Katiba Mpya Bado Shughuli Pevu-Warioba

Katiba Mpya Bado Shughuli Pevu-Warioba

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Bunge Maalumu la Katiba kupitisha Katiba inayopendekezwa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Katiba hiyo bado ina maswali mengi kuliko majibu, hasa katika muungano na mgombea binafsi.

Amesema licha ya Zanzibar kuridhia mambo kadhaa kuwekwa katika orodha ya mambo ya muungano, hali inaweza kuwa tofauti ukifikia wakati wa Zanzibar kubadili Katiba yao ili kuwezesha utekelezaji wa mabadiliko hayo.

Juzi Bunge hilo lilipitisha Katiba inayopendekezwa kwa tofauti ya kura mbili na kuhitimisha kwa sasa mchakato wa kuandika Katiba hadi mwaka 2016 ambapo litafanyika zoezi la upigaji wa kura ya maoni.

Akizungumza na Mwananchi Jumamosi jana, Jaji Warioba alisema, “Wasiwasi wangu ni juu ya muungano kwa sababu katika masharti ya mpito ni lazima Zanzibar ifanye marekebisho ya Katiba yake. Rasimu inayopendekezwa inasema Tanzania itakuwa nchi moja pamoja na madaraka ya rais kugawa nchi. Kwa maana hiyo lazima Katiba ya Zanzibar ibadilike.”

Alisema katika mambo ya muungano, Katiba inayopendekezwa imeliweka suala la kodi ambalo halikuwamo katika rasimu iliyotolewa na Tume ya Katiba, kusisitiza kuwa kitendo hicho hakitajibu swali la ‘Tanganyika kuvaa koti la Muungano’.

“Wameongeza kodi ya mapato, ushuru wa forodha na bidhaa katika mambo ya muungano. Maana yake ni kwamba kodi yote inayokusanywa, ikiwamo ya kutoka Zanzibar itaingizwa kwenye mfuko wa muungano,”alisema.

Aliongeza, “Wakati huo huo Zanzibar imepewa uwezo wa kusimamia mambo yake yenyewe na ili iweze kulitekeleza hilo ni lazima iwe na vyanzo vyake vya mapato. Sasa watasimamiaje wakati mapato yote yanaingia kwenye mfuko wa muungano.”

Alisema ili suala hilo liweze kutekelezwa ni lazima Zanzibar ibadili Katiba yake na kusisitiza kuwa utakapofika wakati wa kubadili Katiba ya Zanzibar, jambo hilo linaweza kukwama.

“Sioni kama Wazanzibar watakubali suala hili. Kama mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yatakwama, ni wazi kuwa Katiba inayopendekezwa haitatekelezeka. Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yanategemea maridhiano ya Wazanzibari wenyewe na kumbuka kuwa CUF na CCM wanavutana sana,” alisema Jaji Warioba.

Akifafanua hilo, alisema mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar lazima yapate theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kusisitiza kuwa kwa mvutano wa vyama hivyo viwili visiwani Zanzibar, itakuwa kazi ngumu kupitisha jambo hilo.

“Katiba ya Zanzibar isipobadilishwa kero za muungano zinazozungumzwa zitaendelea. Kazi iliyopo sasa ni kufikiria maridhiano kuhusu muungano, lazima tuhakikishe Zanzibar imekubali kubadili katiba yake na kuridhia mapato yake kuingizwa katika mfuko wa muungano,” alisema.

Aliongeza, “Kama ambavyo Tanzania Bara waliitegemea Zanzibar kupitisha Katiba inayopendekezwa, ni lazima pia ihakikishe kuwa Zanzibar inakubali kubadili Katiba yake.”
 
Kuhusu mgombea huru Jaji Warioba alisema, "Katiba inayopendekezwa imeweka masharti ya mgombea ubunge na kutaja sifa za ziada za mgombea huru ambazo ukizitazama kwa undani utabaini kuwa wanamkataa mgombea huru kistaarabu."

Alisema sifa hizo za ziada walitakiwa kuwekewa na wagombea wengine, si mgombea huru pekee.

"Mfano ni kutoruhusu mtu kutoka katika chama cha siasa kisha kugombea kama mgombea huru," alisema.

Jaji Warioba aliyataja baadhi ya mambo ya msingi yalikuwamo katika rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuingizwa tena katika Katiba inayopendekezwa kuwa ni malengo muhimu ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimazingira.

Source: Mwananchi Jumapili Oktoba 5 2014
 
nashindwa hata niseme nn ila nikupongeze tena kwa kuonyeshe kiasi gani taaluma yako ya sheria ilivo mkombozi kwa taifa hili
 
Huyu Warioba kapewa nini na Wazanzibari? Mbona wenyewe wamekaa kimya yeye anachonga tuu kila siku!
 
nashindwa hata niseme nn ila nikupongeze tena kwa kuonyeshe kiasi gani taaluma yako ya sheria ilivo mkombozi kwa taifa hili
Huyu mzee Warioba ni mchawi/adui wa Muungano wetu! Apingwe kwa gharama yoyote!
 
Kuhusu mgombea huru Jaji Warioba alisema, “Katiba inayopendekezwa imeweka masharti ya mgombea ubunge na kutaja sifa za ziada za mgombea huru ambazo ukizitazama kwa undani utabaini kuwa wanamkataa mgombea huru kistaarabu.”

Alisema sifa hizo za ziada walitakiwa kuwekewa na wagombea wengine, si mgombea huru pekee.

“Mfano ni kutoruhusu mtu kutoka katika chama cha siasa kisha kugombea kama mgombea huru,” alisema.

Jaji Warioba aliyataja baadhi ya mambo ya msingi yalikuwamo katika rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuingizwa tena katika Katiba inayopendekezwa kuwa ni malengo muhimu ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimazingira.

Source: Mwananchi Jumapili Oktoba 6 2014
Mgombea huru anatakiwa kuwa huru kweli kweli, sio kutapatapa tu mara uko huku, mara kule!
 
Huyu Warioba kapewa nini na Wazanzibari? Mbona wenyewe wamekaa kimya yeye anachonga tuu kila siku!

Hoja yako ni ipi? Hivi Znz si sehemu y a Tz?
Try to think outside the box, u may see the arguements of Judge Warioba.
Are u trying to tell us to have similar understanding for each n every thing?
You may wish to know that our differences are our important resources.
 
na sidhani kama ni issue ya wazenji ....umedadavua vizuri
Hoja yako ni ipi? Hivi Znz si sehemu y a Tz?
Try to think outside the box, u may see the arguements of Judge Warioba.
Are u trying to tell us to have similar understanding for each n every thing?
You may wish to know that our differences are our important resources.
 
Ukimsikiliza Mzee Warioba,anayazungumza masuala kiufundi zaidi na kwa lugha nyepesi yenye kueleweka. Kwa nini watawala wanampuuza mawazo yake? Dah!
 
Mgombea huru anatakiwa kuwa huru kweli kweli, sio kutapatapa tu mara uko huku, mara kule!

Mkuu acha kua ---- sababu tu jamaa zako wamepitisha ule ujinga,kama mtu anakubalika na wananchi wengi na chama chake kina misimamo isiyo eleweka kwa nn asipewe nafasi ya kusimama mwenyewe?,ukitaka kujua ccm ni janga angalia hotuba ya baba wa taifa ya mwaka 95 full halafu utajua ujinga wenu
 
Huyu mzee Warioba ni mchawi/adui wa Muungano wetu! Apingwe kwa gharama yoyote!

kama ni mchawi jibu alicho wasilisha siyo kuja na muhemko wako wa kipuuuzi angalia tupo kwenye kipindi kigumu sna tz namashaka makubwa sna na ufahamu wako
 
ukimsikiliza mzee warioba,anayazungumza masuala kiufundi zaidi na kwa lugha nyepesi yenye kueleweka. Kwa nini watawala wanampuuza mawazo yake? Dah!
hekima huumba na kuumbua
 
Back
Top Bottom