Katiba: Wabunge wa CCM mbona hamna dhamira! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba: Wabunge wa CCM mbona hamna dhamira!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by USTAADHI, Feb 9, 2012.

 1. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kitendo cha wabunge waCCM kuendelea kutengeneza malumbano ya kuwakataa Wakurugenzi wa halmashauri na kulazimisha kuwa wakuu wa wilaya ndiyo wanafaa kuongoza tume ya kuratibu maoni na kuendeleza vijembe tena katika michango yao kinaashiria jinsi wasivyokuwa na dhamira ya kuleta katiba nzuri na yenye maslahi na taifa jamani wabunge wa Ccm mbona mnajichafua kila kukicha,wengine wanadiriki kusema eti wakurugenzi hawako kwenye katiba ya ccm hivyo mkuu wa wilaya basi pia na vyama vingine vipendekeze wenyeviti wa wilaya kuwa wajumbe km ccm wanavyopendekeza wakuu wa wilaya
   
 2. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Yaani ccm wabunge wake ni vilaza na wanamaudhi sana hata kuwasikiliza. Kama alivyohoji Mdee kuwa kuna siri gani mpaka wabunge wa ccm kung'ang'ania wakuu wa wilaya. Yaani wabunge wa ccm ni kama kundi la nyati yaani wote huenda kundi moja hata kama wanaona mbele kuna mamba bila kutumia akili.
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wapigieni magoto wao ndio wengi na mlambe miguu yao ndio watawasikiliza, CDM kwa hili lazima mlifanye.

   
 4. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  kwani mengine waliyokubali walipigiwa magoti?
   
 5. T

  Tafadhali Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amesema hayo wakati anachangia hoja ya mswada Wa marekebisho ya katiba leo jioni!
   
 6. T

  Tafadhali Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau ni mkuu Wa wilaya sio Mkurugenzi
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndio, ww huoni kauli za wabunge wa CDM za kuwaomba waweke mbali itikadi za vyama, huko sio kuwapigia magoti na kuwaomba wawaonee huruma ?
   
 8. d

  dada jane JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ila wewe lazima utakuwa unaumwa ugonnjwa.
   
 9. sterling

  sterling Senior Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nasukumwa kusema kuna hoja ya mlango wa nyuma,,, ila tatizo ni kuwa wabunge wa ccm wana tabasamu la nyoka
   
 10. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  They are suffering from misconception!
   
 11. Mwamikili

  Mwamikili JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 416
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  wapuuzi sana hawa mijitu mizima na watoto nyumbani haina hata akili inakuwa kama nyati kufuata upepo, nimeshangazwa sana na wabunge wengi wa ccm kuona kana kwamba wenzao ni vinganganizi wao mbona ni vinganganizi kwa nini wao wasikubali yaishe kama vile wao wanavyotaka wenzao wakubali yaishe

  nimependa sana kauli ya mbowe akiwaambia wao wanajivunia wingi wao ila chadema wanajivunia wananchi

  hivi akiwa hata mwenyekiti wa serikali za mitaa tatizo nini hapo wacha mkurugenzi afanye hiyo kazi why mkuu wa wilaya? nimewahi kucoment hapo nyuma katiba mpya ifute wakuu wa wilaya wabaki wakurugenzi ambao watawajibika kwa mkuu wa mkoa na wabunge viti maalumu wafutwe maana wanajaza mashuzi yao tu kushindana kuvaa na mamikufu ya dhahabu wakati vichwani mwao empty kabisa

  ebu angalia vijana kama zitto, mnyika, mbowe, lissu, wanavyoweza kujenga hoja mpaka unavutiwa kuangalia
   
 12. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ccm inawabunge kina Mwanaasha wengi sana, kazi yao ni kupigapiga meza bila hata kujua ni nini kinachangiwa, huzuni sana kwa hii nchi. Huyu mama huwa ni Mwanaasha wala hata huwa sitamani kumsikia.
   
 13. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Si ndiyo huyu anayedai amehitimu kidato cha sita pale Mwenge sekondari Singida wakati kaishia std VII. Kanjanja wa elimu ya sekondari
   
 14. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Akafie mbali huko na chama chao cha kishetani!Magamba ni zaid ya shetan ktk dunia hii,MANYAUUUUUU.............!
   
 15. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Umemsahau Halima Mdee mkuu.
   
 16. m

  mtamba Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Kwanza kiswahili hajui,anaongea anachanganya na kinyiramba.
   
 17. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nani atasimamia zanzibar?
   
 18. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 890
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  Marekebisho ya Sheria ya Mchakato wa Katiba mpya yamependekeza kuwaondoa maDc kuwa wenyeji wa Tume ya kuratibu maoni itakapofika katika wilaya zao na kuiandalia mikutano ya kupata maoni ya wananchi kama ilivyoainishwa katika muswada uliopitishwa awali na kuwaweka Wakurugenzi wa Halmashauri badala yake. Wabunge wa CCM wamechachamaa na kuTeamUp kudai lazima maDc hao warejeshwe kuwemo kama mwanzo kwa
  sababu ndie mwakilishi wa Rais wilayani, wabunge wa upinzani ukiongozwa na Mh Mbowe umekataa katakata ma Dc kupewa majukumu hayo kwa sababu ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya za CCM, kwa hiyo ni dhahiri watatetea maslahi ya chama chao. Wakiongozwa na Mh Anna Kilango, wabunge wa CCM walitaka kutumia nguvu ya wingi wao bungeni kupitisha hoja yao kwa kupiga kura, lakini Mh Mbowe alishatoa tahadhari kuwa wanaweza kuipitisha hoja hiyo kwa kutumia wingi wao ndani ya bunge, lakini nje ya bunge kwa wananchi hakutakuwa na muafaka na mchakato mzima utaathirika, kwani wananchi wanashuhudia kinachoendelea bungeni. Mwanasheria Werema alijaribu kutumia busara kutaka iainishwe kisheria kuwa Tume ipewe hiari ya kuamua kama imtumie Dc au DED au wote lakini kambi ya CCM ilitaka lazima kura ipigwe ili kuamua kama maDc wawemo au la, lakini Mh Spika alitumia busara za hali ya juu kukataa kura zisipigwe, alijua kuwa hoja hiyo itapita kwa ushabiki wa kichama lakini madhara yake kwa mchakato mzima yatakuwa makubwa kama alivyoonya Mh Mbowe.
  Kwanini wabunge wanang'ng'ania maDc wawemo? Ingawa Mh Lukuvi alisema kuwa kuwemo au kutokuwemo maDc hakuna uzito wowote, kwani kazi yao ni kuandaa tu mikutano na sio kutoa maoni, sasa kama hivyo ndivyo, kwanini basi wabunge wa CCM walazimishe kwa nguvu zote maDc hao wawemo? Pamoja na msimamo huo kuhatarisha kuvurugika kwa mchakato mzima?
  Ukweli ni huu;
  Licha ya kuwa maDc ni wajumbe wa Kamati za siasa za CCM wilayani, lakini pia ndio makamisaa wa chama hicho serikalini, jambo lolote ambalo CCM inataka litekelezwe na Serikali wilayani hulifanya kupitia kwa Dc, huitwa kwenye kikao cha Kamati ya siasa na hupewa maagizo atekeleze na kikao kinachofuata hutakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji, asipowajibika basi hutochomewa utambi ngazi za juu za Chama na anaweza kuwajibishwa au hata kuondolewa katika nafasi yake.
  Katika mchakato huu wa katiba mpya, endapo itapitishwa kuwa maDc ndio waandae mikutano ya kuwasilisha maoni kwa tume ya uratibu maoni, basi kitakachotokea ni kuwa maDc hao wataandaa mikutano hiyo kwa maelekezo na kushirikiana na uongozi wa CCM wilaya, na kwa kutumia mtandao wake uliotanda mpaka kwenye vitongoji, basi mikutano hiyo, kwa makusudi kabisa, itahusisha wanaCCM walioandaliwa kutoa maoni yatakayoendana na maslahi ya chama hicho, lakini yatafanywa yaonekane ni maoni ya wananchi wengi, hii inaitwa "Political Juggling" au "Manipulation of Public Opinion" hivyo basi, juggling hii kwa kawaida Wakurugenzi, DED's, huwa hawaiwezi kwani wao ni Technocrats zaidi, wanaweza kuchakachua upigaji kura kitaalam lakini kumanipulate utoaji maoni hawawezi kwani ni suala la kisiasa zaidi, kwa vile maDc ni wanasiasa zaidi na kwa kushirikiana na viongozi wa chama chao, kazi hii wataiweza vizuri zaidi, ndio maana, baada ya vipengele vingine vya kuhodhi mchakato huu kupanguliwa, inabidi kupambana kufa kupona maDc wabakishwe ili angalau kuwa na starting point ya kutekeleza dhamira ya kuinfluence mchakato huo ili kulinda maslahi ya CCM katika chaguzi zijazo na utawala wake.
  Habari Ndiyo Hiyo.
   
 19. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana dhihirisha kwamba hawapo kutetea maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla bali matumbo yao na vibaraka wao.
   
 20. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi kilichonisikitisha ni kauli ya Anne Kilango eti kwa kuwa rais ndiye kiongozi wa nchi basi mkuu wa wilaya ndiye rais wa wilaya.Sasa hii katiba ni ya wananchi au rais na wakuu wake wa wilaya?
   
Loading...