Katiba Mpya ya Chit Chat: Maoni

TANMO

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
12,211
Reaction score
13,051
...Katiba mpya iruhusu Mods nao wapigwe Ban na hata life Ban pale inapobidi.

...Katiba mpya ikataze Ku-bip na iweke wazi adhabu zitakazomkabili Mbipuji yeyote Yule.

...Katiba mpya ipige marufuku kuchangia harusi (manake inaelekea kusababisha Hati Konkesheni)

...Katiba Mpya ilitambue JF Udaku liwe Gazeti la Sirikali na litengewe fungu kutoka mfuko wa Sirikali Kuu.

...Katiba mpya iweke wazi ukomo wa watu kufanya ukaguzi (Kiasprini kina Miaka 102 lakini bado ndiyo kikaguzi kikuu humu)

...Katiba mpya ihalalishe rasmi matumizi Bhange.

...Katiba mpya iruhusu Wanawake kuolewa na wanaume zaidi ya Mmoja alimradi ataweza kuwatimizia mahitaji yao wame wote watakaomuoa. (hii itapunguza watu kupigana sababu ya wanawake)

...Katiba mpya ikataze watu kutumia majina ya ajabu ajabu humu na badala yake watu watumie majina yao ya ukweli.

...Katiba mpya ilazimishe membaz wote wa Jeiefu waweke picha zao kwenye avataa na pia umri wao uwe displeidi.

...Katiba mpya ipige marufuku majungu na umbea: copy to Bishanga

...Katiba mpya ipige marufuku kunyemelea wake za watu: Copy to Erickb52

...Katiba mpya ikitambue Kimasai kuwa lugha ya Taifa.


Niandikie Maoni yako nami nitayawasilisha kwenye Tume ya Mabadiliko ya katiba.
Email: Tanmo@jfudaku.net
Simu: Sifuri Saba Nane Saba Arubaini Sifuri Sifuri Sifuri Sifuri..
Faksi: Mzamini kazingua kutununulia Faksi Mashini.
Twita: jfudaku
Fesibuku:facebook.com/jfudaku
Instagramu: ni ki nini hiki?


Mapendo.
TANMO
 
..... Katiba mpya izuie TONGOZO via PM anayemtongoza mwenzie PM zake ziwekwe hadharani

..... Katiba mpya iruhusu matumizi ya dildo kama ilivyo kwenye Condoms, make wanaume wamekuwa pasua kichwa.

..... Katiba mpya iruhusu ndoa za mkataba.. Yaan mkianza kufunga ndoa tu unaspecify muda wa ndoa yako. Hii itapunguza wingi wa talaka humu Chitchat na pia wakataze mkataba mrefu zaidi ya miezi mitatu.. Pia hakuna kurenew na mtalaka wako..Wengine humu wanaturingishia ndoa zao eti zimedumu kha!!!!!

...... Katiba mpya iruhusi open relationship. Ila kwamba iwe halali mimi kuwa na Bishanga, Vin Diesel bila kipingamizi.

....... Katiba mpya iruhusu matumizi ya gongo kama kinywaji halali. Make bia zimepanda bei sana.

Nawasilisha.....
 
Last edited by a moderator:
Endapo katika mpya itaruhusu bangi basi kipengelw cha lawama kiondolewe JF hasa mtu atakapotukana kwa sababu ya bangi alizovuta!

Katiba mpya isiruhusu wanawake kuwa na mabwana wawili, kwa sababu wanawake hawajaisha bado mpaka kufika stage ya kugombea.

MoDs kupigwa ban hapo naona kama unataka kumchezea sharubu Simba ukidhani kalala, shauri yako litakalokukuta!!

Kuhusu ukaguzi, sifa za mkaguzi lazima awe na CPA (J) lakini inaoneka members wengi wanakimbia mahesabu na kupelekwa wakaguzi kuwa wachache! Hapa itabidi kiwango cha ukali wa mitihani kipunguzwe ili babu Asprin msifikiri anatesa bure kumbe ni msuli wake tehe tehe.

Kuhusu majungu kabla ya kuweka kwenye katiba hatuna budi kutoa tafsiri sahihi ya majungu ni nini ili kuepuka mgongano.
 
Last edited by a moderator:

Tafadhali rejea kipengele chako cha ndoa ya mkataba.

Nafanya booking kabisa ya ndoa yako itakapoisha toka kwa Bishanga na Vin Diesel hata kwa siku moja bora ni mkataba tehe tehe.

Kuhusu PM naunga mkono hoja watu wote wanaotaka kutongoza watongoze hapa hapa jukwaani ili tujue kabisa fulani anamtaka nani na kama kawin au katolewa mbavuni lol!!!
 
Last edited by a moderator:
Kwangu mimi naomba nguvu na mamlaka ya mod hasa yapunguzwe, kwa sasa hivi mod ni kila kitu. Anaweza toa ban apendavyo na anaweza kutoa post yeyote atakavyo. kiukweli mamlaka haya yakimkuta mod mwenye akili mbaya anaweza kuabuse atakavyo.
 

Shaka shaka gani Mzee wa Rula wacha tujimwaye mwaye uwanja wetu huu..... Hebu waite marafikizo waunge mkono hoja ili maoni yangu yapitishwe bila pingamizi hatimaye nifunge ndoa na wewe..... Can't wait uhuhuuuuuu!!!!!! :smile: :smile:
 
Last edited by a moderator:
Shaka shaka gani Mzee wa Rula wacha tujimwaye mwaye uwanja wetu huu..... Hebu waite marafikizo waunge mkono hoja ili maoni yangu yapitishwe bila pingamizi hatimaye nifunge ndoa na wewe..... Can't wait uhuhuuuuuu!!!!!! :smile: :smile:

Aiseee yaani nawaita wadau haraka sana hapa waje wachangie hii kitu ili wapate shemeji na wifi yao chappuuuu:

Arushaone Filipo, marejesho, sweetlady, Mungi, Preta, Madame B, PakaJimmy, Asprin kwa ushauri, Bishanga aache wivu,
 
Last edited by a moderator:

Kwenye Blue mi napinga maana hapa watu watakuwa wan copy na kupaste mistari ya wengine, lasivyo iwekwe hati miliki ukitupia mistari maeneo mtu asikopy.

Kwenye Green nasapoti asilimia 100, hiyo iwekwe bila kupingwa

Kwenye red, hapana maana mtatutesa sana Charminglady mkiwa na hivo vijitu mtakua mnavunja haki za binadamu hasa zetu sisi wanaume
 
Sasa mbona hata katiba mpya bado iko rasimuni , ktk kipengele cha kuruhusu Mneli (bhange), hapa viashiria vyote vyaonyesha mtoa hoja keshaanza kuvuta?
Akiwa tayari "anabembea" ndy kaleta muswada!
Btw napendekeza rekebisho hapo ulipomuelezea @Aspirini pasomeke ;
"Libabu kama lia'Aspirini lina mamiaka 120 lakini ndiyo bado likaguzi likuu humu kwenye lijukwaa la lijamvi la lichitchat".
 

Hapan inabidi kipengele hicho kiwepo ila kuwe na adjustmenti, maana kikiondoilewa wanachi wa Chit Chati watafanya makusidi alafu wasingizie jani, hata wale ambao hawalitumii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…