Wahamiaji kutoka CHADEMA na CUF (Mollel na Mtulia) walipitishwa bila kura za maoni ndani ya CCM kugombea Siha na Kinondoni. Tukavumilia. Tukasonga mbele. Tena, kuna mpango wenye viwango wa kuwapitisha Wahamiaji wengine Mwita Waitara na Kalanga kugombea Ukonga na Monduli bila kura za maoni. Utekelezaji wa mpango umeshaanza.
Waungamkono wa mpango huo wanajificha kwenye Kanuni za Kiuchaguzi za CCM. Eti, Kamati Kuu yaweza kuondoa utaratibu wa kura za maoni. Sasa, lini na wapi Kamati Kuu ya CCM iliketi, iliamua na kuelekeza kuwa Ukonga na Monduli kusiwe na kura za maoni? Halafu, Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wengine mpo kimya tu. Kwanini?
Kura za maoni ni mchakato muhimu. Ni mchakato wa kichama na kisiasa. Lazima mgombea apimwe kukubalika kwake kuanzia kwa wanachama wa CCM wa Jimbo lake/Wilaya yake. Halafu, Kamati Kuu huidhinisha. Kura za maoni huonesha picha halisi ya mgombea mtarajiwa wa CCM katika Jimbo husika.
Ukimya huu wa viongozi wetu, huku kukiwa na malalamiko ya makada wetu wa CCM wa Monduli na Ukonga unatokana na kuwa na uhakika wa 'kushinda' chaguzi hizi za marudio? Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu yangu Dr. Bashiru Ally uko wapi? Kuna tatizo chamani!
Majibu ya Jeshi la Polisi kwa Waziri Lugola yamemuimarisha na kumjenga sana!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam