Katiba Mpya: CHADEMA, CUF na NCCR- Mageuzi wakutana na wanahabari Sept 15, 2013

nyantella

Pumba ni pumba tu hata ukiziandika kwa kimombo zitabaki kuwa pumba tu. Uliposema katiba haina umuhimu badala yake tuongelee gesi nikaacha hata kusoma post yako. Hivi si ndiyo hiyo gesi wanayoingia nayo mikataba ya siri. Hivi si ndiyo hii katiba mpya ambayo inatamka mikataba iwe ya uwazi.

Sasa mbona sioni uhusiano wa ulichokiandika. Acha kulewa na upuuzi wa CCM kwa kigezo cha kupata buku saba Lumumba
 
Last edited by a moderator:
Afica, africans!! we never learn any lesson! libya had every thing, now it is nothing but ruins and a gun for everybody, Egypt is burning and TZ is now another egypt in a making! tunastahili kwenda huko tunako kutaka kwa unafiki wetu! tunaimba "...Taanzania tanzania, nakupenda kwa moyo wote halafu watu hao hao tunapanga kuivunja! shem on you all!! tunaimba tazama ramani utaona nchi nzuri,..... blah blah halafu tupo mstari wa mbele kuitokomeza kwenye ramani ya dunia!, tunimba Mungu ibariki Tz halafu tunafanya nini kuhusu hiyo Tanzania? afadhali wakenya wamepata matumizi ya jina Tanzania sasa hivi ni brand ya majani ya chai halafu humu humu tunalalama ohh wameiba jina letu, ......blah, blah!
CCM at least wanaonyesha wakiimba Taanzania, Tanzania they mean it!, wkiimba tazama ramani they mean it!, wakiapa kuitetea katiba they mean it! wana mapungufu mengi though lakini sii wanafiki! and kwa watu wenye akili issue sii katiba! issue ni gas! waafrika tulilaaniwa mali asili zituangamize badala ya kutunufaisha! Julius aliliona hili mapema akaamua kivyake watu hawkumuelewa now we are in ngoja tuone maana if we do not know where we are going, any way will take us there, in the name of katiba!

Inaelekea CCM mna Tanzania yenu ndani ya Tanzania!!! Ndiyo maana mnataka katiba yenye maslahi kwenu.
 
image.jpg More pics
 
Katiba kumng'oa JK

na George Maziku

Tanzania Daima

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa asaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 ili iwe sheria, viongozi wa upinzani nchini wameamua kuanza mchakato wa kumng'oa kiongozi huyo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Wenyeviti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), leo wanatarajia kukutana na wahariri na waandishi wa habari kueleza mikakati na mbinu watakazozitumia kunusuru taifa lisiingie kwenye utungaji wa Katiba mpya itakayobeba masilahi ya chama tawala.

Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa mikutano ya hadhara, maandamano na elimu kwa umma juu ya athari ya muswada huo ni miongoni mwa mbinu zitakazotumiwa kuhakikisha Rais Kikwete hasaini muswada huo au serikali inapeleka tena mabadiliko ya sheria hiyo katika Bunge lijalo iwapo rais atasaini.
Wapinzani wanadai kuwa serikali iliubadili kwa nguvu muswada huo kwa kuondoa maoni muhimu ya wadau, pia walilalamikia kitendo cha wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge kutokwenda Zanzibar kuchukua maoni ya upande huo wa muungano.

Wakati wapinzani wakijipanga kuweka wazi mikakati ya kumshinikiza Rais Kikwete asisaini muswada huo, wadau mbalimbali wamemtaka kiongozi huyo atumie busara ili taifa lipate katiba itakayokuwa na manufaa kwa taifa kuliko inavyoonekana itikadi za vyama kugubika mchakato huo.
Wiki iliyopita akiwa Dodoma, Mbowe alikionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa wasitarajie kuwa kupitishwa kwa marekebisho ya muswada huo ndiyo Katiba mpya, bali kura ya maoni ndiyo itakayoamua jambo hilo.

Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa wapinzani wamejipanga kuhakikisha wananchi wanaitumia kura ya maoni kupinga mpango wa Rais Kikwete na serikali yake kupitisha Katiba mpya yenye mwelekeo wa kukibeba chama tawala.

Hoja za wapingaji
Kamati Maalumu ya Katiba, nayo imepinga marekebisho ya muswada huo ikiainisha eneo mojawapo lenye tatizo ni kuruhusu asilimia 72 ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kubeba wanasiasa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Khoti Kamanga, alisema iwapo Katiba mpya itaundwa bila upungufu unaoonekana sasa kupatiwa ufumbuzi itazalisha migogoro zaidi, itakayosababisha nchi kuingia kwenye machafuko.

Alikosoa Kifungu cha 8 na Kifungu kidogo cha 4 na 5 cha muswada huo kwamba vina kasoro, kwa kuruhusu wabunge wa Bunge la Katiba kufanya uamuzi kwa wingi wa kura badala ya kutumika utaratibu wa theluthi mbili kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, naye anapinga muswada huo kwa madai kuwa una upungufu mkubwa, ukiwamo wa Zanzibar kutoshirikishwa, pia kumpa nafasi kubwa rais kuteua watu kutoka katika asasi mbalimbali badala ya watu hao kuteuliwa moja kwa moja na asasi au asasi husika.
Hofu ya yaliyotokea Kenya

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa Tanzania inafuata njia iliyopitwa na Kenya katika kupata katiba mpya, ambayo ilipatikana baada ya kutokea machafuko mwaka 2007 mara baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.

Mwaka 2005, wananchi wa Kenya wakiongozwa na wanasiasa maarufu, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka, waliibwaga serikali ya rais mstaafu wa nchi hiyo, Mwai Kibaki, katika kura ya maoni ya kuamua kuikubali au kuikataa rasimu ya katiba iliyokuwa imependekezwa na utawala wa rais Kibaki.
Ni kutokana na matokeo ya kura hiyo, uchaguzi mkuu wa 2007 ulizaa machafuko na mauaji ya mamia ya Wakenya wasiokuwa na hatia, baada ya kushindikana kupatikana kwa katiba mpya, hivyo utawala wa Kibaki kuamua kuitisha uchaguzi mkuu kwa kutumia katiba na sheria za uchaguzi za zamani zilizokuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu.

Wachambuzi wa siasa hapa nchini wanasema kuwa mwenendo wa hivi karibuni wa mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Tanzania unaonesha ishara za wazi za kutokea yaliyotokea nchini Kenya. Kwamba, kushindwa kufikia mwafaka baina ya wabunge wa Bunge la Tanzania lililomaliza vikao vyake hivi karibuni mjini Dodoma, kuhusu muundo wa Bunge Maalumu la Katiba ni uthibitisho wa wazi wa matatizo yanayoweza kutokea siku za usoni.

Bunge Maalumu la Katiba ndilo litakaloandaa rasimu ya mwisho ya Katiba mpya itakayopelekwa kwa wananchi mapema mwakani kwa ajili ya kura ya uamuzi, hivyo muundo wake na kukubalika kwake ni jambo muhimu na linalohitaji mwafaka wa kitaifa.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilipeleka mapendekezo ya kutaka uwakilishi wa Bunge hilo upanuliwe kutoka wajumbe 600 wa sasa na kuwa wajumbe 789 ili kulifanya bunge hilo lisihodhiwe na wanasiasa ambao zaidi ya asilimia 70 ni wanachama wa CCM.

Hata hivyo, pendekezo hilo lilishindwa baada ya wabunge wa CCM kutumia wingi wao katika Bunge hilo kuyakwamisha mapendekezo ya upinzani na badala yake kuamua kuendelea na muundo wa sasa unaoipa CCM haki ya kisheria ya kulihodhi Bunge la Katiba.
Wachambuzi hao wanatabiri kuwa kama Rais Jakaya Kikwete atakubaliana na msimamo wa wabunge wa chama chake, kwa kuitia saini sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba na hatimaye kuwa na Bunge la Katiba na baadaye kura ya maoni, basi kuna uwezekano katiba hiyo mpya ikakataliwa na wananchi katika kura ya maoni kama ilivyokuwa kwa Kenya mwaka 2005.

Kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya 2011, kama wananchi wataikataa katiba inayopendekezwa, basi katiba ya zamani itaendelea kutumika katika shughuli zote za nchi, ikiwamo kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, jambo ambalo linapingwa vikali na viongozi, wanachama, wafuasi wa vyama vya upinzani na wanaharakati.
Ni kutokana na mazingira haya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini wanaamini na kutabiri kuzuka kwa ghasia, machafuko na umwagikaji wa damu kama ilivyotokea Kenya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Alli, anasema: "Tunakabiliwa na hatari mbele yetu, maana tunakwenda kwenye kura ya maoni kuhusu Katiba mpya tukiwa tumemeguka vipande vipande. Tulipaswa kufika huko tukiwa wamoja kama taifa, tulipaswa kuwa na mwafaka wa kitaifa katika suala hili la katiba ya nchi badala ya kwenda kwa kuongozwa na itikadi zetu za kisiasa," alieleza Bashiru na kuongeza:
"Machafuko na mauaji yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 yalitokana na makosa ya utawala wa rais mstaafu wa nchi hiyo, Mwai Kibaki, ambaye aliamua kuwadharau na kuwapuuza wananchi katika mchakato wa kuunda katiba ya nchi yao kama inavyofanyika sasa nchini mwetu, hili ni jambo la hatari sana," alionya Bashiru.

Bashiru anasema kuwa ili kuufanya mchakato wa sasa wa Katiba mpya kuwa wa wananchi na kuepusha kuiingiza nchi kwenye machafuko na mauaji ya wananchi wasio na hatia, mchakato wote unapaswa kurudiwa.
"Ili yasitufike yaliyotokea Kenya, tunapaswa kuanza upya mchakato wa Katiba mpya, wananchi wapewe fursa ya kuumiliki mchakato mzima. Kwa mfano, wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanapaswa kuchaguliwa na wananchi, si kuteuliwa. CCM na wapinzani wanataka wajumbe wapatikane kwa kuteuliwa, mimi nasema huo si utaratibu sahihi, dhana ya Bunge la Katiba inataka wajumbe wake wapatikane kwa kuchaguliwa na wananchi, si kuteuliwa," anabainisha Bashiru.

Ulivyopitishwa
Mjadala wa muswada huo uliopitishwa Ijumaa iliyopita na wabunge wengi wakiwa wa CCM, ulizua tafrani bungeni iliyosababisha Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) kutolewa nje na askari. Katika tafrani hiyo, baadhi ya wabunge wa upinzani walirushiana makonde na maofisa usalama, huku wabunge wote wa upinzani, isipokuwa Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, wakiususia.

Afica, africans!! we never learn any lesson! libya had every thing, now it is nothing but ruins and a gun for everybody, Egypt is burning and TZ is now another egypt in a making! tunastahili kwenda huko tunako kutaka kwa unafiki wetu! tunaimba "...Taanzania tanzania, nakupenda kwa moyo wote halafu watu hao hao tunapanga kuivunja! shem on you all!! tunaimba tazama ramani utaona nchi nzuri,..... blah blah halafu tupo mstari wa mbele kuitokomeza kwenye ramani ya dunia!, tunimba Mungu ibariki Tz halafu tunafanya nini kuhusu hiyo Tanzania? afadhali wakenya wamepata matumizi ya jina Tanzania sasa hivi ni brand ya majani ya chai halafu humu humu tunalalama ohh wameiba jina letu, ......blah, blah!
CCM at least wanaonyesha wakiimba Taanzania, Tanzania they mean it!, wkiimba tazama ramani they mean it!, wakiapa kuitetea katiba they mean it! wana mapungufu mengi though lakini sii wanafiki! and kwa watu wenye akili issue sii katiba! issue ni gas! waafrika tulilaaniwa mali asili zituangamize badala ya kutunufaisha! Julius aliliona hili mapema akaamua kivyake watu hawkumuelewa now we are in ngoja tuone maana if we do not know where we are going, any way will take us there, in the name of katiba!

Really???!!! Eti CCM wakiimba Tanzania, Tanzania they mean it!!! U must be joking, unaijua CCM vizuri lakini unataka kupindisha ukweli, an' why r u so pessimistic?? Sio kila mahali panaweza kuwa Egypt au Libya.
 
Maalim seif yuko serikalini hataki huo muungano maana atakosa kula yake.

Acha kutumia vibaya akili yako Maalim Seif ni mtendaji mkuu wa chama Cha Cuf angekuwa hataki lisingefikia hapo..Yaan Jf mtu akitunga uongo wake ww unaamin tu.Ipo cku Mtu ataandika ww umefanywa vibaya Je Tuamini?
 
Afica, africans!! we never learn any lesson! libya had every thing, now it is nothing but ruins and a gun for everybody, Egypt is burning and TZ is now another egypt in a making! tunastahili kwenda huko tunako kutaka kwa unafiki wetu! tunaimba "...Taanzania tanzania, nakupenda kwa moyo wote halafu watu hao hao tunapanga kuivunja! shem on you all!! tunaimba tazama ramani utaona nchi nzuri,..... blah blah halafu tupo mstari wa mbele kuitokomeza kwenye ramani ya dunia!, tunimba Mungu ibariki Tz halafu tunafanya nini kuhusu hiyo Tanzania? afadhali wakenya wamepata matumizi ya jina Tanzania sasa hivi ni brand ya majani ya chai halafu humu humu tunalalama ohh wameiba jina letu, ......blah, blah!
CCM at least wanaonyesha wakiimba Taanzania, Tanzania they mean it!, wkiimba tazama ramani they mean it!, wakiapa kuitetea katiba they mean it! wana mapungufu mengi though lakini sii wanafiki! and kwa watu wenye akili issue sii katiba! issue ni gas! waafrika tulilaaniwa mali asili zituangamize badala ya kutunufaisha! Julius aliliona hili mapema akaamua kivyake watu hawkumuelewa now we are in ngoja tuone maana if we do not know where we are going, any way will take us there, in the name of katiba!
Tofautisha uasi, na demokrasia ya vyama vingi.

Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
 
Bora mtafute nguvu ya kuhuzunika pamoja 2015 maana kipigo cha karne kitakua na mshindo mkubwa wakati ccm inaelekea Ikulu 2015,
Je safari hii wataiba kwa mtindo upi? Watatumia ule waliotumia uchaguzi uliopita au watakuja na mpya? Hii ni kwa kuwa bila hiyo no way out!!
 
Tanzania itajengwa na watanzani wenyewe na sio kikundu cha watu wachache wenye masilahi yao binafsi wakidhania kuwa waweza kufanya chochote watakacho,katiba ya nchi sio ya chama furani au watu fulan au kikundi cha watu fulan, kinachotakiwa ni kutengeneza katiba ambayo haiegemei upande wowote ule, nahdan Mungu yu pamoja nasi na atatuongoza tutayafikia malengo ya kuwa na katiba ya watanzania na sio ya mtanzania na isiyo pendelea upande wowote Ee MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE
 
Back
Top Bottom