Katiba mpya yaipasua CCM


Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,780
Likes
2,030
Points
280
Age
36
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,780 2,030 280
• Makundi ya urais yachochea maandamano kupinga serikali tatu

na Mwandishi wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeweka mkakati wa kuipinga rasimu ya Katiba mpya, hususan pendekezo la muundo wa serikali tatu, Tanzania Daima Jumapili limebaini. Mkakati huo umekuja baada ya kubaini kuwa rasimu ya Katiba mpya iliyopendekeza muundo huo imekipasua chama hicho katika makundi yanayohatarisha uhai wa chama.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa kuzungumza na mawaziri, wabunge, viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho tawala, umebaini kuwa makada wengi wameshangazwa na hatua ya Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Warioba kuruhusu pendekezo la kutaka muundo wa serikali tatu liingizwe kwenye rasimu.

Tayari Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anatajwa kutaka kuwania urais amepinga pendekezo hilo, kwa madai kwamba hakuna nchi inayoongozwa na marais watatu duniani. Makundi mengine ya urais yanadai kuwa rasimu hiyo ikipita itawaweka njia panda wasijue wagombee nafasi gani ifikapo mwaka 2015.

Baadhi ya vigogo wa chama hicho waliliambia gazeti hili kuwa lawama za kwanza wanazielekeza kwa Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, kwa madai kuwa aliiona rasimu hiyo kabla ya mtu mwingine yeyote na kuiacha kamati ya Jaji Warioba ikija na pendekezo la kutaka serikali tatu.

"Kwanza Ilani yetu inazungumzia serikali mbili, kule Zanzibar Rais Ali Mohamed Shein na Naibu Katibu Mkuu Visiwani wanagombana na Wazanzibari wa CUF kila siku kuhubiri serikali mbili, leo rasimu inakuja na serikali tatu na rais anaiona na anaipitisha ije kwa wananchi. Hatumuelewi," alisema mmoja wa viongozi wa chama hicho, mjumbe wa NEC kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kigogo huyo alisema chama kinasubiri kwa hamu kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC), inayotarajiwa kukutana Jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam, maalumu kwa ajili ya kujadili rasimu hiyo ya Katiba na kutoka na msimamo wa chama. Kada mwingine ambaye ni mwenyekiti wa CCM kwenye moja ya mikoa ya Kanda ya Kati, alilieleza gazeti hili kuwa kilichotokea ndani ya chama hicho kuhusu pendekezo la serikali tatu ni kama bomu lililolipuka ghafla.

"Mimi nakuambia kilichotokea ni kama bomu vile, sasa kila mtu amenyanyuka, anakung'uta vumbi na kuanza kuvuta fikra nini kimetokea. Nadhani kikao cha CC kesho kutwa ni muhimu sana na lazima tuwe na NEC kabla ya Bunge kumalizika tukawekane sawa," alisema mwenyekiti huyo wa CCM mkoa. Kabla ya chama hicho kuitisha kikao cha CC ya dharura, baadhi ya makundi ya urais yalielezwa kuanza kupanga njama na mikakati ya kuwachonganisha baadhi ya wafuasi wao kuitisha maandamano kupinga pendekezo la serikali tatu.

Mikakati ya kuzima serikali tatu

Wakati Wana CCM wengi wamegawanyika kutokana na rasimu ya pendekezo hilo, upande wa pili wanajipa moyo kwamba hoja hiyo haitapita kuwa sheria ndani ya Katiba mpya. Moja ya mikakati inayofanywa na chama hicho kwa sasa ni kuhakikisha nakala ya rasimu hiyo inawafikia wanachama ngazi ya tawi ili wailewe na kuwataka wawe makini wakati wa upigaji kura kupinga baadhi ya mambo wasiyoyataka, ikiwamo hoja ya kutaka kuwa na serikali tatu.

Pia chama hicho kimeanzisha mabaraza ya Katiba ya chama ili kuwapa fursa zaidi wanachama wao kuijua rasimu hiyo na kushiriki kikamilifu kuipitisha.

Wabunge Viti Maalumu wacharuka

Baadhi ya wabunge wa Viti Maalumu waliliambia gazeti hili kuwa pendekezo hilo linaonesha wivu wa wajumbe wa tume hiyo kwa wabunge hao. "Umoja wa wanawake (UWT) ulishapitisha azimio kwamba ukomo wa Viti Maalumu ni awamu mbili. Lakini kusema viti hivyo viondoke, havina maana, ni uamuzi uliotokana na wivu," alisema mbunge mmoja wa Viti Maalumu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Mbunge huyo ambaye aliungwa mkono na wenzake, alisema watahakikisha hoja hiyo haipiti na kuingizwa kwenye Katiba mpya.
Wiki iliyopita, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa rasimu ya mapendekezo ya katiba mpya ambayo imesheheni masuala mazito ambayo kama yatapitishwa yataleta mabadiliko makubwa ambayo yamekuwa yakipiganiwa kwa zaidi ya miaka 20.

Miongoni mwa mambo makuu yaliyoingizwa katika rasimu hiyo ni mfumo mpya wa Muungano wa serikali tatu; serikali ndogo ya mawaziri 15; Tume Huru ya Uchaguzi; spika na naibu wake wasio wabunge wala viongozi wa vyama vya siasa. Mengine yaliyoingizwa ni kumnyang'anya rais madaraka ya kuteua peke yake viongozi wa ngazi za juu. Tume inapendekeza kwamba rais adhibitiwe katika kuteua mawaziri na manaibu wao, majaji na manaibu wao, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na makatibu wakuu na manaibu wao.

Imependekeza rais asaidiwe na vyombo kadhaa katika uteuzi huo. Mawaziri watakaoteuliwa na rais hawatashika nyadhifa zao hadi waidhinishwe na Bunge. Vile vile, rais atateua majaji kutoka miongoni mwa majina yatakayopendekezwa kwake na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Tume imependekeza liundwe Baraza la Ulinzi na Usalama litakalomshauri rais kuhusu uteuzi wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Zaidi ya hayo, kinga ya rais kutoshitakiwa imependekezwa ibaki pale pale, ingawa Bunge lina mamlaka ya kumshitaki kama ilivyo sasa. Rasimu pia imependekeza umri wa mgombea urais ubaki miaka 40 ya sasa. Katika uchaguzi, rais atatangazwa mshindi iwapo atakuwa amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote; na matokeo yake yatahojiwa mahakamani ndani ya mwezi mmoja tangu yalipotangazwa.

Mbali na kurejeshwa kwa taifa la Tanganyika, tume imependekeza pia mgombea binafsi aruhusiwe katika ngazi zote, kuanzia kitongoji hadi Ikulu. Akisisitiza umakini uliotumika kuchakata mapendekezo yaliyokusanywa kwa wananchi tangu Aprili mwaka jana, Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Warioba alisema wamezingatia masilahi ya taifa na mahitaji ya wakati katika kila eneo.

Chanzo: Mwananchi
 
N

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Messages
7,725
Likes
28
Points
145
N

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2008
7,725 28 145
Tunajuwa msimamo wa CCM wa serikali 2. Wadau wengine katika tasnia ya usihasa kama CDM hebu tujuvyeni msimamo wenu. Naona baada ya rasimu muweweseko umewakumba Watanzania wa upande mmoja.
 
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined
Jul 29, 2010
Messages
11,192
Likes
435
Points
180
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined Jul 29, 2010
11,192 435 180
Nawapongeza CDM kwa ukimya wao. Bila shaka wanajipa mda kuisoma na kuichambua rasimu vyema. Tuwaache CCM warukeruke, lakini kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake...
 
Mtumbatu

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Messages
327
Likes
81
Points
45
Mtumbatu

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2012
327 81 45
Niliwaambia kuwa Tanganyika imefuka, na mfu alioza si "The Mumy", hivyo hakuna atakayeifufua. Mlikosea kuifuta asili yenu katika vitabu vya historia sasa mnaweweseka na Zanzibar. Zanzibar ipo na intaendelea kuwepo kwa sababu ina asili, na anayekataa asili ni mtumwa, msipoipata Tanganyika yenu sasa, mjue hilli ni basi la mwisho kuelekea Tangayika, msipokuwemo, hamtaifikia Tanganyika tena mpaka kiyama, na mtabaki kuwa watumwa watu msio na asili. Aibu kubwa mmepoteza mamilioni ya shillingi kuendesha Tume ya Katiba na hamtaipata Tanganyika. looooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooser.
 
Mtumbatu

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Messages
327
Likes
81
Points
45
Mtumbatu

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2012
327 81 45
Nawapongeza CDM kwa ukimya wao. Bila shaka wanajipa mda kuisoma na kuichambua rasimu vyema. Tuwaache CCM warukeruke, lakini kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake...
Chadema haina jipya katika hili maana Kanisa Katoliki (msome Askofu Kilaini alivyosema leo) nalo pia halitaki serikali tatu, na Chadema haiwezi kwenda kinyume na kanisa, so forget it.
 
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Messages
716
Likes
66
Points
45
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2012
716 66 45
1+1=3

Hesabu hii kwa wana CCM wa makundi inaleta hasira na haipandi.

Imekula kwao safari hii, wamepigwa mbigili tatu matakoni.
 
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Messages
716
Likes
66
Points
45
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2012
716 66 45
Tanganyika daima.
Ile sala ya Mtikila imekuwa kitendo halisi.
Tunataka Tanganyika yetu kwa gharama yeyote.


Niliwaambia kuwa Tanganyika imefuka, na mfu alioza si "The Mumy", hivyo hakuna atakayeifufua. Mlikosea kuifuta asili yenu katika vitabu vya historia sasa mnaweweseka na Zanzibar. Zanzibar ipo na intaendelea kuwepo kwa sababu ina asili, na anayekataa asili ni mtumwa, msipoipata Tanganyika yenu sasa, mjue hilli ni basi la mwisho kuelekea Tangayika, msipokuwemo, hamtaifikia Tanganyika tena mpaka kiyama, na mtabaki kuwa watumwa watu msio na asili. Aibu kubwa mmepoteza mamilioni ya shillingi kuendesha Tume ya Katiba na hamtaipata Tanganyika. looooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooser.
 
rayun

rayun

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2013
Messages
240
Likes
3
Points
35
rayun

rayun

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2013
240 3 35
hiiish! ccm ina wenyewe. i like it. sasa mkajipange upya. si mlishachakachua mabaraza ya katiba.sasa bado hamjiamini
 
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Messages
716
Likes
66
Points
45
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2012
716 66 45
Yarabi Toba.

Kwani aliye nyuma ya kudai ZaNZIBAR YENU ni nani??
Watu hawaruhusiwi kuwa na mawazo yao sharti kundi fulani liwaongoze??
Kama nyie mmetumwa kudai Zanzibar , sisi huku Tanganyika tunadai serikalio 3 kwa akili zetu wenyewe.

Chadema haina jipya katika hili maana Kanisa Katoliki (msome Askofu Kilaini alivyosema leo) nalo pia halitaki serikali tatu, na Chadema haiwezi kwenda kinyume na kanisa, so forget it.
 
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Messages
716
Likes
66
Points
45
Msalagambwe

Msalagambwe

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2012
716 66 45
Gharama ya baraza la mawaziri 45 ni Tshs ngapi kwa mwaka????

kWA NINI WANAKIMBILIA GHARTAMA YA KUENDESHA NCHI KATIKA URAIS TU.

GHARAMA YA KURUHUSU wAZUNGU WATUIBIE DHAHABU YETU NI TSHS NGAPI

TANZANIA HATUNA TATIZO LA FEDHA TUNA TATIZO LA VIWAVI JESHI WENYE MAGAMBA YA KIJANI.
 
Bobwe

Bobwe

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2013
Messages
1,241
Likes
10
Points
0
Age
39
Bobwe

Bobwe

JF-Expert Member
Joined May 21, 2013
1,241 10 0
Naiona tanganyika ileeee...
 
K

Kateka Sanza

Member
Joined
Jun 8, 2013
Messages
44
Likes
6
Points
15
K

Kateka Sanza

Member
Joined Jun 8, 2013
44 6 15
Du taratibu yote hayo ni mapendekezo kura yako ndo itaamua aina ya katiba
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Likes
1,151
Points
280
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 1,151 280
Bila Tanganyika, Tanzania haiwezekani, bila Tanzania, CCM haiwezekani; Huo ndio mtihani uliopo; Mungu ibariki na ilinde Tanganyika na watanzania wake;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Domy

Domy

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
4,701
Likes
20
Points
135
Domy

Domy

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
4,701 20 135
Serikali tatu ndio mpango mzima! Hongera sana Warioba kwa kukataa kutumiwa na mafisadi!
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,347
Likes
145
Points
160
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,347 145 160
Niliwaambia kuwa Tanganyika imefuka, na mfu alioza si "The Mumy", hivyo hakuna atakayeifufua. Mlikosea kuifuta asili yenu katika vitabu vya historia sasa mnaweweseka na Zanzibar. Zanzibar ipo na intaendelea kuwepo kwa sababu ina asili, na anayekataa asili ni mtumwa, msipoipata Tanganyika yenu sasa, mjue hilli ni basi la mwisho kuelekea Tangayika, msipokuwemo, hamtaifikia Tanganyika tena mpaka kiyama, na mtabaki kuwa watumwa watu msio na asili. Aibu kubwa mmepoteza mamilioni ya shillingi kuendesha Tume ya Katiba na hamtaipata Tanganyika. looooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooser.
Hapo penye bold nimepapenda. Kwa kuwa Watanganyika watakuwa watumwa, wakoloni ni kinanani? Nadhani hawatakuwa Wazanibzar
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,347
Likes
145
Points
160
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,347 145 160
Bila Tanganyika, Tanzania haiwezekani, bila Tanzania, CCM haiwezekani; Huo ndio mtihani uliopo; Mungu ibariki na ilinde Tanganyika na watanzania wake;
Mchambuzi,
Nimesoma ulichoandika na saini yako kama nilvyoikoleza hapa chini. Je, vinaendana, au tuendelee kusubirii?
"In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."
 
Mgosi Mokiwa

Mgosi Mokiwa

Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
34
Likes
0
Points
13
Mgosi Mokiwa

Mgosi Mokiwa

Member
Joined Dec 21, 2012
34 0 13
Issue kubwa hapa ni ubinafsi wa CCM ambao walifanya siasa ni yao.Hao wanawake si wamewekewa nafasi zao kuna tatizo gani?Tatizo walizoea dezo na kupata ubunge kwa njia ya mgongo ushindani hata na wanawake wengine hawauwezi!! Watanzania wameongea na watahakikisha matakwa yao yanasimama.
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Likes
1,151
Points
280
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 1,151 280
Mchambuzi,
Nimesoma ulichoandika na saini yako kama nilvyoikoleza hapa chini. Je, vinaendana, au tuendelee kusubirii?
"In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."
Unaweza fafanua una maana gani unapouliza je vinaendana au tuendelee kusubiri mkuu?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
S

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,835
Likes
3
Points
0
S

sokoinei

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,835 3 0
Mkutano wa halmashauri kuu ya Ccm umemalizika usiku wa manane leo hii. Mkutano huo ulikua ukijadili pamoja Rasimu mpya ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba!
Msemaji mkuu wa Ccm Nape Nauye akihojiwa na Mtangazaji wa BBC Daved Nampesia,alisema kua Ccm watatoa tamko la Chama leo mchana juu ya nini msimamo wao kwa Rasimu hiyo ya Katiba Mpya.

Hii ni wazi kuwa Ccm hawakufurahishwa na Rasimu hii ya Katiba mpya chini ya Jaji Warioba haswa ktk vipengele viwili. Kipengele cha Mgombea binafsi na kile cha Muundo wa serikali tatu. Ndio maana ccm wameweweseka na kuamua kujadili swala hili ktk mkutano wao mkuu.

Imekua ni kawaida kwa ccm kupinga kile kinacho kubalika na vyama vya upinzani huku ikikubali kile kinachopingwa na Vyama vya upinzani. Rasimu ya Katiba mpya ni MAONI ya Watanzania na sio maoni ya Tume wala Vyama! Inashangaza Ccm kupinga MAONI ya Wananchi huku wakijisahau kuwa hata wao wamepewa uongozi na hao hao Wananchi.

CCM imejikuta ktk wakati mgumu kwa kuwa tangia mwanzo wa kuunda Tume wamekua wakijitahidi kuhakikisha kwamba tume hiyo inakua chini yao na kuwa maoni ambayo yangewasilishwa yangekua ya wana ccm na sio Wananchi.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania akizungumza jana alisema kuwa vyama na wanaharakati lazima waheshimu matakwa ya Wananchi kwa kuwa ndio Demokrasia.
Je Ccm kutaka kupinga Maoni ya Watanzania kwa vile tu inaingilia Masilahi yao Kisiasa haswa kwa kipengele cha Mgombea Binafsi ni DEMOKRASIA?
 

Forum statistics

Threads 1,274,855
Members 490,833
Posts 30,526,037