoshe hakuna tofauti uwe Malaika, Jambazi, Muuwaji haijalishi wote mwisho wa siku mtapotea Dunia hii na kuja wengine, hii Dunia haijaanza jana!
 
Mtenda mema hajisemei, isitoshe hakuna tofauti uwe Malaika, Jambazi, Muuwaji haijalishi wote mwisho wa siku mtapotea Dunia hii na kuja wengine, hii Dunia haijaanza jana!

Kwa mtu usiye na dini kama wewe aka Mpagani maana umetokana na Chama Cha Mauaji siwezi kukubadili fikra zako ovu.Pole sana.Duniani tunapita tu
 
Kwa mtu usiye na dini kama wewe aka Mpagani maana umetokana na Chama Cha Mauaji siwezi kukubadili fikra zako ovu.Pole sana.Duniani tunapita tu


Ndiyo umelijua hilo leo kwa kila kitu kina mwisho?
 
Back
Top Bottom