Katibu Mkuu CHADEMA: Kiongozi lazima awe na maono, hasa mwenye nafasi ya juu kama Rais

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,259
2,000
Kiongozi lazima awe na maono, hasa mwenye nafasi ya juu kama Rais. Fikra zake lazima ziwe pana na asiishi kama karani.

Binti mwanafunzi kapata mimba ya utotoni anaondolewa shule. Anaenda kujifungua na kuleta Mtanzania mwingine/wengine. Anaambiwa hawezi kusoma tena labda aende VETA, na huko VETA hawakusaili kama huna cheti walau cha form 4!

Binti ana opt kuwa mama lishe ili alee mtoto, huku mzazi mwenzie akiwa jela miaka 30! Pamoja na Karama zote ambazo Mwenyezi Mungu kamjalia...hapo ndo mwisho wake!

Kwangu mimi, kauli ya Rais kuhusu Mimba kwa Wanafunzi ni sawa na "hukumu ya kifo kwa kosa la wizi wa kuku"

Tusimwangalie huyu binti katika umri wake wa miaka 16, 17 mpaka 22 anapopata mimba bali tumwangalie kwa ukamilifu wake mpaka kwenye "Life Expectancy yake ambayo ni miaka 62 kwa Tanzania"

Kwa kumzuia kwenda shule haumkomoi yeye na wala hauzuii mchezo huu kwani zaidi ya 70% ya Watanzania wanaishi vijijini na 39% wapo katika umaskini uliokithiri. Hawajui maana na Elimu na umuhimu wake. Hivyo tuna kazi ya kufanya watambue kwanza maana ya Elimu.

Mheshimiwa Rais atakuwa shahidi wa maisha ya kijijini na hata umuhimu wa Elimu. Isingekuwa Elimu asingeweza hata kuwa Mwalimu wa Kemia na pia anajua maisha yalivyo magumu kijijini. Hebu tuwe binadamu kidogo na kuwawezesha hawa mabinti ili watoe mchango wa maendeleo kwa Taifa.

Bado naamini kupata Elimu ni Haki ya kila mmoja wetu na hata kama ni mfungwa!
 
Dundo_Boy

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,464
2,000
Vijijini hakuna elimu??... Ndio sababu ambayo inawafanya wale wa vijijini kupata mimba?.

Mimi nadhani hii kauli ameitoa maana watangulizi wake hawakuwahi kuitolea ufafanuzi isipokuwa walikuwa wakiitendea kwa vitendo. Sio lazima urudi kusoma serikalini.... Wewe ukipata mimba rudi nyumbani zaa, endelea na elimu yako ktk shule za private ambazo utakuwa unajilipia wewe binafsi na wazazi wako. Hapo sidhani kama Rais amemaanisha kwamba akipata mimba ndio asisome tena hadi kifo...big NO!.
Elimu vijijini nadhani wana mikakati ya kuinua elimu huko......hilo linajulikana. Ila ni bora umtishe Mtoto na Mzazi wake ili wawe makini.... Ili likitokea hata wakisamehewa inakuwa sio mbaya...kuliko uje hadharani useme akipata mimba atazaa alafu arudi kuendelea na shule...hapo utakuwa unabomoa na sio kujenga!!
Mm binafsi nampongeza sana Rais maana anafanya mambo kwa uwazi. Haya yote tulikuwa hatuambiwi...ila ukifanya kosa huko mahakamani unasomewa hizo adhabu....hongera JPM....tuendelee kujitambua
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,119

Unatetea nini ujinga mtupu? Kwa nini asisome serikalini?
 
zimwimtu

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
1,989
2,000
jpm anaendelea kuwachezesha upinzani kama toys! yeye anabadilisha santuri tu wao ni kucheza. wanasubiri aweke mziki gani nao wabadili style ya unenguaji.

kama jpm asingeongelea kuhusu wanafunzi wanaopata mimba (ambalo lilishajadiliwa bungeni na kuhitimishwa kwamba hawataruhusiwa kuendelea na masomo) leo mashinji angezungumza nini?????
 
Mtambwe

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
711
1,000
Vijijini hakuna elimu??... Ndio sababu ambayo inawafanya wale wa vijijini kupata mimba?.

Mimi nadhani hii kauli ameitoa maana watangulizi wake hawakuwahi kuitolea ufafanuzi isipokuwa walikuwa wakiitendea kwa vitendo. Sio lazima urudi kusoma serikalini.... Wewe ukipata mimba rudi nyumbani zaa, endelea na elimu yako ktk shule za private ambazo utakuwa unajilipia wewe binafsi na wazazi wako. Hapo sidhani kama Rais amemaanisha kwamba akipata mimba ndio asisome tena hadi kifo...big NO!.
Elimu vijijini nadhani wana mikakati ya kuinua elimu huko......hilo linajulikana. Ila ni bora umtishe Mtoto na Mzazi wake ili wawe makini.... Ili likitokea hata wakisamehewa inakuwa sio mbaya...kuliko uje hadharani useme akipata mimba atazaa alafu arudi kuendelea na shule...hapo utakuwa unabomoa na sio kujenga!!
Mm binafsi nampongeza sana Rais maana anafanya mambo kwa uwazi. Haya yote tulikuwa hatuambiwi...ila ukifanya kosa huko mahakamani unasomewa hizo adhabu....hongera JPM....tuendelee kujitambua
Rafiki yangu naona unazungumza kama kwama kwamba uko usingizini. Unafikiri ni watanania wote wenye uwezo wa kulipia Elimu?
Au wewe ndio yule mtoto wa mfalme alie muuliza mama yake watu wanaandamana kwa nini? akaambiwa sababu hawana Mkate, kwa vile yeye hajui kabisa kwamba binaadamu anaweza kuwa na shida, akajibu inamaana kwa Leo moja hawawezi kula mayai.
 
tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,833
2,000
Gambe ya Kienyeji haijawahi kuchangia ukuaji wa uchumi.
Lawama zimfikie baba fulani kwa kutuletea Gambe ya kienyeji.
 
The Stig

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,117
2,000
Ukishakuwa na cheo kikubwa kuliko wenzako, lazima uwe mzito kidogo kutoa maamuzi. Unatakiwa pia utambue kuwa wewe ni kimbilio la mwisho la watu wako. Hata kama unataka kufanyiza, ni bora umtume mmoja wa viranja wako afanyize, ili hata ikibidi uweze kutengua uamuzi husika. Ukiwa kiongozi halafu ukaumiza mtu, unakuwa haujaacha kimbilio. Mfano wa pressure cooker unahusika hapa - valve ikiharibika, maji yatachemka mpaka pressure cooker italipuka kama bomu.
 
mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,048
2,000
Hili ni andiko la Dr Mashinji au! Mbona hakuna kinachomtambulisha zaidi ya kichwa cha habari?

Anyway,
Ni mawazo yake tunapaswa kuyaheshimu.
Kiongozi lazima awe na maono, hasa mwenye nafasi ya juu kama Rais. Fikra zake lazima ziwe pana na asiishi kama karani.

Binti mwanafunzi kapata mimba ya utotoni anaondolewa shule. Anaenda kujifungua na kuleta Mtanzania mwingine/wengine. Anaambiwa hawezi kusoma tena labda aende VETA, na huko VETA hawakusaili kama huna cheti walau cha form 4!

Binti ana opt kuwa mama lishe ili alee mtoto, huku mzazi mwenzie akiwa jela miaka 30! Pamoja na Karama zote ambazo Mwenyezi Mungu kamjalia...hapo ndo mwisho wake!

Kwangu mimi, kauli ya Rais kuhusu Mimba kwa Wanafunzi ni sawa na "hukumu ya kifo kwa kosa la wizi wa kuku"

Tusimwangalie huyu binti katika umri wake wa miaka 16, 17 mpaka 22 anapopata mimba bali tumwangalie kwa ukamilifu wake mpaka kwenye "Life Expectancy yake ambayo ni miaka 62 kwa Tanzania"

Kwa kumzuia kwenda shule haumkomoi yeye na wala hauzuii mchezo huu kwani zaidi ya 70% ya Watanzania wanaishi vijijini na 39% wapo katika umaskini uliokithiri. Hawajui maana na Elimu na umuhimu wake. Hivyo tuna kazi ya kufanya watambue kwanza maana ya Elimu.

Mheshimiwa Rais atakuwa shahidi wa maisha ya kijijini na hata umuhimu wa Elimu. Isingekuwa Elimu asingeweza hata kuwa Mwalimu wa Kemia na pia anajua maisha yalivyo magumu kijijini. Hebu tuwe binadamu kidogo na kuwawezesha hawa mabinti ili watoe mchango wa maendeleo kwa Taifa.

Bado naamini kupata Elimu ni Haki ya kila mmoja wetu na hata kama ni mfungwa!
 
Dundo_Boy

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,464
2,000
Rafiki yangu naona unazungumza kama kwama kwamba uko usingizini. Unafikiri ni watanania wote wenye uwezo wa kulipia Elimu?
Au wewe ndio yule mtoto wa mfalme alie muuliza mama yake watu wanaandamana kwa nini? akaambiwa sababu hawana Mkate, kwa vile yeye hajui kabisa kwamba binaadamu anaweza kuwa na shida, akajibu inamaana kwa Leo moja hawawezi kula mayai.
Hapa na ndg, kwahiyo wewe unatetea warudi shule ileile ya serikali ili wamalizie??, private kuna masharti yake ambayo yapo tofauti na haya ya shule za serikali.

Inamaana uwezo wa kupata elimu bure alikuwa nao, na uwezo wa kupata mimba bure nao pia anao??... Aisee!, hapa sheria ni lazima. Chamuhimu ni kuwaelimisha watoto wetu na kuwaasa Mara kwa Mara...hii ya kupinga na kukosoa haitasaidia sana!!!!....
 
Drop

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
570
500
Yeye kashindwa kuwa na maono na chama chake kinazidi kudolola zaidi ya asilimia hamsini anataka wengine wawe na maono huyu jamaa vipi
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,308
2,000
Dundo_Boy: CCM kweli inapendwa na watu wenye elimu duni. Sasa wewe unasema eti waende private. Huko vijijini kuna shule za binafsi ngapi za Msingi kwa mfano. halafu ujue shule binafsi gharama ni kubwa wakati serikalini ni bure. Nyie miccm mkoje? yaani wewe ukiwa hapo Ilala, Dar es Salaam unaona kama vile maeneo yote yako kama ya hapo Ilala. Ndio tatizo la kuzaliwa mhimbili na kukulia na kuzeekea Upanga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom