Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahm Kinana amwandikia barua Mwenyekiti wa CCM Taifa, Magufuli akiomba kujiuzulu

Kinana ilikua lazima aondoke maana hii ni awamu ingine na JPM anatakiwa awe mchaguliwa wake. Kwahio kuondoka kwake wala sio pigo kama vile upande wa pili wanavyodhania. Sasa hivi atakuja mpambanaji mwingine zaidi yake. Hivi ule upande wa pili yao wameyamaliza vipi kule dom, naona wao wana vyeo vya usultani. Hapa kazi tu.
Tunasikitika mvulana analoweza wanaume
 
20180527_051854.png


Nawasilisha bandiko hili kama lilivyowekwa huko kwenye mtandao wa kijamii wa Medium

Kutoka Dawati la Siasa Idara ya Usalama wa Taifa: Mtikisiko Ndani ya CCM: Kinana Kumuachia Chama Magufuli

Ni habari za kuthibitishwa bila chembe ya shaka kwamba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameamua kujiuzulu nafasi hiyo. Hii ikiwa ni mara ya tatu sasa katika nyakati mbalimbali. Mara zote za siku za nyuma zilikataliwa, ikiwemo mara moja ambapo barua yake ya kujiuzulu aliisoma (na kuikataa hadharani) Mwenyekiti Magufuli wakati anachukua Uenyekiti wa CCM mwaka 2016 kule Dodoma. Taarifa za uhakika tulizokusanya ni kwamba safari hii Kinana amedhamiria kuachia nafasi hiyo na hakuna ushawishi wowote utakaomgeuza.

Mtakuwa mmeona picha mbalimbali vikao anavyofanya Mwenyekiti Magufuli na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkapa, Sheni na Mangula. Madhumuni ya vikao hivyo ni kupanga namna ya kumshawishi Kinana aendelee angalau hadi kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Hadi tunaripoti jioni hii, jitihada hizo zilikuwa hazijafanikiwa.

Sababu za kujiuzulu Kinana zinaelezwa kuwa ni zilezile zilizosomwa hadharani, kwamba ametimiza kazi ya kujenga uhai wa Chama aliyoombwa na Kikwete mwaka 2012, na kazi ya kukivusha Chama kwenye mchakato mgumu wa kumpata mgombea Urais wa CCM, na kazi kubwa ya kuendesha uchaguzi na kuleta ushindi kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.

Hata hivyo, kuna sababu za ziada ambazo hazitajwi hadharani ambazo ni pamoja na yeye kuvunjika moyo kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa bila kufuata Katiba na taratibu za Chama ikiwemo kuwafukuza na Makatibu wa Wilaya na Mikoa 78 na kuwateua wengine wapya bila kumshirikisha wala kushirikisha vikao, kutoitishwa kwa vikao, kuvunjwa Katiba ya Chama mara kwa mara (ikiwemo kupata Wagombea Ubunge wa Siha na Kinondoni bila mchakato wa Chama wala vikao), na pia ngazi za matawi, Kata, Wilaya na Mikoa kuondolewa nguvu za kiuchumi kwenye miradi yao na Chama kukosa sauti na kuwekwa mfukoni mwa Serikali, na viongozi wa Chama wa Wilaya na Mikoa kupuuzwa.

Kuondoka kwa Kinana kwenye CCM ni pigo kubwa kwenye Chama hicho kwani anajulikana na kuheshimika kwa nguvu yake na ushawishi wake mkubwa ndani ya Chama hicho. Pia Katibu Mkuu huyo ni mmoja wa viongozi wachache katika CCM wanaoaminiwa na kuheshimiwa na Watanzania wengi. Wanachama wengi wa CCM waliokuwa wanasikia tetesi zake za kuondoka kwake wamevunjika moyo na kukata tamaa kwani Kinana aliaminika kwamba ni nguzo kuu ya kuwaunganisha wana-CCM wote. Hata hivyo, baadhi yao wamebaki na matumaini kwamba ataendelea kuwa na nguvu na ushawishi hata akiwa nje ya uongozi wa Chama.

Kuondoka kwa Kinana kunaifanya CCM kuingia katika zama mpya za kutokuwepo katika safu zake za uongozi vijana wa zamani waliolelewa na kukulia ndani ya Chama (Kikwete, Lowassa, Mkuchika, Jaka Mwambi, Chiligati, Kinana, Mohammed Seif Khatib na wengineo). Pia vijana wapya waliolelewa na kukulia ndani ya Chama (E.Nchimbi, Nape, A.Makala, J.Makamba na wengineo) nao wakiwa nje ya safu za uongozi wa Chama. Jambo hili wanaamini wajuzi wa siasa za CCM linaleta shaka juu ya mwendelezo wa kiuongozi na kimalezi ya Chama, hasa pale wanaopewa sauti kwenye Chama ni wale ambao hawakijui (Humphrey Polepole, nk).

Bado haijafahamika kama Kinana atashiriki katika kutafuta ushindi wa Chama mwaka 2020. Pia, kazi kubwa sasa aliyonayo Mwenyekiti ni kutafuta mrithi wa Kinana ambaye ataweza kuvaa viatu vyake, na kuwa na ushawishi alionao Kinana ndani ya Chama, nje ya nchi, kwa viongozi wa dini, kwa Wabunge, kwa Wazanzibari na kwa sekta binafsi.

— — — — — — -Mwisho — — — — — — — — -


Chanzo :


Personally niko very disturbed maana naona kama wale wanaokijua Chama na mbilinge zake hawapo zimebaki sura mpya tupu.
 
What is so spesho kwa huyu mzee ambaye awam ya IV amehusishwa sana na Ujangili na Meli yake ikihusishwa kubeba nyara za taifa na akakiri kuwa ni kweli ilibeba ila mzigo dnio aliukataa..............
 
Jana niliisoma hii article huko [HASHTAG]#Medium[/HASHTAG]. Kuna kaukweli kanakuja juu ya saga nzima ya Mzee kujiudhulu.
 
What is so spesho kwa huyu mzee ambaye awam ya IV amehusishwa sana na Ujangili na Meli yake ikihusishwa kubeba nyara za taifa na akakiri kuwa ni kweli ilibeba ila mzigo dnio aliukataa..............
Hahaha and who's clean
 
Siasa bhana, uongo mtupu, wanadanganya umma wakati kila kitu kiko wazi kwa nini anajiuzulu! Hapo atafutwe mkoromije mmoja kujaza nafasi hiyo!
 
Siasa bhana, uongo mtupu, wanadanganya umma wakati kila kitu kiko wazi kwa nini anajiuzulu! Hapo atafutwe mkoromije mmoja kujaza nafasi hiyo!
Kuna kijiji kidogo Uingereza kinaitwa Santon bridge kila mwaka huwa kuna mashindano ya kusema uongo na mtu hupewa dakika tano kusema uongo.
Lakini politicians na lawyers hawaruhusiwi kwenye mashindano hayo kwani wanajua sana uongo.
 
.Maajabu ya nyumbu kumuona Kinana dhahabu. Mmesahau Nyumbu Mkuu yule Mchungaji wenu alivyomtukana na kumkashifu?
 
Sasa ccm Bara uongozi ni 95% wakristo watupu.chama hichi sasa kimechukua rasmi mikoba ya kile walicho kuwa wakikituhumu cuf kuwa chama cha kidini.
Waislam sasa hawana chao tena huko.
 
What is so spesho kwa huyu mzee ambaye awam ya IV amehusishwa sana na Ujangili na Meli yake ikihusishwa kubeba nyara za taifa na akakiri kuwa ni kweli ilibeba ila mzigo dnio aliukataa..............
Mmekuwa watu wa ajabu sana na chama chenu,mpaka mtu atoke au ajiengue kwenye cheo ndio mnaanza kumjadili maovu yake?ndio hapo mnatuaminisha kweli hicho ni kijiwe cha majambazi
 
Back
Top Bottom