Kikwete akiwa na busara asisaini hicho kipeperushi cha genge la Sitta walichokipitisha wiki iliyopita hapo Dodoma kama Rasimu ya katiba kwani itamletea fedheha huko mbele!!! Hakuna uwezekano hata siku moja kuwa baraza la wawakilishi wataipitisha hiyo Rasimu na huo ndio utakuwa mwisho wake hata kabla ya REFERUNDUM huko Zenj!!! Sitta na genge lake wamefanikiwa kuhalalisha matumizi makubwa ya fedha ya bunge la katiba kwa kupitisha kipeperushi ambacho hakiwezi kukubalika na Zanzibar kama ni katiba; kusaini hiyo document iliyopitishwa kiujanja ujanja na baadae kukwama huko Zanzibar ni sawa na kupokea cheki ya fedha ambayo tarakimu na maneno ya thamani ya hiyo cheki ni tofauti hivyo huwezi kucash benki na ukapata fedha!! Kwa vile kikwete amezoea kupokea cheki za aina hiyo basi pengine atasaini hicho kipeperushi!!!