Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahm Kinana amwandikia barua Mwenyekiti wa CCM Taifa, Magufuli akiomba kujiuzulu

Ili iwe pigo zaidi,na kuonesha ccm haina usawa aamie CHADEM,Na atangaze kumuunga mkono lisu 2020.

Mkuu hapo kwenye "aamie" ni kuamia kama kule kwa ndege walioko kwenye shamba la mpunga au ulitaka kusemaje
 
yani huyu mpiga zumari anaboa na vijihabari vyake vya kidaku
Anajifanya ana nyeti. Kama ana nyeti zaidi ya kupiga zumari kwanini asiweke viambatanisho? Hii habari ya nimezipata kutoka ndani ni mgongo wa kuficha uongo wake. Kama anataka kuwa kama Julian Asange ama NYT wenzake wanakua na uthibitisho wa ku back up habari zao huyu kila kukicha nyeti nyeti. Anajua kuna watu wanamsikiliza waliopigwa na maisha ama wafuasi wa wezi watazifurahia hizi habari za kizushi.

Chahali anika barua ya kinana ya kujiuzuru sisi kina Thomaso tukuamini.
 
Sidhani kama kuna sababu ya kuwa na tashwishwi yoyote kwa mzee ambaye alitakiwa ameshastaafu kama Kinana anapoamua kujipumzisha. Kuna vijana wengi wenye nguvu, na akili ambao wakipewa nafasi hiyo watafanya tu vizuri. Kwa mfano Prof. Kitila Mkumbo mbali na ugeni wake katika Chama, lakini ni mmoja wa visionary leaders na anaweza akawa wa manufaa makubwa kuliko hata huyo mzee
Utu uzima dawa...huyo kitila juzi tu alikuwa anaiponda ccm leo ukampe nafasi nyeti namna hiyo wazee wa ccm hawatokubali...ni mtazamo tu.
 
Anajifanya ana nyeti. Kama ana nyeti zaidi ya kupiga zumari kwanini asiweke viambatanisho? Hii habari ya nimezipata kutoka ndani ni mgongo wa kuficha uongo wake. Kama anataka kuwa kama Julian Asange ama NYT wenzake wanakua na uthibitisho wa ku back up habari zao huyu kila kukicha nyeti nyeti. Anajua kuna watu wanamsikiliza waliopigwa na maisha ama wafuasi wa wezi watazifurahia hizi habari za kizushi.

Chahali anika barua ya kinana ya kujiuzuru sisi kina Thomaso tukuamini.
kabisa kila siku nyeti nyeti uongo mtupu mwanaume mzima amekalia udaku
 
20180527_051854.png

Nawasilisha bandiko hili kama lilivyowekwa huko kwenye mtandao wa kijamii wa Medium

Kutoka Dawati la Siasa Idara ya Usalama wa Taifa: Mtikisiko Ndani ya CCM: Kinana Kumuachia Chama Magufuli

Ni habari za kuthibitishwa bila chembe ya shaka kwamba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameamua kujiuzulu nafasi hiyo. Hii ikiwa ni mara ya tatu sasa katika nyakati mbalimbali. Mara zote za siku za nyuma zilikataliwa, ikiwemo mara moja ambapo barua yake ya kujiuzulu aliisoma (na kuikataa hadharani) Mwenyekiti Magufuli wakati anachukua Uenyekiti wa CCM mwaka 2016 kule Dodoma. Taarifa za uhakika tulizokusanya ni kwamba safari hii Kinana amedhamiria kuachia nafasi hiyo na hakuna ushawishi wowote utakaomgeuza.

Mtakuwa mmeona picha mbalimbali vikao anavyofanya Mwenyekiti Magufuli na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkapa, Sheni na Mangula. Madhumuni ya vikao hivyo ni kupanga namna ya kumshawishi Kinana aendelee angalau hadi kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Hadi tunaripoti jioni hii, jitihada hizo zilikuwa hazijafanikiwa.

Sababu za kujiuzulu Kinana zinaelezwa kuwa ni zilezile zilizosomwa hadharani, kwamba ametimiza kazi ya kujenga uhai wa Chama aliyoombwa na Kikwete mwaka 2012, na kazi ya kukivusha Chama kwenye mchakato mgumu wa kumpata mgombea Urais wa CCM, na kazi kubwa ya kuendesha uchaguzi na kuleta ushindi kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.

Hata hivyo, kuna sababu za ziada ambazo hazitajwi hadharani ambazo ni pamoja na yeye kuvunjika moyo kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa bila kufuata Katiba na taratibu za Chama ikiwemo kuwafukuza na Makatibu wa Wilaya na Mikoa 78 na kuwateua wengine wapya bila kumshirikisha wala kushirikisha vikao, kutoitishwa kwa vikao, kuvunjwa Katiba ya Chama mara kwa mara (ikiwemo kupata Wagombea Ubunge wa Siha na Kinondoni bila mchakato wa Chama wala vikao), na pia ngazi za matawi, Kata, Wilaya na Mikoa kuondolewa nguvu za kiuchumi kwenye miradi yao na Chama kukosa sauti na kuwekwa mfukoni mwa Serikali, na viongozi wa Chama wa Wilaya na Mikoa kupuuzwa.

Kuondoka kwa Kinana kwenye CCM ni pigo kubwa kwenye Chama hicho kwani anajulikana na kuheshimika kwa nguvu yake na ushawishi wake mkubwa ndani ya Chama hicho. Pia Katibu Mkuu huyo ni mmoja wa viongozi wachache katika CCM wanaoaminiwa na kuheshimiwa na Watanzania wengi. Wanachama wengi wa CCM waliokuwa wanasikia tetesi zake za kuondoka kwake wamevunjika moyo na kukata tamaa kwani Kinana aliaminika kwamba ni nguzo kuu ya kuwaunganisha wana-CCM wote. Hata hivyo, baadhi yao wamebaki na matumaini kwamba ataendelea kuwa na nguvu na ushawishi hata akiwa nje ya uongozi wa Chama.

Kuondoka kwa Kinana kunaifanya CCM kuingia katika zama mpya za kutokuwepo katika safu zake za uongozi vijana wa zamani waliolelewa na kukulia ndani ya Chama (Kikwete, Lowassa, Mkuchika, Jaka Mwambi, Chiligati, Kinana, Mohammed Seif Khatib na wengineo). Pia vijana wapya waliolelewa na kukulia ndani ya Chama (E.Nchimbi, Nape, A.Makala, J.Makamba na wengineo) nao wakiwa nje ya safu za uongozi wa Chama. Jambo hili wanaamini wajuzi wa siasa za CCM linaleta shaka juu ya mwendelezo wa kiuongozi na kimalezi ya Chama, hasa pale wanaopewa sauti kwenye Chama ni wale ambao hawakijui (Humphrey Polepole, nk).

Bado haijafahamika kama Kinana atashiriki katika kutafuta ushindi wa Chama mwaka 2020. Pia, kazi kubwa sasa aliyonayo Mwenyekiti ni kutafuta mrithi wa Kinana ambaye ataweza kuvaa viatu vyake, na kuwa na ushawishi alionao Kinana ndani ya Chama, nje ya nchi, kwa viongozi wa dini, kwa Wabunge, kwa Wazanzibari na kwa sekta binafsi.

— — — — — — -Mwisho — — — — — — — — -

Chanzo :

Wewe msomi na mwana usalama wa Taifa utachukua tweet na kuipeleka mahakamani kama ushahidi wako?. Sasa hivi kila kitu nilichokisoma huko nyuma kuhusu Lowasa na Chadema ulichokiandika sitaviamini kama source zako zenyewe ni facebook na tweets
 
kabisa kila siku nyeti nyeti uongo mtupu mwanaume mzima amekalia udaku
Mrema alisifiwa sababu nyeti zake kutoka TISS zilikua na mshiko. Pia zilimfanya Mbilinyi ajiuzulu sababu zilikua za ukweli. Huyu namuita mpiga zumari huo uandishi wake wa udaku utamsaidiia kupata likes kutoka kwa wadaku wenzake humu JF.
 
haswaaaa:p:p:p
 
haswaaa:p:p:p:p halafu wadaku wenzie wa JF nao kama wameanza kumshitukia likes sio za kivile
 
Back
Top Bottom