Katiba mpya ni ya wananchi au vyama?

Mroojr

Member
Nov 15, 2010
65
8
Nashangazwa na kauli ya CCM kuingia bunge la katiba kwa misimamo ya chama chao kiasi kwamba wanasahau kuwa iliundwa tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuwa wanataka katiba mpya iweje na nini kiwekwe ili kupata katiba itakayotuongoza. Wabunge wa bunge la katiba mnapoingia bungeni kwa kuelekezwa misimamo ya chama maoni ya wananchi yalikusanywa ya nini. Au serikali ilikuwa inafanya zoezi la kuchezea hela! Ok kwa kuwa wao wameingia na misimamo yao basi na sisi wananchi tujipange kuikwamisha katiba hiyo ktk kura ya maoni ikiwa wataipitisha kuzingatia misimamo yao mpaka hapo watakapozingatia maoni ya wananchi.
 
Back
Top Bottom