Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima sii hiyari, tudai vyote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima sii hiyari, tudai vyote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Nov 4, 2010.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana Jamaii

  Kwa tangu J3 sijapata usingizi kabisa hasa mara baada ya uchaguzi. Hii ni kutokana na kwamba nilikua na wasiwasi mkubwa hususani hatma ya kura yangu niliyopiga. Jana baada ya Dr Slaa kutoa tamko la mwenendo wa uchaguzi basi usingizi hakuja kabisa mpaka sasa hasubui hii. Dr Slaa jana alisema baadhi ya matokeo ya Urais yamechakachuliwa alitoa mfano kuna Jimbo ana kura 15,000 lakini Tume imetangaza 3,000. Ina maana kuna panga la kura 12,000.

  Inawezekana kura niliyopiga au uliyopiga ni miongozi mwa hizo 12,000. Hii inauma sana na inasikitisha. Pia ni kinyume na haki za binadamu kwa mojibu wa katiba ya sasa. Pia Dr Alisema kulikua na kata hewa ambazo hazipo physically.

  Kwa maana hiyo tutakubaliana na mtu mmoja aliyewahi kutamka kua SISIMU inaweza kutawala milele. Sasa basi nini kifanyike ili kuepusha haya? Mimi nadhani tukianzia na wabunge wote wa upinzani, vyama visivyo na wabunge, taasisi ya haki za binadamu, vyama vya kiraiya na makundi mbalimbali kutia msukumo wa kubadilisha katiba na kua na tume huru ya uchaguzi. Bila hivi viwili kufanyiwa kaza ili kua na katiba mpya kabisa na tume huru ya uchaguzi, swala la utawala wa raiya umma ni ndoto Tanzania. Napata uchungu sana.

  Katiba Mpya kabisa

  1.Itakayoruhusu kuchallenge matokeo yeyote yakiwemo ya urais Mahakamani
  2.Kumwondolea mkuu wa nji kinga
  3.Kupunguza madaraka mengi kwa mtu mmoja
  4.Kuwa na mgombea binafsi
  5.Kuwe na tume huru ya Upinzani
  6.Spika wa bunge na makamu wake wasiwe wanatoka chama kimoja

  Tume Huru Ya uchaguzi

  Tume isiwe inateuliwa na kuriport kwa mtu mmoja, pia wasimamizi wote wasiwe watumishi au wanachama wa chama chochote. Ikiwezekana hii tume iwe inawajibika kwa bunge na sio kwa mtu mmoja. Tume iruhusu matokeo ya ngazi zote kutangazwa kuanzia vituoni, katani, jimboni n.k.

  Makundi yaliyotajwa hapo juu, mvifanyie kazi hivi ili uchaguzi ujao uwe wa raiya/umma na sio kwa matakwa ya mtu Fulani. Bili hivi viwili kufanyiwa kazi uchakachuaji hautaisha kamwe.

  Pia unaweza kusoma...

  1. Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

  2. Tufanyaje tuwe na Tume huru ya Uchaguzi kama Kenya?

  3. Lowassa: Niko tayari kufa nikitetea Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya
   
 2. c

  carmsigwa Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatuhitaji kuongea tunahitaji kutekeleza, saa ya ukombozi ni sasa hatuwezi kukubali nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 iamuliwe mambo yao na kikundi cha watu wasiozidi milioni 1.

  Mabadiriko ya katiba ni lazima angalia uchafu unao jitokeza kwenye katiba ya jamhuri haitambui serikali ya umoja wakitaifa wakati Tanzania visiwani hilo linatambulika, chama kinacho ongoza visiwani ndio hicho hicho kinacho ongoza jamhuri hivi unahitaji elimu yanamna gani kujua uchafu huu.
   
 3. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,708
  Trophy Points: 280
  Hivi kama katiba mpya imeshindikana,uhakika wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi unatoka wapi?

  Ninachojiuliza ni kuwa CCM hao waliokwamisha upatikanaji wa katiba bora ndio hao hao waliopo madarakani.Isitoshe, sheria ya kuunda tume hiyo itatungwa na bunge hili hili lililotawaliwa na CCM.Sasa matumaini ya kupata tume huru yanatoka wapi?!

  Kama ilivyokuwa kwa katiba mpya,ni lini CCM walikuwa na nia ya kuwa na tume huru ya uchaguzi?Hivi mazingira ya kuanzisha mchakato wa katiba mpya yana tofauti gani na mazingira ya kudai tume huru ya uchaguzi?

  Swali lingine ni je wapinzani mmejiandaa vipi kuhakikisha mchakto huu nao hauchakachuliwi?

  Na je,tume huru ikishindikana nini kitafuata?!

  In short,lets get prepared for the same scenario!
   
 4. n

  nkongu ndasu JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2014
  Joined: Jan 19, 2013
  Messages: 22,526
  Likes Received: 3,757
  Trophy Points: 280
  Binafsi sina imani na uwezekano wa kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi. Wabunge wa ccm watafanya kila jitihada ya kuvuruga uwezekano wa kupatikana tume huru ya uchaguzi.
   
 5. Bobwe1

  Bobwe1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 8, 2014
  Messages: 396
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukoo wa panya,baba sharubu mama sharubu na mtoto sharubu.
   
 6. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,708
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa UKAWA wanapaswa kutazama mbali zaidi vinginevyo wataishia kuwa walalamikaji tu na jamii itawachoka.
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2014
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Inabidi wajumbe wa tume ya Uchaguzi waapatikane kutoka katika vyama vya Siasa vilivyo na wawakilishi Bungeni. CCM,CDM,CUF na NCCR wapendekeze majina ya Watendaji wakuu katika tume ya Uchaguzi
   
 8. manning

  manning JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 1, 2013
  Messages: 3,514
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  umenena mkuu hapa ukawa wajiandae kwa kszi nyingine pevu iliyo mbele yao, ila kwa msimamo waliounyesha kwenye katiba i funzo tosha kwa CCM yenye akili.
   
 9. NAKEMBETWA

  NAKEMBETWA JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,449
  Likes Received: 2,455
  Trophy Points: 280
  inabidi Jaji Joseph Sinde Warioba ndio awe mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi, hapo ndio nitaamin hyo tume ni huru!
   
 10. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,708
  Trophy Points: 280
  CCM hawawezi kujifunza lolote linapokuja swala la kuachia madaraka ya nchi.Mifano ni mingi katika huu ulimwenge lakini wanajitia upofu.
   
 11. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,708
  Trophy Points: 280
  Huyo atapingwa kwa nguvu zote.
   
 12. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,897
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  Nani amekuwaambia kuwa katiba mshindikana.
   
 13. Simiyu Yetu

  Simiyu Yetu JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 29, 2013
  Messages: 18,897
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  Au mzee mtei nayo imekaa vema.
   
 14. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2014
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,002
  Likes Received: 37,708
  Trophy Points: 280
  Katiba ya CCM nani ataikubali zaidi yenu?
   
 15. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2014
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mawazo mazuri!!!!! Umeona mbali sana mkuu!!!!!!!
   
 16. m

  mshumbue-soi JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2014
  Joined: Aug 28, 2013
  Messages: 1,840
  Likes Received: 786
  Trophy Points: 280
  Na bunge linaloenda kutunga sheria ya tume huru ni lile la NDIOOOoOOOO ndiyo nini HAWAJUI
   
 17. Buldoza

  Buldoza JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2014
  Joined: May 2, 2013
  Messages: 2,303
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Unajitoa ufahamu enhee!
   
 18. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,523
  Trophy Points: 280
  Ikishindikana tunaahirisha uchaguzi mkuu wa mwakani hadi yawepo makubaliano.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Sep 11, 2014
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii hadith nyingine tena mbaya zaidi kwa sababu yale yale yalofanyika mwaka 1984 ya kuondoa Azimio la Arusha kwa maslahi ya viongozi wa chama na mwaka 1992 kuridhia demokrasia ili tupewe mikopo lakini kwa maslahi ya chama tawala ndio yatafanyika tena - MABADILIKO mapya.

  Sisi wananchi tuliitaka KATIBA MPYA ili baada ya uchaguzi ujao wa mwaka 2015 tusiongozwe tena na katiba ya mwaka 1977, maajabu ya Mussa jambo kubwa kwa wananchi limetupwa kipindoni sasa inatazamwa tena mambo ya kuwarahishia wanasiasa kututawala na katiba ile ile tuloikataa kwa miaka sijui mingapi ijayo. Tume haiwezi kuwa huru ikiwa rais atakuwa na mamlaka makubwa kiasi kile kile na hamuwezi kumshitaki - Haiwezekani.

  Ama Kweli Miafrika ndivyo Tulivyo..
   
 20. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #20
  Sep 12, 2014
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,960
  Likes Received: 6,725
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa unachosema nkongu ndasu, lakini vile vile tukumbuke kuwa hata huku kuanza kwa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, haukuanza kwa 'mapenzi' ya CCM, bali ilitokana na shinikizo kubwa sana, kutoka kwa makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii.

  Kwa maana hiyo basi , let's hope for the best, the same spirit which enabled our country to 'launch' starting 'fetching' the path of having new constitution, can also enable us having 'real' National Electoral Commission!
   
Loading...