Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Ni kweli mkuu unachosema, salary slip, kuwa linapokuja suala la kuendelea kubaki madarakani kwa njia zozote zile, ziwe za halali au haramu, CCM watafanya jambo lolote lile ili mradi liwe linawahakikishia kuendelea kubaki madarakani.CCM hawawezi kujifunza lolote linapokuja swala la kuachia madaraka ya nchi.Mifano ni mingi katika huu ulimwenge lakini wanajitia upofu.
Lakini nieleze kitu kimoja, naweza kuifananisha CCM kwa sasa kama mgonjwa aliyeko ICU ambaye kuendelea kuishi kwake, kunategemea kuendelea kuwekwa 'ON' kwa mitambo ya oxygen inayomsaidia kupumua, na siku madaktari watakapoamua kuchukua maamuzi 'magumu' ya kuswitch 'OFF' mitambo hiyo, ndiyo itakuwa mwisho wa maisha ya huyo mgonjwa.
Vivyo hivyo kwa CCM, hivi sasa wapo ICU na wanapumulia mashine, na 'mashine' hiyo inayowafanya waendelee kupumua si nyingine, bali ni katiba ya zamani ya mwaka 1977, na kama ingetokea katiba hiyo ingefanikiwa kuwa replaced na katiba hii iliyoandaliwa kutokana na maoni ya wananchi, yaliyoratibiwa na Tume ya Warioba, hiyo ingekuwa sawa na mgonjwa aliyeko ICU na madaktari wakaamua kuzima mitambo inayomfanya aendelee kupumua, siku ambayo katiba ya zamani itaseize kutumika nchini, basi tutambue kuwa huo ndiyo utakuwa mwisho wa chama chetu 'kipenzi' cha CCM kuendelea kutawala nchini!
Ni ukweli ambao ni mgumu sana kuupokea, BUT THAT IS PURELY REALITY!