Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo aeleza mazito kuelekea miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
"Chama cha Mapinduzi kinajivunia kuwa ni chama cha ukombozi na haswa kwa mataifa ya Kusini mwa
Afrika, kupitia Chama Cha Mapinduzi na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sisi ndio tumewasaidia wengine wote waliokuwa na changamoto kwenye mataifa yao."

Akizungumza katika mkutano wa mtandaoni wa 'zoom' leo Februari 4, 2021 Katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha umma wa watanzania juu ya juhudi za chama anachokiongoza katika kihakikisha Tanzania na Afrika kiujumla inatoka katika makucha ya wakoloni na hatimae kujipatia uhuru wake wa kisiasa.

Katibu Mkuu Chongolo pia, ametoa rai kwa watanzania wote kutambua namna Chama Cha Mapinduzi kimejikita katika kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa na kutumika kwa matumizi mapana ya watanzania wote katika awamu zote za uongozi chini ya Chama hicho na kuwa ndio sababu ya msingi ya kuadhimisha miaka 45 ya kuanzishwa kwake katika mkoa wa Mara kama sehemu ya kumuenzi muasisi katika uongozi wenye uadilifu na utetezi wa rasilimali na maslahi ya watanzania wote, baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ambae alitokea mkoani humo.

"Mwaka huu pia tunaadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Baba wa Taifa hayati Mwalim Julias Kambarage Nyerere, ambapo ndio kusudio letu la msingi kuleta sherehe huku za miaka 45 ya chama chetu mkoani mara Mjini Musoma" chongolo
 
Sema unajua nini Maryam...

Hapa najisikia uvivu kusoma, sijui nikupigie ili unisimulie ulichoandika...

Lakini kwa ninavyomfahamu Chongolo lazima itakuwa ameelezea masikitiko yake ya jinsi CCM na babake TANU walivyokuwa chachu ya umaskini wa kutupwa kwa Watanzania.

Nimepatia, si eti?! Manake hili lipo wazi hata kwa watoto wa Darasa la IV, seuze Chongolo!

NB: Kama nimepatia nishtue ili nisiku-call manake najisikia kuchoka choka tu hapa!
 
Umekosea pa kubwa mno
 
Back
Top Bottom