GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,745
- 109,190
Nina Rafiki yangu mmoja ni Dereva wa Dala Dala Juzi nadhani ‘ alikengeuka ‘ na akapita njia isiyoruhusiwa ya JW na bahati nzuri Gari lake lilikuwa halina Abiria na alipokamatwa nao wala hawakumpiga ila kulikuwa na Uwanja wa Mpira pembeni wakamuuliza kama Gari yake ina Mafuta ya kutosha na aliposema haina wakamuongezea na ikajaa ‘ Full Tank ‘ na akaambiwa auzunguke huo Uwanja kwa Spidi ya Magari ya Mashindano ya ‘ Langa Langa ‘ hadi yale Mafuta yaishe na akatii ‘ Amri ‘ na baadae wakamuachia ila sasa hivi kila akikaa tu anasema anasikia ‘ Kizunguzungu ‘ na harufu ya ‘ Petroli ‘ inatawala Puani na Ubongoni mwake.
Ni jana tu Rafiki yangu mmoja Mmachinga akiwa maeneo ya Ukonga nadhani nae labda ‘ alikengeuka ‘ akawa anapita eneo la FFU huku akiwa anapiga Kelele za Kutangaza Nguo zake alizobeba kumbe alikuwa ameingia sehemu isiyotakiwa Kelele na walipomkamata wala hawakumpiga ila alipewa Kazi ya Kukata Michongoma kwa Kutumia Mkasi wa Kunyolea Ndevu na ule wa Mafundi Cherehani zoezi ambalo hadi leo hajalikamilisha labda atalikamilisha Wiki ijayo.
Je kati ya MP na FFU nani ni ‘ Mafundi ‘ wa Kutoa Adhabu?
Nawasilisha.