KATIBA: CCT nao watoa tamko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KATIBA: CCT nao watoa tamko!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Invisible, Apr 6, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  6 Aprili 2011

  Mhe. Celine Kombani
  Waziri wa Katiba na Sheria

  Mheshimiwa Waziri
  ,

  Yah: TAHADHARI KUTOKA CCT JUU YA MUSWADA WA MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA KWA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2011

  Jumuiya ya Kikrito Tanzania (CCT) inaipongeza hatua ya kijasiri ya Serikali katika kusikiliza maoni ya wananchi hadi kufikia hatua hii ya kutoa muswada kuhusiana na hitaji lao la Katiba mpya. Hii ni hatua kubwa ambayo tumefurahishwa nayo sana.

  Tarehe 11 Machi 2011, Serikali ilitangaza kuwepo kwa muswada uliokusudiwa kujadiliwa Bungeni mwezi Aprili mwaka huu, juu ya mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Muswada Namba 1 wa mwaka 2011.

  Mategemeo ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania na wananchi kwa ujuma ni kwamba muswada huu utaruhusu uwazi na nafasi ya kushiriki kwa wanajamii wote ili kuweza kuweka bayana ni aina gani na mfumo upi wa Katiba wanayoitaka.

  Lakini Muswada huo unaonyesha kutokuzingatia matarajio halisi ya wananchi, kwani lengo wanalolitaka wananchi ni kutungwa kwa Katiba mpya inayoendana na zama hizi na zijazo na sio mabadiliko tu ya Katiba ya nchi. Maudhui ya muswada yanafifisha na kudhoofisha ari na matarajio yao, maana mabadiliko yamekuwa yakifanyika kila mara lakini licha ya mabadiliko hayo mengi bado lengo la kupata Katiba mpya halijakidhiwa.

  Hivyo basi CCT inatoa tahadhari kama ifuatavyo:-

  Katiba ni mkataba ambao wananchi wanajiwekea kuonyesha jinsi wanavyotaka nchi itawaliwe na kuweka misingi ya kufuatwa na ukomo wa mamlaka kati ya watawala na watawaliwa. Hivyo wananchi ndio wenye usemi wa mwisho juu ya Katiba ya Nchi. Watawala wote akiwemo Rais ni waajiriwa wa wananchi ikiwa ni pamoja na Bunge; kwani wao huomba na kuingizwa kwenye utumishi kwa ridhaa ya wananchi kwa kutumia taratibu za kidemokrasia. Kwa hiyo hawana budi kuwarudia wananchi ili wapate maoni yao juu ya mstakabali endelevu wa nchi yao. Hivyo, ni sharti wananchi wenyewe wawezeshwe kutoa maoni yao moja kwa moja au kwa njia ya wawakilishi wa makundi yote ya kijamii.

  Ipo hatari ya kukasimu mamlaka haya kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Tawala kuteua Tume ya kusimamia mchakato huu ikiwemo Sekretarieti yake.

  Utaratibu huu unamfanya Rais awe wa mwanzo na mwisho (Alpha na Omega) na kuondoa ushiriki wazi wa wananchi katika kusimamia na kuamua mstakabali wa nchi yao. Ni vyema mamlaka haya yakakasimiwa kwa wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge na vyama vya siasa.

  Mambo haya yanahitaji kupata muda wa kujifunza kutoka ndani na nje ya nchi (katika mtazamo hasi na chanya) ili kuwa na uelewa dhahiri utakaolenga katika kupata Katiba inayokidhi mahitaji ya wananchi. Tusijikute kwamba tunaharakia kufanya mabadiliko ya Katiba ili kukidhi hitaji la Uchaguzi ujao wa 2015 tu.

  Ni vyema Tume ihusishe ushiriki wa wadau wote wa makundi yote ya kijamii, kisha iwasilishe taarifa yake kwa wawakilishi wa wananchi watakaokuwa wameiteua; kwa kupata ridhaa na maamuzi.

  Tunakuomba utumie weledi na hekima yako kuhakikisha kwamba rai yetu inapewa nafasi na umuhimu katika jambo hili ili kuleta umoja, usawa, amani na utangamano pamoja na maendeleo ya nchi yetu yatakayotokana na Katiba iliyoandaliwa na wananchi wenyewe.  Askofu Mkuu Dkt. Valentino Mokiwa
  MAKAMU WA KWANZA WA MWENYEKITI - CCT


  Nakala: - Waziri Mkuu - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  - Mwanasheria Mkuu wa Serikali
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  great ... leadership needs 3D view
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280


  Askofu Mkuu Dkt. Valentino Mokiwa
  MAKAMU WA KWANZA WA MWENYEKITI - CCT
   
 4. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tunasubiri pia na tamko la BAKWATA. Katiba ya watanzania wote hivyo baada ya Askofu Ruzoka jana (TEC) na Dr Mokiwa leo (CCT) naamini BAKWATA nao watakuja na Positive opinions katika hilo.

  Ni tahadhari kabla ya hatari na panapofuka moshi ujue pana moto! Waziri wa sheria fanyia kazi hayo pamoja na yale ya UDASA na wadau wengine, Rais hana cha kupoteza katika katiba ijayo awe fair tu katika mchakato wake kama alivyoanza kuonyesha. I'm just thinking

  :yield:
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  This is what mr Gsana wants to hear. He is also anxiously waiting for other institutions whether religious or political. Mr Gsana has promised to be against all who are against the Constitutional Movement. All the best well wishers. Gsana.
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Naona watu wanamsubiria Kupeng'e avuruge kwanza wamvae...
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  CCM inadhani wanaolinda AMANI ni jeshi la polisi kumbe sivyo..wenye kufanya hii kazi kwa usahihi wake ni viongozi wa kiraia na dini,mfano mzuri ni kule Tarime

  Sasa ukiona wameamka na kutoa tahadhari zao ujue kazi imebaki kwa watawala,vinginevyo tusije kuwarudia (viongozi wa dini) huku barabara zishafungwa.

  MWENYE KUSIKIA NA ASIKIE na MWENYE SHIDA KAMWE HANGOJEI PAPAMBAZUKE
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  haa haaaa .... kupeng'e na muhadhiri watakua wanaandaa tamko lao ... ngoja tusubiri
   
 9. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Yule jamaa ana kipaji cha kuharibu mada....

  Hiyo barua imetulia sana, imeeleza mapungufu makubwa katiba muswada na jinsi rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM Taifa alipojiweka kwenye nafasi ngumu ku hakikisha KATIBA MPYA inapatikana.

  Kutokana na jinsi mambo yalivyo ni wazi kabisa Rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM Taifa atalazimika kutosa kundi moja either wananchi au CCM. Kufurahisha wote haitawezekana.
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,691
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Yeah,whatever...they should show us the polls from credible institutions as to why they think that majority of Tanzanians want a new constitution.
   
 11. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Safi sana, acha waendelee kupambana ni haki yao ya msingi kuwasemea watu wanaowaongoza kiimani,ili hata kama likitokea la kutokea mjue kuwa walisema ila wahusika hawakusikia.

  Ni muhimu Mkuu wa nchi akaelezwa ukweli juu ya kile kiinimacho anachotaka kukifanya kwa wananchi wake kuhusu katiba,
   
 12. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Barua imejaa busara sana.

  Hongereni CCT
   
 13. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Hofu yangu tu ni wale wanazi wa mambo ya udini wataanza propoganda zao kisa chombo cha kidini kimetoa maoni yao.

  Kimsingi naunga mkono hoja zao kwani wameeleza mambo ya msingi kabisa, yaani rais anaendeleza ubabe kwenye katiba mpya.

  Kwa maoni yangu huu muswada sio wa katiba mpya bali muendelezo wa katiba ya zamani tena kuikaza zaidi.
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Kama mtakumbuka, sisi wenyewe hapa JF ndo tuliwapigia kelele viongozi wa dini kwa kukaa kwao kimya mambo yakienda mrama, so far wanachofanya wanasaidia kuzipaza sauti zetu tulio wengi na sijaona UDINI wowote katika nyaraka mbili hizi, ya jana na hii ya leo.

  Natambua kuwa kuna maslahi ya watu yanaguswa sasa, ni wazi watataka kuvuruga hoja hizi, hapa itakuwa ngumu, vema waje kivingine, hoja ijibiwe na hoja.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  A very timely letter. And to the point.
   
 16. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Katika matamko haya sijaona sehemu inayotaja udini, lakini nadhani BAKWATA wakija na lakwao sitashangaa kuona wameweka udini!
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  yaani BAKWATA kwanza hawajui hata kuna nini kinaendelea wao wako bize na mambo ya Gadafi anaonewa
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu .... kuna watu wapo makini bana....!
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu Invisible, hiyo barua nilioipenda sana na kuonyesha kuwakilisha vilivyo maoni yangu na mimi katika mamilioni wengine nchini; ina maana haikuandikwa kwenye letterhead kabisa???

  I mean, I am just being a litle more good nurturedly curious apart from my ever deep respect for the authenticity and authoritativeness of all previous documents presented in here.
   
 20. L

  LAT JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  it could be a 1:1 scale of the content of the letter
   
Loading...