Katibu Mkuu TAMISEMI 'amfunga breki' DC Polepole

Katibu Mkuu TAMISEMI 'amfunga breki' DC Polepole

Kwani hao wafanyibiashara wanakusanya hayo mapato kwa niaba ya halimashauri?Kama sio Katibu haoni kwamba anaikosesha halimashauri mapato?Na hata kama hao wafanyibiashara wanakusanya mapato kwa niaba ya serikali labda DC kaona kuna ujuaji.Dah,pole zake Humphrey,siasa ni ngumu sana.Kiutendaji hii inakatisha tamaa sana.Humprey aachie ngazi tu,hatawezana na waswahili hao.
Wanakusanya kwa niaba ya halmashauri. Lazima mkataba uheshimiwe!
 
Wanakusanya kwa niaba ya halmashauri. Lazima mkataba uheshimiwe!
Uko sahihi sana Mkuu. Kampuni ya Majimoto,ya wafanyabiashara haohao,ina mkataba wa pango na mmiliki halali wa eneo ambaye ni Kiwanda cha Urafiki. DC Polepole ametumia ubabe tu kutwaa eneo hilo. Amewamwagia majigambo na nyodo nyingi wafanyabiashara hao.

Mzee Tupatupa
 
Hapo ndipo penye shida.Mikataba yote iliyoingiwa kwenye awamu ya nne ni utata mtupu.Kwa sababu hiyo kwa maslahi ya nchi hasa ukizingatia kwamba kilichokuwa kinaendelea ni ulaji mtupu, ni lazima mkataba huo uvunjwe.Kwa taswira hii napata picha kwamba Katibu Mkuu Tamisemi naye ana maslahi katika dili hilo.Atumbuliwe tu.
Wanakusanya kwa niaba ya halmashauri. Lazima mkataba uheshimiwe!
 
Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa,Mhandisi Mussa Iyombe amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole kuacha utaratibu wa wafanyabiashara wa Soko la Ndizi Mabibo uendelee.

Katibu Mkuu Iyombe ametoa agizo hilo jioni ya leo alipokutana na wawakilishi wa wafanyabiashara wa soko hilo ofisini kwake. Akitoa agizo hilo kupitia kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo,Katibu Mkuu Iyombe ametaka utaratibu wa kukusanya ushuru na ulipaji kodi uliokuwepo uendelee.

Katibu Mkuu Iyombe amesema kuwa kama kutakuwa na haja ya mabadiliko au maboresho yoyote,wafanyabiashara wahusishwe. DC Polepole 'alilichukua kimabavu' soko la Mabibo na kuanza kukusanya mapato sokoni hapo kupitia watumishi wa Halmashauri bila kujali uwepo wa Kampuni ya Majimoto ya wafanyabiashara hao iliyopangishwa eneo hilo na Kiwanda cha Urafiki,mmiliki wa eneo husika.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hivi ni tangu lini dc akawa mkusanya mapato ya serikali?hii nchi ni zaidi ya tuijuwavyo
 
Ndio maana Hamphrey Polepole alitoa maoni mazuri sana katika makongamano ya Rasimu ya Warioba kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana kazi. Hivi vyeo vifute. Kwa nini Raisi wetu mpendwa hataki kufuata ushauri wa HampreyPolepole?
Naona unamtafuta cha moyoni polepole,unataka watoto wake wakose ada?
 
Nchi hii imekuwa kama shule kila mwalimu anafundisha somo lake kwa wanafunzi wale wale na lengo ni moja tu kufaulisha mitihani na sio kumjenga mwanafunzi kuelewa somo husika
Ccm wanachohitaji ni kuwalaghai wananchi ili wapate kura tu
 
pole pole ali tweet akisema anaona shubiri tu kuendelea na ukuu wa wilaya
 
Polepole amepata pigo la Mwenyezzi Mungu kwa usaliti wake amekaa na mkuu wa mkoa anayemuogopa asije akapewa yeye ukuu wa mkoa kwa sababu kichwani mwake hana mipango sasa wanamkandamiza amebaki kulalama facebook wanajifaanya hawaoni hilo ndilo tunda la kusaliti wananchi na kutukana watu wazima bado kufa tu kwa sasa ni very irrelevant hawezi hata sema kitu channel ten watu wakamsikiliza
na hivi wamekaa mkao wa kuchimbana na kutafutana na yule mpenda kiki aliyempiga makofi warioba.

natabiri mpenda kiki ataandika barua ndeeefu kuomba polepole afukuzwe kazi,na atafukuzwa na kubambikwa makorokocho,na hapo ndipo mwanzo wa mwisho utakuja
 
Hapo ndipo penye shida.Mikataba yote iliyoingiwa kwenye awamu ya nne ni utata mtupu.Kwa sababu hiyo kwa maslahi ya nchi hasa ukizingatia kwamba kilichokuwa kinaendelea ni ulaji mtupu, ni lazima mkataba huo uvunjwe.Kwa taswira hii napata picha kwamba Katibu Mkuu Tamisemi naye ana maslahi katika dili hilo.Atumbuliwe tu.
Tatizo hii sanaa ya "utumbuzi" mumeibeba vibaya, mkataba kama una tatizo au kama wenyewe mnavyoita dili, kuna taratibu za kushughulikia! Zifuatane tu hizo taratibu!
 
Mhe DC tukenjengee soko kubwa na la kisasa maeneo ya kibamba ili tuongeze mapato kwenye halmashauri ya Ubungo.

Wilaya ya Ubungo ndio Wilaya pekee ktk mkoa wa Dsm inaonekana bado iko nyuma kimaendeleo lkn inayo maeneo makubwa na mazuri kuvutia uwekezaji, kilicho baki na kuhamasisha wawekezaji na kutenga maeneo.

Kuanzia Luguruni hadi Kiluvya( along Morogoro road) bado kuna maeneo mazuri ya uwekezaji na hivyo kupunguza msongamano katikati ya mji, tutumie fursa!
 
Back
Top Bottom