Katiba mpya-kusiwe na 'presidential appointees' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya-kusiwe na 'presidential appointees'

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by TWIZAMALLYA, Mar 21, 2012.

 1. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa watu wanakuwaga ni tatizo sana. na huwa wanakuwa jeuri mno kwa mamlaka zingine za nchi ila tu wanakuwa watiifu kwa aliyewachagua
   
 2. kiagata

  kiagata Senior Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Hilo jambo ni kubwa katika Nchi zetu za Dunia ya tatu ni tatizo,ila katika nchi za wenzetu hakuna.(ulaya)
  1.Una mchagua mtu akuwakilishe ktk masuala fulani ukitambua unamjua sababu mlisoma naye,yeye ndiyo anakuangusha.
  2.Pia anajua huwezi kumfanya lolote sababu utamwonea haya na mnaongea kabila moja.
  * Ulaya hakuna sababu ukabila hakuna,lugha ni moja na ndugu yako ni yule anayeweza kukuletea faida katika kazi/biashara yako(hata kama siyo ndugu).
  Hivyo bado tuna safari ndefu katika kumaliza hili.
   
 3. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa wale watakaopata nafasi ya kuteuliwa kwenye tume ya kuboresha katiba ya nchi mambo haya lazima wayazingatie kwa manufaa ya nchi. kipindi cha KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI kimepitwa na wakati maana kudumu kwa chama kunatugharimu mno.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya inatakiwa, pamoja na mambo mengine ihakikishe yafuatayo:

  (a) Mikoa ifutwe.
  (b) Kila wilaya iwe na serikali yake ikiongozwa na wakuu wa wilaya waliochaguliwa na wanachi.
  (c) Muundo wa serikali kuu na serikali za wilaya uwe kwenye katiba; rais asichague watu wengi kuunda serikali kwa vile eti ni marafiki yake. Idadi ya wizara iwe kwenye katiba na wala kusiwe na mabadiliko ya kiholela kwenye muundo wa serikali.
  (d) Uteuzi wa mawaziri ufanywe na Bunge, Rais awe ni mpendekezaji tu. mapendekezo ya Rais yanaweza kukataliwa na bunge.
  (e) Uapishwaji wa rais baada ya uchaguzi lisiwe ni jambo la haraka haraka; baada ya uchaguzi kuwe na muda wa kutosha kabla hajaapishwa ili watu wanaopinga uhalali wa uchaguzi wake wapate nafasi ya kufanya hivyo.
  (f) Iwe ni halali kumshitaki raisi akishamaliza muda wake au hata akiwa madarakani; itasaidia maraisi wasifanye maamuzi ya kijinga wakidhani kuwa wako immune.
  (g) Kuwe na muundo maalum unaosimamia uteuzi wa Majaji, Mabalozi, na makamanda wa maheshi yetu ya ulinzi na usalama, na makatibu wakuu wa mawizara kusudi teuzi hizi sisiwe za kisasa.

  (h) Rais assingilie utezui wa viongozi wa mashirika yote ya umma kama vile vyuo vikuu, NSSF, TANESCO, Posta, TRC, na mabenki, Watu wanotaka nafasi wawe waname maombi ya nafsi hizo, wasailiwe na kuajiliwa bila kuteuliwa na rais.

  Nitaongeza mengine nikipita nafasi
   
 5. N

  Naffanya New Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  looks good !
   
Loading...