Katibu Mkuu wa CCM uko wapi? Kuna tatizo chamani!

Katibu Mkuu wa CCM uko wapi? Kuna tatizo chamani!

Wahamiaji kutoka CHADEMA na CUF (Mollel na Mtulia) walipitishwa bila kura za maoni ndani ya CCM kugombea Siha na Kinondoni. Tukavumilia. Tukasonga mbele. Tena, kuna mpango wenye viwango wa kuwapitisha Wahamiaji wengine Mwita Waitara na Kalanga kugombea Ukonga na Monduli bila kura za maoni. Utekelezaji wa mpango umeshaanza.

Waungamkono wa mpango huo wanajificha kwenye Kanuni za Kiuchaguzi za CCM. Eti, Kamati Kuu yaweza kuondoa utaratibu wa kura za maoni. Sasa, lini na wapi Kamati Kuu ya CCM iliketi, iliamua na kuelekeza kuwa Ukonga na Monduli kusiwe na kura za maoni? Halafu, Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wengine mpo kimya tu. Kwanini?

Kura za maoni ni mchakato muhimu. Ni mchakato wa kichama na kisiasa. Lazima mgombea apimwe kukubalika kwake kuanzia kwa wanachama wa CCM wa Jimbo lake/Wilaya yake. Halafu, Kamati Kuu huidhinisha. Kura za maoni huonesha picha halisi ya mgombea mtarajiwa wa CCM katika Jimbo husika.

Ukimya huu wa viongozi wetu, huku kukiwa na malalamiko ya makada wetu wa CCM wa Monduli na Ukonga unatokana na kuwa na uhakika wa 'kushinda' chaguzi hizi za marudio? Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu yangu Dr. Bashiru Ally uko wapi? Kuna tatizo chamani!

Majibu ya Jeshi la Polisi kwa Waziri Lugola yamemuimarisha na kumjenga sana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Tangazo la kuchukuwa fomu jimbo la Ukonga limebandikwa dakika 15 kabla ya deadline wilayani ilala lakini Mwita Waitara katoka karime ndani ya muda huo kawahi, kachukuwa na karejesha.

Ni heri kutokuwa na chama kuliko kukaa na waigizaji kama hawa.
 
Yule anayepinga ujenzi wa SGR kwangu ndie Nyumbu wa tanapa.
Nyumba wa Afrika tunaambiwa tunaambiwa SGR inajengwa kwa hela zetu ,kesho hiyo yake bakuli linatembea

Acha WaEurope watuite nyumbu maana hata kujenga hiyo SGR badala kutumia material ya ndani mfano chuma kutoka Mchuchuma tunatumia zaidi ya matrilion kununua chuma njee

Nyumbu hatuna akili za kutosha hatufikirii badala ya kujenga SGR kwenda Kigoma (Economic zone) tusafirishe bidhaa za Rwanda,Burundi na Congo na nchi zingine za central Afrika badala yake kwa vile Waafrika ni nyumbu kwa akili na matendo SGR unajengwa kwenda mwanza ili tusafirishe abiria

Mwafrika ni nyumbu tu naunga Mkono European Scholars
 
Kila mikataba ina masharti yake
Na hayo ni baadhi ya masharti
Ukijivua unavaa ubunge
Tuna maajabu sana yaani kama sales person nimemuiba kwenye kampuni kubwa na kumuahidi more money and a house plus car wow
 
Ambacho wewe hujui ni kuwa hiyo ni biashara kweli na inalipa sana.

Mbunge ili ahame analipwa si chini ya Mil 500 hapo Polepole lazima achukue kabisa 10% na hiyo huchukuliwa toka kwa Mbunge alielipwa,kisha Mbunge huyo hutakiwa kulipa karibu milioni 100 kwa vigogo wa chama ili wapindishe kanuni kuhakikisha anarudishwa yeye.

Hapo ndipo watu wanapigia pesa,ninyi mtaona kalipwa mil 500 lkn anaambulia kama mil 350,zingine zinagawiwa kwa wawezeshaji(wazee wa logistic)

Wapambe wa chama endeleeni kuimba Iyena iyeba ,wenye akili watengeneze pesa.
Duh
 
Uongo uko wap? Soma akina Coupland kuhusu Afrika wanasema au wanafananisha waafrika na wanyama wa porini

Ukishwa fananishwa na mnyama na akili zako ni ni sawa na wanyama akina nyumbu
Mkuu hebu acha kumtukuza mzungu kiivo ...yaan wazungu mshawaona km mungu vile
 
CCM asilia mtapata tabu sanaaaaaaaa.
 
Mkuu hebu acha kumtukuza mzungu kiivo ...yaan wazungu mshawaona km mungu vile
Ndo maana tunaingia darasani tunasoma wazungu wanavyotutathimini na kurelate na tabia zetu naunga mkono niliyosoma kuhusu Afrika wazungu wapo sahihi,tunafanya mambo ovyo ovyo sana
 
Ndo maana tunaingia darasani tunasoma wazungu wanavyotutathimini na kurelate na tabia zetu naunga mkono niliyosoma kuhusu Afrika wazungu wapo sahihi,tunafanya mambo ovyo ovyo sana
Wanaofanya mambo ya hovyo hawafiki hta 1% sasa kwanini unajumuisha watu wote?
 
Ndoto yangu ya kugombea ubunge 2020 inaanza kufifia! Kwa hali hii, kuna uwezekano mkubwa 2020 wagombea wakateuliwa toka juu bila kufuata michakato ya kura za maoni jimboni!!
 
Wahamiaji kutoka CHADEMA na CUF (Mollel na Mtulia) walipitishwa bila kura za maoni ndani ya CCM kugombea Siha na Kinondoni. Tukavumilia. Tukasonga mbele. Tena, kuna mpango wenye viwango wa kuwapitisha Wahamiaji wengine Mwita Waitara na Kalanga kugombea Ukonga na Monduli bila kura za maoni. Utekelezaji wa mpango umeshaanza.

Waungamkono wa mpango huo wanajificha kwenye Kanuni za Kiuchaguzi za CCM. Eti, Kamati Kuu yaweza kuondoa utaratibu wa kura za maoni. Sasa, lini na wapi Kamati Kuu ya CCM iliketi, iliamua na kuelekeza kuwa Ukonga na Monduli kusiwe na kura za maoni? Halafu, Katibu Mkuu wa CCM na viongozi wengine mpo kimya tu. Kwanini?

Kura za maoni ni mchakato muhimu. Ni mchakato wa kichama na kisiasa. Lazima mgombea apimwe kukubalika kwake kuanzia kwa wanachama wa CCM wa Jimbo lake/Wilaya yake. Halafu, Kamati Kuu huidhinisha. Kura za maoni huonesha picha halisi ya mgombea mtarajiwa wa CCM katika Jimbo husika.

Ukimya huu wa viongozi wetu, huku kukiwa na malalamiko ya makada wetu wa CCM wa Monduli na Ukonga unatokana na kuwa na uhakika wa 'kushinda' chaguzi hizi za marudio? Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu yangu Dr. Bashiru Ally uko wapi? Kuna tatizo chamani!

Majibu ya Jeshi la Polisi kwa Waziri Lugola yamemuimarisha na kumjenga sana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mzee Tupatupa,wewe si uko Lumbamba?Mbona unalalamika mitandaoni?Tuamini kwamba umekosa mahali pa kupeleka malalamiko yako?
 
Demokrasia imeminywa hadi ndani ya chama cha mapinduzi. Nilijua ni upinzani waliominywa kumbe ni wote, pinga uvunjaji wa demokrasia, pamoja tunaweza.
 
Ndo maana mikosi imewaandama Maishani mwenu halafu mnatafuta mchawi kumbe ninyi wenyewe, sasa wewe kubwa zima kudanganya na kujifanya CCM wakati ni Mtumwa wa Mbowe kwa nini usilaanike? Mungu hapendi uongo tubu jisafishe kuwa mkweli maishani ili upate baraka, watu kama ninyi ndo mnaoifanya chadema ilaaniwe kwa kuwa Muongo na mnafiki!
 
Waitara anaondoka chadema anadai chadema hakuna demokrasia,natamani niwepo siku moja kwenye kampeni zake nimuulize vip ulichaguliwa na nani au demokrasia gani imetumika ndani ya ccm na kukupitasha kuwa mgombea?

Waafrika chini ya jangwa la sahara hawana akili,akili zao ni sawa na nyumbu- by European scholars
Hakika mkuu
 
Back
Top Bottom