Katibu mkuu wa ccm na ufisadi wa maji tegeta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu mkuu wa ccm na ufisadi wa maji tegeta

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SG8, Feb 20, 2011.

1. SG8

SG8 JF-Expert Member

#1
Feb 20, 2011
Joined: Dec 12, 2009
Messages: 3,198
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Mh. Yusuph Makamba leo amesababisha kizaazaa maeneo ya Tegeta baada ya kujipendelea maji ya kisima huku wananchi wenzake wakikosa maji kwa muda mrefu. Wakilezea tukio hilo kwa Mwandishi wa ITV wananchi hao wamemkumbuka Marehemu Rashid Kawawa (Mungu amlaze mahala pema peponi) kwamba hakuwa na tabia kama zinazoonyeshwa na Mh. Makamba.

My take: Kama mtindo huu wa kuwaonea wananchi utaendelea siku zenu zinakaribia kufika mwisho. Hata Ben Ali na Mubarak walikuwa na tabia hizihizi, wako wapi leo?

2. apolycaripto

apolycaripto JF-Expert Member

#2
Feb 20, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 636
Likes Received: 24
Trophy Points: 35

Tatizo lako ni kuruka na ngao ya siasa hata kwenye mambo ya kijamii kama hili.Acha uchadema wewe,hapa issue ni Makamba kama mkazi na si Ccm.Kifupi Makamba kama kweli anayotenda kwa wenzie aidha kwa kutumia kofia ama ualuatani wake ni kweli,amenitia kabisa kichefuchefu.Huu ni urafi usio kuwa na macho na hata huruma katika imani anayojifanya kunukuu kila siku katika maandiko.Wananchi wamenena nafanya uchunguzi na nitamrudia kwa thread mpya nitakapo baini ukweli wa jambo hili.Kwa kifupi ''uswahili ukizidi unakuwa mwanga''.

3. Kingcobra

Kingcobra JF-Expert Member

#3
Feb 20, 2011
Joined: Jan 28, 2011
Messages: 1,008
Likes Received: 137
Trophy Points: 160
Hako kababu siku zote kanafanya mambo kwa upendeleo. Ndiyo maana kameota NDONGA usoni.

4. SG8

SG8 JF-Expert Member

#4
Feb 20, 2011
Joined: Dec 12, 2009
Messages: 3,198
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Sijui nani anayeleta siasa hapa labda umekurupuka. mimi nimemnuku Mwananchi aliyesema katibu Mkuu wa Chama chetu kisha akamtaja Makmba. Sasa mwenzangu unazungumzia Chadema, labda tuwaachie wenzetu wapime nani analeta siasa hapa.
Kwa mtazamo wangu ambao hata wewe umekubaliana ni kwamba amechukua maji yote ya kisima kwa sababu ya nafasi yake katika jamii, angekuwa mwananchi wa kawaida asingefanya hivyo.
Tunapotoa maoni yetu tusikurupuke wala ufikiri kwa kutumia matumbo yetu. Unaweza usieleweke

5. apolycaripto

apolycaripto JF-Expert Member

#5
Feb 20, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 636
Likes Received: 24
Trophy Points: 35

Nashukuru kwa kujiweka wazi,japo thread yako na ideal yako ulikuwa na lengo la kisiasa zaidi.Nasisitiza kuwa Makamba kama makamba hakuanzia ukatibu bali alianza kukaa tegeta kabla ukatibu mkuu,hivyo upuuzi wake usiwe ngao ya thread ya uchama na ufisadi.Awajibike kama yeye.Narudia kama katenda hayo,wananchi wa Tegeta wasikubali na waendelee kupambana na Dawasco kwa hujuma dhidi yao mpaka hicho kizee kisome nyakati.

6. WA MAMNDENII

WA MAMNDENII JF-Expert Member

#6
Feb 20, 2011
Joined: Jun 5, 2010
Messages: 310
Likes Received: 15
Trophy Points: 35
alaaaa! mgosi shasha hiyo ni haki kweli kujipendelea vijimaji vichache huku wtz wakisota?

7. Preta

Preta JF-Expert Member

#7
Feb 20, 2011
Joined: Nov 28, 2009
Messages: 24,113
Likes Received: 3,035
Trophy Points: 280
ameniuzi kweli...yaani ni m'binafsi sana...sijui kibabu kikoje kile.....wananchi hawana maji wewe unajipendelea peke yako.....uchawi mtupu huu

8. G

Gurtu JF-Expert Member

#8
Feb 20, 2011
Joined: May 15, 2010
Messages: 1,202
Likes Received: 5
Trophy Points: 135
Naona sasa mambo yanaanza kueleweka. kumbe aliyekinyume na CCM lazima awe Chadema! hongera.

9. apolycaripto

apolycaripto JF-Expert Member

#9
Feb 20, 2011
Joined: Feb 11, 2011
Messages: 636
Likes Received: 24
Trophy Points: 35

<br /
Vizuri kwa maana siasa zimebakia kwao,huku vyama vingine vilishatoka huko kwenye uchaguzi.Nadhani ata wewe pia ni kada.Ebu tujaribu kuiga siasa za Marekani,ukishapigwa chini,ndio imetoka hiyo.Anyway turudi kwenye hoja ya hiki kizee na issue ya water!kamekuwa customer peke yake huko na ukichunguza ata bill unaweza kuta akalipi.Nchii hii watendaji wabovu kwelikweli hasa hizi water sector ni upupu mtupu.

10. SG8

SG8 JF-Expert Member

#10
Feb 21, 2011
Joined: Dec 12, 2009
Messages: 3,198
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Sijui unaelewa unachozungumza au porojo tu! Marekani ipi unayoizungumzia wewe? Mimi ni mtumishi tu wa serikali, sikugombea nikapigwa chini wala sina status ya Makamba. Nafikiri umeamua kuwa mpiga ramli kwamba asiyeipenda SSM basi ni Chadema.

11. SG8

SG8 JF-Expert Member

#11
Feb 21, 2011
Joined: Dec 12, 2009
Messages: 3,198
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Sijui kwanini hutaki kuelewa. Kama hujaangalia taarifa ya habari shauri, but Mwananchi ndiye aliyesema katibu mkuu wa Chama na mimi na wewe tunajua ni chama gani, nongwa iko wapi? Ok tufanye lengo ni siasa ndo maana ipo kwenye jukwaa la siasa tatizo liko wapi? Kitendo si kimefanywa na Mwanasiasa?

12. Arafat

Arafat JF-Expert Member

#12
Feb 21, 2011
Joined: Nov 17, 2009
Messages: 2,582
Likes Received: 41
Trophy Points: 0
upeo wa kufikiri unaendana na avatar unayotumia, una-bahati mbaya wote unaowapenda hawakubaliki, unatenganisha vipi siasa na Jamii hata std seven hana upeo huo

13. Tiba

Tiba JF-Expert Member

#13
Feb 21, 2011
Joined: Jul 15, 2008
Messages: 4,511
Likes Received: 95
Trophy Points: 145
Naona wadau mmeanza kushambuliana kiitikadi badala ya kudeal na suala lenyewe linalozungumziwa hapa. Mleta hoja hebu tufafanulie hayo maji ya kisima Makamba ameyafanyaje mpaka wananchi walalamike? Amewazuia wengine kutumia hayo maji? Hicho kisima ni cha nani?

Nikipata majibu labda nitakuwa kwenye nafasi nzuri kuchangia.

Tiba

Loading...