Katiba: Wabunge wa CCM mbona hamna dhamira!

Katiba: Wabunge wa CCM mbona hamna dhamira!

Hebu tuchukue mfano hai, kwa mfano yule mama Fatuma Kimaro aliyekuwa Dc wa Igunga, awe ndio anaandaa mikutano ya maoni ya katiba, unatarajia ataandaa mikutano ya aina gani?
 
Wakuu wa wilaya ni wana CCM na wanaingia kwenye kamati za siasa za wilaya wakati Wakurugenzi ni wataalamu na si wanasiasa. Wabunge wa CCM wanajali maslahi ya chama chao hawako kwaajili ya maslahi ya nchi. Wakurugenzi ndio wanatakiwa wawe waratibu wa maoni ya katiba mpya sio MA-DC (WanaCCM).
 
Kwani huyu mama nini cha maana alichowahi kuongea bungeni?
 
Kwa kweli, uwepo wa MaDC ni kwa maslahi ya CCM tu. Hakuna atakayebisha ktk hili na hata wao (CCM) wanajua lengo la kuhitaji MaDC wapewe consultation power ya kuitisha mikutano linamaanisha nini!! Kupitia MaDC wataweza kuandaa mikutano yenye sura ya "public centred meeting" lakini watakuwa party influenced na composition ya washiriki wanaweza kuwamanipulated ili waeleze masuala yatakayolinda maslahi ya CCM.
 
Mnatupotezea muda kwa maswala yasiyo na maana.
Hata kilaza yeyote anaweza kuandika tangazo kuwaambia watu kuwa leo kutakuwa na mkutano kati ya wananchi na tume ya katiba.
Sasa DED hapa anaingiaje?..... yaani kazi yake haihusiani kabisa na siasa. Anne kilango yuko right.
Nyie wote ushabiki ndiyo unawazingua, hamna pointi.
 
Kwanini mnangang`ania wakuu wa wilaya watumike kwenye mchakato wa kuandaa mikutano ya utoaji wa elimu na Siyo wakurugenzi? au mmegundua kuwa huo ndo mwarubaini?.
 
Tuache kulaumu tu, hebu tujadili Kwanini Mkuu wa wilaya na sio Mkurugenzi, au kwanini Mkurugenzi na sio mkuu wa wilaya?
 
Tuache kulaumu tu, hebu tujadili Kwanini Mkuu wa wilaya na sio Mkurugenzi, au kwanini Mkurugenzi na sio mkuu wa wilaya?
Mkuu popiexo hilo mbona MgungaMiba ameshalieleza kwa kirefu, au unataka mjadala wa aina gani?
 
Kwanini mnangang`ania wakuu wa wilaya watumike kwenye mchakato wa kuandaa mikutano ya utoaji wa elimu na Siyo wakurugenzi? au mmegundua kuwa huo ndo mwarubaini?.


Huwa inasemekana wakuu wa wilaya wengi ni mapandikizi ya EL nadhani jamaa anafanya kazi yake
 
Si ndiyo huyu anayedai amehitimu kidato cha sita pale Mwenge sekondari Singida wakati kaishia std VII. Kanjanja wa elimu ya sekondari

yule ni mfano wa viongozi ambao wananchi waliwapigia kura kuliongoza taifa hili hivi kweli yule ana mawazo zaidi ya kutafuta fedha yule na kwa ni i hivi viti maalum viwepo mi sioni kazi yake
 
nilichooona pale ni kwamba ccm wanajitahidi sana kuuwa ile nguvu ya vile vipengele vilivyopelekwa mle ndani ili hoja ile ibaki kasha tu sasa mkuu wa wilaya si nyampara wa CCM hana wataalam chini yake anawezaje kuiongoza tume ilhali kuna wataalam wilayani isitoshe wakuu wa wilaya tunaowajua wengi ni akina yakhe anapata kulingana na uwezo wa majungu vipi kuhusu uwezo wao wa uchambuzi wa mambo?
 
Marekebisho ya Sheria ya Mchakato wa Katiba mpya yamependekeza kuwaondoa maDc kuwa wenyeji wa Tume ya kuratibu maoni itakapofika katika wilaya zao na kuiandalia mikutano ya kupata maoni ya wananchi kama ilivyoainishwa katika muswada uliopitishwa awali na kuwaweka Wakurugenzi wa Halmashauri badala yake. Wabunge wa CCM wamechachamaa na kuTeamUp kudai lazima maDc hao warejeshwe kuwemo kama mwanzo kwa
sababu ndie mwakilishi wa Rais wilayani, wabunge wa upinzani ukiongozwa na Mh Mbowe umekataa katakata ma Dc kupewa majukumu hayo kwa sababu ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya za CCM, kwa hiyo ni dhahiri watatetea maslahi ya chama chao. Wakiongozwa na Mh Anna Kilango, wabunge wa CCM walitaka kutumia nguvu ya wingi wao bungeni kupitisha hoja yao kwa kupiga kura, lakini Mh Mbowe alishatoa tahadhari kuwa wanaweza kuipitisha hoja hiyo kwa kutumia wingi wao ndani ya bunge, lakini nje ya bunge kwa wananchi hakutakuwa na muafaka na mchakato mzima utaathirika, kwani wananchi wanashuhudia kinachoendelea bungeni. Mwanasheria Werema alijaribu kutumia busara kutaka iainishwe kisheria kuwa Tume ipewe hiari ya kuamua kama imtumie Dc au DED au wote lakini kambi ya CCM ilitaka lazima kura ipigwe ili kuamua kama maDc wawemo au la, lakini Mh Spika alitumia busara za hali ya juu kukataa kura zisipigwe, alijua kuwa hoja hiyo itapita kwa ushabiki wa kichama lakini madhara yake kwa mchakato mzima yatakuwa makubwa kama alivyoonya Mh Mbowe.
Kwanini wabunge wanang'ng'ania maDc wawemo? Ingawa Mh Lukuvi alisema kuwa kuwemo au kutokuwemo maDc hakuna uzito wowote, kwani kazi yao ni kuandaa tu mikutano na sio kutoa maoni, sasa kama hivyo ndivyo, kwanini basi wabunge wa CCM walazimishe kwa nguvu zote maDc hao wawemo? Pamoja na msimamo huo kuhatarisha kuvurugika kwa mchakato mzima?
Ukweli ni huu;
Licha ya kuwa maDc ni wajumbe wa Kamati za siasa za CCM wilayani, lakini pia ndio makamisaa wa chama hicho serikalini, jambo lolote ambalo CCM inataka litekelezwe na Serikali wilayani hulifanya kupitia kwa Dc, huitwa kwenye kikao cha Kamati ya siasa na hupewa maagizo atekeleze na kikao kinachofuata hutakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji, asipowajibika basi hutochomewa utambi ngazi za juu za Chama na anaweza kuwajibishwa au hata kuondolewa katika nafasi yake.
Katika mchakato huu wa katiba mpya, endapo itapitishwa kuwa maDc ndio waandae mikutano ya kuwasilisha maoni kwa tume ya uratibu maoni, basi kitakachotokea ni kuwa maDc hao wataandaa mikutano hiyo kwa maelekezo na kushirikiana na uongozi wa CCM wilaya, na kwa kutumia mtandao wake uliotanda mpaka kwenye vitongoji, basi mikutano hiyo, kwa makusudi kabisa, itahusisha wanaCCM walioandaliwa kutoa maoni yatakayoendana na maslahi ya chama hicho, lakini yatafanywa yaonekane ni maoni ya wananchi wengi, hii inaitwa "Political Juggling" au "Manipulation of Public Opinion" hivyo basi, juggling hii kwa kawaida Wakurugenzi, DED's, huwa hawaiwezi kwani wao ni Technocrats zaidi, wanaweza kuchakachua upigaji kura kitaalam lakini kumanipulate utoaji maoni hawawezi kwani ni suala la kisiasa zaidi, kwa vile maDc ni wanasiasa zaidi na kwa kushirikiana na viongozi wa chama chao, kazi hii wataiweza vizuri zaidi, ndio maana, baada ya vipengele vingine vya kuhodhi mchakato huu kupanguliwa, inabidi kupambana kufa kupona maDc wabakishwe ili angalau kuwa na starting point ya kutekeleza dhamira ya kuinfluence mchakato huo ili kulinda maslahi ya CCM katika chaguzi zijazo na utawala wake.
Habari Ndiyo Hiyo.
hivi CCM hawajui life span ya katiba au wanafikiria ni ni kutaka mchakato uwe mbovu maana wanaweza kuja kuathirika wao na vitu vibovu wanavyotaka kuvipitisha leo
 
Mnatupotezea muda kwa maswala yasiyo na maana.
Hata kilaza yeyote anaweza kuandika tangazo kuwaambia watu kuwa leo kutakuwa na mkutano kati ya wananchi na tume ya katiba.
Sasa DED hapa anaingiaje?..... yaani kazi yake haihusiani kabisa na siasa. Anne kilango yuko right.
Nyie wote ushabiki ndiyo unawazingua, hamna pointi.
wewe ni mkimbizi nadhani unaishi kwa ajili ya katiba mbovu huoni haja ya marekebisho
 
wewe ni mkimbizi nadhani unaishi kwa ajili ya katiba mbovu huoni haja ya marekebisho
Badala ya kujiuliza kama una haki ya kuongelea muungano unaleta kejeli kwenye jambo ambalo halina umuhimu. Kuitisha mkutano hata wakiwapa hayo mamlaka bakwata hakuna tofauti il mradi uwe wa hadhara.
 
Nani atasimamia zanzibar?
Sheria hakatazi kuweka DED au equivalent Znz, na kuwaweka ma-DED tanganyika.

After all, hawa wazenji hawa na mbinu za kijinga za CCM, itakuja kuwatokea puani one time.
Wanatakiwa waingie kwenye mchakato wa Katiba mpya kwenye mambo yanayowahusu - mambo ya muungano tu!!

Lakini kwa sababu CCM wanapenda ujanja ujanja, its Ok, huko mbele tutaonana tu!!!
 
Back
Top Bottom