Mchana
Senior Member
- Sep 27, 2007
- 183
- 16
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametengua nafasi ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo, Henry Lihaya na sasa nafasi hiyo itashikiliwa na Mohamed Kiganja.
Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za BMT katika kikao kilichohudhuriwa pia na Lihaya pamoja na mwenyekiti wa baraza hilo, Dioniz Malinzi, alisema kuwa katibu huyo alishindwa kuvisaidia vyama vya michezo.
Alisema kuwa vyama vya michezo vina matatizo mengi lakini mtendaji mkuu huyo alishindwa kabisa kuvisaidia, hivyo alisema anaondoka naye ili akampangie kazi nyingine wizarani.
Mbali na wafanya kazi wa BMT, Kaimu mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Makoye Mkeyenge naye alikuwepo katika mkutano huo.
Wakati huo huo, Malinzi jana alimtangaza Mohamed Kiganja kuwa kaimu katibu wa BMT kuchukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Henry Lihaya kutenguliwa.
Chanzo: HabariLeo