Katiba mpya iwe na kipengele cha presidential debate

nyotanjema

Senior Member
Sep 24, 2011
136
32
Heshima kwenu wana JF.

Nimepata kufatilia mijadala inayoendelea kuelekea uchaguzi mkuu wa Marekani kwa bahati nzuri nikashawishika kutambua yafuatayo

  • Huwezi kuwa Rais wa Marekani kirahisi kama huko nyumbani/ africa inavyokuwa .
  • Inabidi uwe na akili za ziada katika kujua kiuhalisia kile unachotetea maana inabidi uifahamu vizuri nchi yako na matatizo au challenge kwa ujumla maana kama ni siasa basi hizi zimekomaa sana huwezi kwepa maswali wala kuong'opa watu wanajua ukweli.(Huwezi kuwa Rais kama wewe ni kilaza na mpiga siasa tu)
Baada ya kung'amua hayo machache kati ya mengi nikaona ni dhahiri sasa katika katiba mpya PRESIDENTIAL DEBATE inabidi iwepo.

Nawasilisha (TUNAWEZA KUJADILI)
 
Hakuna kujadili kitu cha kipuuzi kama hiki. Unaonyesha hata katiba ya Tanzania inayotumika sasa au ya Marekani bado ujaisoma. Sio kila utaratibu wa unaotumika na jamii lazima uwepo kwenye katiba.

Na sio lazima uwe na katiba hili nchi iendelee vizuri au iwe na demokrasia ya kweli. Uingereza haina katiba.
 
Acha uongo, wiingreza ina unwritten constitution, hii haina maana hawana katiba! Kuna aina mbili za katiba written and unwritten! Kuhusu kuwa presidential debate ni muhimu sana, hapa tanzania CCM imekuwa ikikwepa midahalo ya marais kwanini, hata 2010 waliwakwepesha wabunge wao midahalo! Ikibidi hili swala liwe la kisheria ili lifanyike be it! Hatuwezi kucha mwanya kwa vilaza kuongoza nchi!
 
Ndio mimi muongo. Wanayo unwritten constitution. Lakini point yangu ni sio kila kitu kinachoendesha jamii ni lazima kiwe codified katika katiba (kipengere).

Mdahalo haumo katika katiba ya Marekani. Na wagombeaji hawalazimishwi kwenda kwenye midahalo. Vilevile high performance in speech delivery doesn't translate to work performance.

Take for example Messiah Obama. He's a gifted orator, but his work performance has left a lot to be desired.
 
Naunga mkono 100% kuwe na mdahalo kwa wagombea urais, itasaidia taifa letu sana kujua viongozi wanaotaka kwenda magogoni, JK alikimbia mdahalo 2010 na madhara yake yameonekana wazi
 
Mdahalo kwa wagombea wote ni muhimu sana. Lazima kuwe na kipengele cha kuwabana wagombea kushiriki kwenye midahalo kwenye Sheria ya Uchaguzi. Naungo mkono kabisa jambo hili.
 
Hii ni zuri ila ianze kwa wake wa wagombea. Unajua nchi yetu inakufa kwa sababu hii. Mke wa rais ana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi.

Ndo anakaa na rais masaa mengi, hivyo anamchango wa mawazo pengine kuliko washauri wa rais.

Hakuna kujadili kitu cha kipuuzi kama hiki. Unaonyesha hata katiba ya Tanzania inayotumika sasa au ya Marekani bado ujaisoma. Sio kila utaratibu wa unaotumika na jamii lazima uwepo kwenye katiba.

Na sio lazima uwe na katiba hili nchi iendelee vizuri au iwe na demokrasia ya kweli. Uingereza haina katiba.

Sio kweli kuwa haina katiba!!!!!!!!!!!!!!!!!!bali haina written katiba. Huwezi kuendesha nchi bila katiba, where do you base your maamuzi
 
Nyota Njema na Wana JF,
Mkuu wazo hili ni zuri kwa Ustawi wa Nchi, Na kuongezea iwepo Debate zaidi ya Moja, ziwe kama 3 au 4 hivi Mikoa tofauti, Kusini na Kaskazini, Mashariki na Magharibi, Kuwe moja Moderator awe na Maswali yake mada iwe ya Maswala ya Ndani, nyingine ya Watazamaji kuuliza Maswali, na nyingine aka zingine.
Hii itasaidia kila mwenye Nia ya kugombea Urais tumpime Ujuzi na Matarajio yake kwa Nchi Yetu aka Yake
Nawakilisha

Heshima kwenu wana JF.

Nimepata kufatilia mijadala inayoendelea kuelekea uchaguzi mkuu wa Marekani kwa bahati nzuri nikashawishika kutambua yafuatayo

  • Huwezi kuwa Rais wa Marekani kirahisi kama huko nyumbani/ africa inavyokuwa .
  • Inabidi uwe na akili za ziada katika kujua kiuhalisia kile unachotetea maana inabidi uifahamu vizuri nchi yako na matatizo au challenge kwa ujumla maana kama ni siasa basi hizi zimekomaa sana huwezi kwepa maswali wala kuong'opa watu wanajua ukweli.(Huwezi kuwa Rais kama wewe ni kilaza na mpiga siasa tu)
Baada ya kung'amua hayo machache kati ya mengi nikaona ni dhahiri sasa katika katiba mpya PRESIDENTIAL DEBATE inabidi iwepo.

Nawasilisha (TUNAWEZA KUJADILI)
 
Ndio mimi muongo. Wanayo unwritten constitution. Lakini point yangu ni sio kila kitu kinachoendesha jamii ni lazima kiwe codified katika katiba (kipengere).

Mdahalo haumo katika katiba ya Marekani. Na wagombeaji hawalazimishwi kwenda kwenye midahalo. Vilevile high performance in speech delivery doesn't translate to work performance.

Take for example Messiah Obama. He's a gifted orator, but his work performance has left a lot to be desired.

Mimi sijakujibu hoja ya debate kuwepo kwenye constitution, nilikujibu hoja yako ya kusema wiingereza hawana constitution! Uko sahihi kuwa si lazima kila kitu kiwe kwenye constitution, ila lazima kiwekewe mfumo ili kifanyike, kwa mfano marekani wana chombo kinachoitwa commision for presidential debates, zile debate is not for fun they change voters opinion, mfano performance mbovu ya Obama kwenye first debate ilimporomosha kwenye opinion polls, siyo hiari tena mgombea kuhudhurua debate ni lazima unless hataki kuwa rais wa marekani!
 
Mwisho wa siku mdahalo utasaidia nini? Watanzania sidhani ka huwa wanapiga kura kwa kuangalia sera za chama. Asilimia kubwa hata kama kampeni hazijaanza anajua atapiga kura kwa chama gani.
We mwenyewe nina uhakika hadi sasa tayari kura yako ipo kwa chama gani 2015 hata kama kuna chama kingine kitakuwa na sera nzuri kuliko hicho chama chako.
 
Back
Top Bottom