Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar asisitiza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi

G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
43
95
"Niombe tu kwamba, pale inapotokea mwanaume na mwanamke wamelingana vigezo katika nafasi fulani ni vyema nafasi hiyo akapewa mwanamke kwa sababu mda mrefu tumekuwa tukiwekwa nyuma kutokana na mfumo uliokuwepo."

"Mimi sio muumini wa kumpa mwanamke fursa wakati hana uwezo, lazima awe na uwezo kwanza na imeonekana wanawake wanapopewa nafasi hizi wala hawahitaji kubebwa, wakipewa hizi nafasi wanaziweza"

"Na kwenye hili naomba nisisitize. Akifeli mwanamke kwenye nafasi aliyopewa achukuliwe kama yeye mwenyewe na isichukukiwe kwamba ni jamii nzima ya wanawake imefeli, kwa sababu ipo hiyo akifeli utasikia wanawake bana wapo wanavuruga tu wanakati mwanaume akifeli na wanafeli kila siku haionekani kama jamii nzima ya wanaume kwamba wamefeli. Kwahiyo vitu hivi tusiwe na 'double standard' wakati wa kujaji.

"Kwahiyo akifeli mwanamke tujue yeye amefeli kama 'individual' basi wengine tuendelee kuwapa fursa kwa sababu sio wote waliofeli." - Eng. Zena Ahmed Said, Katibu Mkuu Kiongozi na katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar. #MwanamkeNiKiongozi.

IMG-20210214-WA0005.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom