Katiba mpya siyo hisani ya mtu. Tuache kuwaomba wanasiasa watupatie bali tuungane ili ipatikane

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Kwa machozi na damu nchi yetu inahitaji muelekeo mpya. Mwelekeo wa kuwaandaa watu wetu na mabadiriko ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Katika ndiyo mwarobaini.

Katiba itakayomtambua na kumthamini kila raia, itakayotupa haki ya kuwawajibisha viongozi, itakayoheshimu utu wa raia wote.

Wanasiasa hawapaswi kutupangia lini na wapi tunapaswa kupatiwa katiba.
 
Hizi kelele za katiba mpya zinapaswa kupigwa bila kukoma, mpaka walioko madarakani wajione kabisa hawana uhalali wa kuongaza nchi. Kwa asili watanzania sio watu wanaoweza kupigania haki zao kwa maandamano kutokana na athari za ujamaa, na kutawaliwa na chama kimoja kwa muda mrefu, ambapo chama hicho kimekuwa kikwazo cha katiba mpya. Mbinu za kufanya ili kuweza kupata katiba mpya

1. Kufanya makongamano mbalimbali kupandisha public awareness.

2. Kufanya vipindi mbalimbali kwenye. Redio, Tv na media nyingine kuhusiana na umuhimu wa katiba mpya, ikiwemo kuanisha mapungufu ya katiba iliyopo.

3. Kushawishi wananchi wengi kususia kupiga kura kama sehemu ya kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi na katiba iliyopo. Hili naona limeanza kupata uelewa mkubwa.

4. Public disobedience kwa viongozi wanaopatikana kwenye chaguzi hizi.

5.kuanza kuwazomea viongozi wote wasiokubaliana na katiba mpya ikiwemo rais.

6. Kutengeneza tshirt nyingi zenye ujumbe wa kudai katiba mpya, na watu wahamasishwe kuzivaa kwenye maeneo ya mikusanyiko, kama viwanja vya mpira, masokoni, nyumba za ibada, vituo vya mabasi nk.

Tukifanikiwa mbinu wangalau tatu kati ya hizo, watawala watajikuta kwenye wakati mgumu maana hilo ni takwa halali.
 
Kwa machozi na damu nchi yetu inahitaji muelekeo mpya. Mwelekeo wa kuwaandaa watu wetu na mabadiriko ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Katika ndiyo mwarobaini. Katiba itakayomtambua na kumthamini kila raia, itakayotupa haki ya kuwawajibisha viongozi, itakayoheshimu utu wa raia wote. Wanasiasa hawapaswi kutupangia lini na wapi tunapaswa kupatiwa katiba.
Naunga mkono hoja...tumecherewa lakini 'better late than never'!
 
Hizi kelele za katiba mpya zinapaswa kupigwa bila kukoma, mpaka walioko madarakani wajione kabisa hawana uhalali wa kuongaza nchi. Kwa asili watanzania sio watu wanaoweza kupigania haki zao kwa maandamano kutokana na athari za ujamaa...
Tuanzie hapa JF hakuna kupost habari yoyote zaidi ya kudai katiba mpya kila uzi mwanzo mwisho ni kudai katiba mpya
 
Tuanzie hapa JF hakuna kupost habari yoyote zaidi ya kudai katiba mpya kila uzi mwanzo mwisho ni kudai katiba mpya

Duuu hakuna kupost habari yoyote? Mzee hapo si tutapata katiba ya dunia kabisa. Kimsingi post za kuhusu katiba mpya hazipaswi kukoma humu mitandaoni.
 
Kwa machozi na damu nchi yetu inahitaji muelekeo mpya. Mwelekeo wa kuwaandaa watu wetu na mabadiriko ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Katika ndiyo mwarobaini. Katiba itakayomtambua na kumthamini kila raia, itakayotupa haki ya kuwawajibisha viongozi, itakayoheshimu utu wa raia wote. Wanasiasa hawapaswi kutupangia lini na wapi tunapaswa kupatiwa katiba.
Huo ni upumbavu wako. Katiba iliyopo bado ni bora kuliko unavyodhani. Sisi kama CCM,katiba mpya siyo agenda yetu kwasasa. Full stop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania kuna nyakati hatujijui tunataka nini kwa kweli. Mungu anaipenda nchi yetu, ameonyesha namna ambavyo nchi yetu inaweza kupoteza utulivu kwa kuruhusu yule DIKTETA kututawala kwa miaka 5 na siku 114 kisha akaitoa roho yake. Ametupa Rais mtulivu, msikivu, mfuata utawala wa Sheria na anayemwogopa Mungu kwa matendo na siyo kwa mdomo kama Mwendazake.

Siku ni chini ya 100 toka amechukua nchi na kazi yake tunaiona kuanzia Uhuru wa kujieleza na kukosoa, mikutano ya ndani. ya vyama vya siasa, ajira za waalimi na watumishi wa afya, TRA kuacha dhuluma kwa wafanya biashara, kufutwa kwa kesi za kubambikiza, ujio wa wawekezaji, utayari wa kupambana na COVID 19 na kufunguka kwa dunia ya kidiplomasia.

Hakuna anayejua To Do List ya Rais SSH ina items gani japo mimi naamini la KATIBA MPYA lipo ni suala la wakati. Cha ajabu WAKOSOAJI wa Rais SSH wanamuona hajafanya kitu. Yaani watakapoona Katiba MPYA ndiyo watakubali.

Pengine niwakumbushe, kupata Katiba nzuri ni kitu kimoja na kuheshimu Katiba ni kitu kingine. Katiba hii mbovu ya sasa yule Mwendazake alikuwa anaivunja anavyotaka. Tumpongeze kwanza huyu Samia ambaye anaiheshimu pamoja na mapunhugu yake.
 
Mmerudisha zile billion 30 mlizokula kama posho kwenye bunge la katiba alafu mwishoni mkatoka nje na kwenda kuunda UKAWA?

Tutakuwa na uhakika gani kama hamtakula posho na kutoka nje tena?

Unaongea utoto gani dogo?
 
Huo ni upumbavu wako. Katiba iliyopo bado ni bora kuliko unavyodhani. Sisi kama CCM,katiba mpya siyo agenda yetu kwasasa. Full stop.

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM sio watanzania wote, kuwa na adabu basi hata kidogo, upumbavu ni kudhani kwamba kila mtanzania anaunazi maandazi wa vyama uchwara!!! Tupo ambao ni free souls, free minded individuals, tukiziangalia siasa za nchi kwa jicho la mbali kabisa.
 
Hizi kelele za katiba mpya zinapaswa kupigwa bila kukoma, mpaka walioko madarakani wajione kabisa hawana uhalali wa kuongaza nchi. Kwa asili watanzania sio watu wanaoweza kupigania haki zao kwa maandamano kutokana na athari za ujamaa, na kutawaliwa na chama kimoja kwa muda...
Kudai katiba mpya si lelemama. Kelele tu hazitoshi. Hili linataka nguvu kubwa hasa kwenye uratibu na kusukuma mbele jitihada ndani ya changamoto zozote:

Wenye pumzi ya kutufikisha hapo ni watu wenye uthubutu na dhamira ya kweli. Hawa labda ni kama Chadema, Shura ya ma Imamu, na wa namna hiyo.
 
Kwa machozi na damu nchi yetu inahitaji muelekeo mpya. Mwelekeo wa kuwaandaa watu wetu na mabadiriko ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Katika ndiyo mwarobaini. Katiba itakayomtambua na kumthamini kila raia, itakayotupa haki ya kuwawajibisha viongozi, itakayoheshimu utu wa raia wote. Wanasiasa hawapaswi kutupangia lini na wapi tunapaswa kupatiwa katiba.
Katiba tuliyonayo imepitwa na wakati sana, mambo ya kuteuliwa kama ma-DC na Ma-RC yamepitwa na wakati sana, katiba iturudishie mamlaka ya kuchagua
 
Katiba tuliyonayo imepitwa na wakati sana, mambo ya kuteuliwa kama ma-DC na Ma-RC yamepitwa na wakati sana, katiba iturudishie mamlaka ya kuchagua
Hapa j4 tumeanzisha vuguvugu la kuaida katiba mpya post tofati na kudai kati mpya nikuipoteze
 
Kwa machozi na damu nchi yetu inahitaji muelekeo mpya. Mwelekeo wa kuwaandaa watu wetu na mabadiriko ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Katika ndiyo mwarobaini. Katiba itakayomtambua na kumthamini kila raia, itakayotupa haki ya kuwawajibisha viongozi, itakayoheshimu utu wa raia wote. Wanasiasa hawapaswi kutupangia lini na wapi tunapaswa kupatiwa katiba.
I support you > 100%. Suggest the starting point and alternative move if the same point is wrongly perceived or deliberately frustrated by any authority.
 
Back
Top Bottom