Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa ACT—Wazalendo ashikiliwa na Jeshi la Polisi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
Katibu Mkuu na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ndugu Ado Shaibu amekamatwa na Polisi ili kuzuiwa asihudhurie Mkutano wa Tundu Lissu unaofanyika Jimboni Kwake.

Ndugu Ado Shaibu natuhumiwa kutumia Kampeni zake kuhamasisha wakulima wa korosho kugomea Mfumo wa Stakabadhi Ghalani mpaka ufanyiwe marekebisho, pamoja na kuhamasisha Wakulima kujilinda dhidi ya Tembo wanaovamia Mashamba na Makazi yao.

Vitendo vya Jeshi la Polisi kuwasumbua, kuwapotezea muda na kuwadhibiti Viongozi wa Vyama vya Upinzani kufanya siasa vimekithiri mno katika kipindi hichi cha uchaguzi. Vitendo hivi vimeutia dosari uchaguzi huu na katu havikubaliki wala havivumiliki.

ado.jpg

Katibu Mkuu akizungumza na muathirika wa Uvamizi wa Tembo katika Mashamba.

adooooo.jpg

Katibu Mkuu akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.
 
Polisi wanazidi kumpaisha kisiasa asanteni Sana policcm Kwa kazi kubwa mnayojitolea ya kuwapandisha Chati wapinzani
 
Ado ratibu mkutano wa kuwaondoa Zitto na Seif kwa usaliti wao dhidi ya mgombea urais
Katibu Mkuu na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ndugu Ado Shaibu amekamatwa na Polisi ili kuzuiwa asihudhurie Mkutano wa Tundu Lissu unaofanyika Jimboni Kwake.

Ndugu Ado Shaibu natuhumiwa kutumia Kampeni zake kuhamasisha wakulima wa korosho kugomea Mfumo wa Stakabadhi Ghalani mpaka ufanyiwe marekebisho, pamoja na kuhamasisha Wakulima kujilinda dhidi ya Tembo wanaovamia Mashamba na Makazi yao.

Vitendo vya Jeshi la Polisi kuwasumbua, kuwapotezea muda na kuwadhibiti Viongozi wa Vyama vya Upinzani kufanya siasa vimekithiri mno katika kipindi hichi cha uchaguzi. Vitendo hivi vimeutia dosari uchaguzi huu na katu havikubaliki wala havivumiliki.

View attachment 1610412

Katibu Mkuu akizungumza na muathirika wa Uvamizi wa Tembo katika Mashamba.

View attachment 1610420

Katibu Mkuu akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.
 
Anapiga kampeni kisayansi keshammaliza mpinzani wake Hassani Myao chaguo la Kassimu Majaliwa ila sio chaguo la wanatunduru.Ado Shaibu my classmate.Pambana wameshalegea.
 
Natumai CDM watampa ushirikiano endapo ni kinara huko.
Wapi #Mdudu Chadema kwa sauti ya Nyoshi, kadema na Mbowe hawana muda ana makamanda wanaosweka ndani kwa "ujinga wao" wa kukipigania chama, yule dogo wa jana aliyetumwa kupiga shoti kwenye mkutano wa Arusha sasa hivi yupo anahangaika yeye tu na wazazi wake!
 
Back
Top Bottom