Kati ya PROF. KABUDI na PROF. SHIVJI nani Zaidi?

Kati ya PROF. KABUDI na PROF. SHIVJI nani Zaidi?

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Wakuu, kwa wafuatiliaji wa mijadala mbalimbali kwa mustakabali wa Taifa letu katika masuala ya kisiasa, kikatiba na kisheria nani zaidi kati ya wasomi hawa wawili ; Prof. Palamagamba Kabudi na Prof. Issa Shivji?
 
Nia ni kuleta mpasuko.....kila mmoja ni zaidi kwa nafasi yake.
Ingawa leo kabudi kanifurahisha mpaka machoz yalinitoka na kuwakumbuka watu kama Prof Jwani Mwaikusa na Dk Mvungi.
 
Wakuu, kwa wafuatiliaji wa mijadala mbalimbali kwa mustakabali wa Taifa letu katika masuala ya kisiasa na kisheria nani zaidi kati ya wasomi hawa wawili ; Prof. Palamagamba Kabudi na Prof. Issa Shivji?

Hakuna msaliti kama Shivji kile kipindi chake cha katika ITV nilikifuatilia sana na alikuw muumini wa 3 lakini alivyopigwa biti sikuhizi anahubiri2 na tena kwa kuwakashifu wajumbe wa tume ya katiba.
 
...huwezi kulinganisha mchumia tumbo aliyenunuliwa na ccm mpaka anakimbiwa kuitwa kwenye midahalo ya kizalendo na wazalendo...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Zaidi katika NINI? wakati gani? nani zaidi kwa NANI?....... hebu fafanua ndugu!

Yaani hata paragraph fupi hiyo hujaelewa je ingekuwa ni page nzima! Rudia tena kusoma utaelewa naulizia nani zaidi katika masuala gani.
 
Sijuhi nani kichwa zaidi ...ila usomi ni pamoja na kuwa independent...huyo paramagamba sijuhi nani labda kama kabadilika...ni kibaraka wa serikali...
 
Shivji Tanzania watu wachache mno wanamuelewa...shivji hapingi serikali tatu...yeye anacho pinga ni warioba kusema wengi wanataka serikali tatu while ni 5 percent only ya waliohojiwa na tume...
 
Wakuu, kwa wafuatiliaji
wa mijadala mbalimbali kwa mustakabali wa Taifa letu katika masuala ya
kisiasa na kisheria nani zaidi kati ya wasomi hawa wawili ; Prof.
Palamagamba Kabudi na Prof. Issa Shivji?

Shivj niwakumpambanisha na kina Nape, Lukuvi au Wasira. hapa umemuonea
 
Kwangu bado Shivji zaidi though kila mmoja ana areas of Strength n Weakness ...
 
Hakuna msaliti kama Shivji kile kipindi chake cha katika ITV nilikifuatilia sana na alikuw muumini wa 3 lakini alivyopigwa biti sikuhizi anahubiri2 na tena kwa kuwakashifu wajumbe wa tume ya katiba.

Shivji ni mzanzibari, aliitaka serikali tatu wakati ule, kwa sasa Shivji amefanikiwa kupata serikali ya Zanzibar yenye madaraka kamili, japo kuna upungufu kidogo. Baada ya katiba ya Zanzibar Shivji aliona kazi imeisha. Serikali mbili inamanufaa zaidi kwa Zanzibar, hasa kiuchumi. Mfano mdogo tu malipo ya wabunge wa Muungano kutoka Zanzibar, wanapeleka shs ngapi Zanzibar? Malipo na ruzuku ya watumishi wa smz nk Ndio maana sasa hataki serikali 3
 
Naam Shivji ni mchumia tumbo ambaye aliamua kuweka pembeni umakini wake kuhusu katiba ambao miaka nenda miaka rudi amekuwa akiuzungumzia lakini baada ya MACCM kumnunua akabadili msimamo wake.

...huwezi kulinganisha mchumia tumbo aliyenunuliwa na ccm mpaka anakimbiwa kuitwa kwenye midahalo ya kizalendo na wazalendo...
 
Kwa maoni yangu, comparison ya kushindanisha watu wawili wanaofanana kwa kuuliza nani zaidi, is not fair kwa members of academia!.

Swali la msingi lingepaswa kuwa "Compare and contrast Prof. Kabudi na Prof. Shivji.Kwa vile wawili ni waalimu wangu, naomba ku reserve comments zangu.
Pasco.

Both ni waalimu wa sheria UDSM
Both ni mabingwa wa sheria waliobobea kwenye constitution law.
Both ni vichwa mbaya, GPA ya 1st Class ya Kabudi (4.8) ni historical kwa UDSM haijawahi kufikiwa na mwanafunzi mwingine yoyote mpaka kesho!. Thinking Capacity and analysis ya Shivji ni kitu ingine.
Wote ni watu wa misimamo isiyoyumba ila mmoja ni extremist, mmoja ni moderate!.
Wote wawili ni watu wa msaada sana kwa wanafunzi wao, mimi nikiwa shuhuda, Kabudi ndio alikuwa supervisor wangu, Prof. Shivji alikuwa mentor wangu.

Mmoja anatanguliza mbele maslahi ya taifa, ikibidi kuipinda sheria kwa ajili ya maslahi ya taifa, anaweza ukaipinda kidogo ili kulinusuru taifa!, mwingine anashikilia misimamo ya kisheria!, maadamu sheria inasema hivi, hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe, ikibidi nchi kuvunjika na ivunjike! lakini sheria ifuatwe!.
Wote ni wanasheria wanasiasa!, kuna uwezekano wa mmoja kuwa ni mshabiki, au mfuasi wa chama cha siasa, mwingine hana chama!.
 
Shivji Tanzania watu wachache mno wanamuelewa...shivji hapingi serikali tatu...yeye anacho pinga ni warioba kusema wengi wanataka serikali tatu while ni 5 percent only ya waliohojiwa na tume...

yule mwanasheria kutoka Zanzibar alitoa ufafanuzi juu ya takwimu hivyo uzito wa hoja hiyo sidhani kama unamashiko na "nafikiria" Jaji aliitumia tu kama daraja au kibwagizo kwenye wimbo wake
 
hivi shivji mnamjua kwel? Mambo ya taaluma yasichanganywe na siasa.
 
Shivji Tanzania watu wachache mno wanamuelewa...shivji hapingi serikali tatu...yeye anacho pinga ni warioba kusema wengi wanataka serikali tatu while ni 5 percent only ya waliohojiwa na tume...

Yeye alitaka wahojiwe asilimia ngapi?
 
Shivji Tanzania watu wachache mno wanamuelewa...shivji hapingi serikali tatu...yeye anacho pinga ni warioba kusema wengi wanataka serikali tatu while ni 5 percent only ya waliohojiwa na tume...

Kwa hiyo yeye anataka kutuambia nini ? na ili iweje ? toa ufafanuzi mrs mwerevu.
 
Back
Top Bottom