Katibu mkuu NCCR MAGEUZI Mkoa wa Arusha ajiunga CHADEMA

Mtoa mada umetudanganya kwa kuwa ndani ya nccr hakuna cheo au nafasi ya katibu mkuu wa nccr mkoa wa manyara, hivyo kuhusu mada yako hapa ni mbwembwe tu, pia hiyo idadi ya wananchama 100 ni usanii mtupu kwa kuwa huyo jamaa wa monduli alipogombea udiwani mwaka huu tarehe 2/10/2011 alipata kura 1 tu kwa ticket ya nccr ambayo inadhaniwa kuwa ni ya kwake, sasa swali la kujiuliza alipata wapi hao watu 100 wa kumfuata yeye. Ina maana na Cdm mnafanya usanii siku hizi wa kupokea matapeli, jiangalieni
 
Gazeti la Habari Leo

KATIBU Mwenezi wa Chama cha NCCRMageuzi wa Mkoa wa Arusha, James Ndarivoi, amejiuzulu uongozi, akipinga kufukuzwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.

Katibu huyo pia amejiunga na Chadema, kwa madai kwamba ndicho chama pekee chenye nguvu na hoja za ukweli kuhusu upinzani, kikilinganishwa na vyama vingine vya upinzani.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Ndarivoi alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo, aliwasiliana na viongozi wake wa makao makuu kutaka kufahamu kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR-Mageuzi, kiliwakilishwa na wajumbe gani, kwani wa Arusha hawakuitwa kwenye kikao hicho, lakini alikatiwa simu.

“Sasa kama wanakata simu wanafahamu ni kosa wamelifanya; huo uamuzi wa kumfukuza huyu
mbunge aliyekuwa analeta chachu katika chama umefanywa kwa hila na umetushtua na kutusikitisha, kwa sababu ni batili na umefanywa na wachache kwa maslahi binafsi bila wajumbe wa mikoani,” alisema Ndarivoi.

Ndarivoi aliendelea kusema kuwa Kafulila alikuwa na haki ya kuhoji kuhusu ruzuku inayoishia
makao makuu, ila kwa sababu ya ufisadi wa watu wachache, hawakutaka kuhojiwa hilo na kuamua kumtimua.

Alisema yeye na jopo la wanachama zaidi ya 1,000 wa mkoa wa Arusha, wanatarajia kuikana
NCCR-Mageuzi ili kupingana na uamuzi huo.

Aidha, alielezea kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini, kwani badala ya kujenga demokrasia komavu na upinzani imara, wanadidimiza kwa kujipendekeza CCM au kwa maslahi binafsi.
 
ila mkuu ndiyo source yenyewe ,sijapata habari hii popote zaidi ya hapo.((Na mmiliki wa wahiyo radio i heard ni Ndesamburo)).

Na mmiliki wa wahiyo radio i heard ni Ndesamburo!

Mkubwa!

Usingeiweka hiyo! Hebu wasubirie sasa watakavyoanguka na maneno yao mbofu mbofu!

Hongera sana Katibu kwa maamuzi mazuri yasiyo na vishaushi zaidi!
Hakika wengi watabadilika!
 
Back
Top Bottom