Kati ya CCM na Wapinzani Nani muuaji

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
362
254
CCM, mnajua hatari mnayohubiri kwenye kuua binadamu?

SIASA ya nchi yetu imechukua sura mpya sana katika awamu hii ya tano. Tumerejea hatua nyingi nyuma katika kuheshimu misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, utawala bora na Uhuru binafsi. Hatuna tofauti na tawala za KIBABE za nyakati za kitambo huko Marekani ya kusini. Tupo sehemu mbaya.

Viongozi wastaafu wapo kimya. Nao wameingiwa na hofu? Hawajui ni hatari sana wao wakiendelea kukaa kimya wakati wana CCM wa sasa wakihubiri kuua, kuteka, kutesa hadharani? Nchi yetu ikiharibika na machafuko hata wao na Ndugu zao wataumia. Wasikae kimya. Wakatae hadharani uovu.

Kuna gharama kubwa sana kuongozwa na chama kilichokataa tamaa, kimepagawa, ni kimefika Mwisho kuzalisha fikra mpya (timamu) na sasa wanafikiria kuwaua watu wengine wanaotofautiana nao fikra, mtazamo na itikadi. CCM wamepagawa. Hawafanyi siasa tena.

CCM sasa sio chama cha siasa. CCM imefilisika hoja na uwezo wa kutengeneza viongozi timamu. Wamebaki wafuasi na walamba nyayo. CCM imejinasibisha na DOLA. wapinzani wa CCM wanapambana na DOLA na mfumo na sio CCM (dead horse). CCM ni kitu mfu sasa. Haipo CCM kuna dola.

Kufikiria kutoa uhai wa mtu mwingine kwa namna yoyote ile ni kiwango/hatua ya Mwisho kabisa kuelekea kufilisika hata uwezo wa ubongo kufanya kazi. Maana yake ubongo umeshindwa kufikiri njia mbadala, umeamua kutoa suluhisho la "kuua". Ubungo uliopooza (paralyze) ndio haufanyi kazi tena.

Mbunge wa CCM, (ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais) Abdallah Bulembo anasimama bungeni,kwa sauti na madoido na kumtuhumu Zitto Kabwe (kwa usaliti?) na anasema Zitto Kabwe hapaswi kurejea nchini, auwawe huko nje ya nchi. Spika wa bunge yupo kimya na wabunge wa CCM wanashangilia.

Kinachotia kinyaa zaidi ni mama anayejiita 'mtumishi wa Mungu' Gertrude Rwakatare (ambaye pia no mbunge wa kuteuliwa na Rais) anapiga makofi pembeni ya Bulembo na kushangilia kauli za kuua binadamu, na baadae atahubiri haki, mshikamano na utulivu kwenye jamii, na ataeleweka, watanzania ni wepesi kuwamudu.

Serikali ya awamu ya tano inajinasibu kufanya maendeleo makubwa ya kiuchumi yenye kugusa watu, kwanini wapambe wa serikali hii, viongozi wake wanakataa kukosolewa? Kwanini wasijitokeze kwa wananchi na kusema maendeleo hayo, wananchi wawashangilie?

Serikali ambayo imejenga SGR, inajenga SGHEP, ikaleta ndege zaidi ya 11, imeleta umeme kila kijiji, imepeleka Maji kila familia nchi nzima, imejenga barabara, imetengeneza Meli, viongozi wake wanaogopa kukosolewa? Hadi hadharani wanasema wanaikosoa serikali yao wanapaswa kuuwawa?

Serikali ambayo imewalipa 'cash' wakulima wa Korosho, ikawalipa 'cash' wakulima wa Pamba, wakulima wa Mbaazi, dengu wanafurahia bei ya bidhaa zao, soko la nje limefunguka, kwenda India kupeleka mazao ni rahisi, inaogpa kukosolewa? Au wanayotupa simulizi ni ya uongo?

Kama huwezi kutetea Hoja zako, huwezi kuitetea serikali yako na umeshindwa kuitetea CCM hadharani (huna hoja) unataka na ambao wanaweza kuikosoa serikali wanyamaze kimya? Wakifanya majukumu yao ya kuikosoa serikali mnakasirika? Mnatamani kuwaua? Mmekuwa watu wa hovyo!

Mwenyekiti wa UVCCM ni mjumbe wa NEC, mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu Taifa. Huyu anawajibu wa kumshauri mwenyekiti wa CCM Taifa kuhusu masuala ya sera za vijana, ajira, uchumi, usalama, Amani na utulivu. Kwa akili hizi, atafanya hayo?

Kheri James anaagiza vijana wake wawashambulie, kuwajeruhina kuwaua viongozi wa upinzani ambao wanatoa maoni yao yenye kupingana na serikali ya CCM. Haya ni Mawazo ya mwenyekiti wa vijana wa CCM Taifa hadharani. Sirini Je? Mnajadiliana kuhusu kuwaua wapinzani wenu kisiasa?

Huyo ambaye mnapanga kumuua, mnadhani hana familia, ukoo, marafiki? Kwamba mnaweza kumuua mtu kwa sababu haipendi CCM na ninyi mkaendelea kuwa salama tu? Hamjui kuna nguvu kubwa katika kulipiza kisasi? Mtamwaga damu zenu nyingi kuliko hao wapinzani. Kaeni kwa kutulia.

Polisi wametulia kimya. Wanasikia yote yanayoendelea. IGP yupo kimya. Hapo anasubiri mwanasiasa wa upinzani asimame, aseme kama huyu Bulembo (wamkamate na kumpa mashtaka ya ugaidi, uchochezi au uhujumu uchumi). Tunaishi kwenye nchi iliyoharibika sana. Imeharibiwa na CCM kwa kiwango KIKUBWA.

Godbless Lema, mwaka 2017 alikamatwa na kuwekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, ARUSHA kwa zaidi ya miezi 4 kwa kosa la kutoa simulizi bungeni, yenye kuhusu ndoto ambayo ilimuonesha JPM atafariki. Kosa! Ndoto ikapewa mashtaka ya uchochezi. Maajabu! Awamu hii ya Awafu mwenye nguvu.

Mwaka 2017, ikulu DSM, wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya Madini (Tanzanite na Almasi), Rais Magufuli alitoa tuhuma za Usaliti kwa "mtu/watu" na akasisitiza wasaliti wanachofanywa kwa mbinu za kiaskari. Alisema "wamedukua" maongezi ya huyo mtu na Mwanyika na wamegundua usaliti wake.

Usaliti wake ni upi mtu huyo ambaye hakutajwa? (wengine tunajua nani alikuwa akizungumziwa) usaliti wake ni kuomba nyaraka (documents) za mikataba ya BARRICK na Serikali. Huu ndio usaliti? Kwamba mtanzania hapaswi kufahamu yenye kuhusu nchi yake kwenye mikataba? Ni kosa la jinai? Dhambi?

Ok! Siku hiyo, saa chache baadae, Tundu Lissu akitoka bungeni kwenda nyumbani kwake, saa saba mchana, Jua kali, alishambuliwa kwa risasi nyingi na risasi 16 ziliingia katika mwili wake. Waliomshambulia Tundu Lissu kwa risasi hadi sasa hawajawahi kujulikana. Inashangaza.

Sasa tunaona viongozi wa CCM wakisema hadharani bila hofu kuhusu kuwaua wapinzani, wakosoaji wa serikali, wanaharakati wa haki za binadamu. Wakiwapa majina mabaya kwanza, wasaliti. Ili jamii ikubali kwamba wapinzani hao kwa sababu ya wao kukataa kusimama na CCM ni usaliti.

CCM imefilisika. Hawajui kukubali katika kutokubaliana pia ni demokrasia? Sio lazima kila kitu kama taifa wananchi mkubaliane. Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuna watanzania zaidi ya milioni 6 hawakumchagua Magufuli aliyekuwa mgombea wa CCM. Hawa watanzania bado wapo. Mnawaua wote?
 
Kidogo kidogo mambo yanaanza kuwekwa wazi.

Na bila shaka wabunge wa CCM inawezekana ndio walioomba hata Mh Tundu Lissu auliwe katika vikao vyao vya siri (Kama wameweza kusema katika kikao cha bunge na nchi zima imeshuhudia, na rekodi zipo kwenye Hansard za Bunge).
 
CCM hawajui kukubali katika kutokubaliana pia ni demokrasia? Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuna watanzania zaidi ya milioni 6 hawakumchagua Magufuli, Hawa watanzania bado wapo. Mnawaua wote?
Nimeusikiliza huu mjadala, kiukweli baadhi ya wabunge wametoa kauli kali na hatarishi, ikiwemo kauli ya kifo kwa Mhe. Zitto Kabwe.

Naendelea kusisitiza kuhusu kauli huumba, kauli kama hii ilitolewa kumhusu Lissu na mara ikatekelezwa, sasa ni kumhusu Zitto, bahati nzuri Zitto ni mtu wa Kigoma, mwisho wa reli, na kule kwao, kaaga!, likimtokea la kutokea, kwa mujibu wa Zitto mwenyewe, hawa waliochangia adhuriwe, kule majumbani kwao, hakuta salia hata panya alive!.

P
 
Mungu akiamua kukuumbua hakuna Wa kuzuia. Vikao na mapendekezo ya mauaji kwa wasiowapenda hufanyika kwenye vikao vyao vya siri. Ila kwa vile Mungu kataka dunia ijue , mwenzao kajistukia karopoka Zitto auawe kwenye kikao cha bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM, mnajua hatari mnayohubiri kwenye kuua binadamu?

SIASA ya nchi yetu imechukua sura mpya sana katika awamu hii ya tano. Tumerejea hatua nyingi nyuma katika kuheshimu misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, utawala bora na Uhuru binafsi. Hatuna tofauti na tawala za KIBABE za nyakati za kitambo huko Marekani ya kusini. Tupo sehemu mbaya.

Viongozi wastaafu wapo kimya. Nao wameingiwa na hofu? Hawajui ni hatari sana wao wakiendelea kukaa kimya wakati wana CCM wa sasa wakihubiri kuua, kuteka, kutesa hadharani? Nchi yetu ikiharibika na machafuko hata wao na Ndugu zao wataumia. Wasikae kimya. Wakatae hadharani uovu.

Kuna gharama kubwa sana kuongozwa na chama kilichokataa tamaa, kimepagawa, ni kimefika Mwisho kuzalisha fikra mpya (timamu) na sasa wanafikiria kuwaua watu wengine wanaotofautiana nao fikra, mtazamo na itikadi. CCM wamepagawa. Hawafanyi siasa tena.

CCM sasa sio chama cha siasa. CCM imefilisika hoja na uwezo wa kutengeneza viongozi timamu. Wamebaki wafuasi na walamba nyayo. CCM imejinasibisha na DOLA. wapinzani wa CCM wanapambana na DOLA na mfumo na sio CCM (dead horse). CCM ni kitu mfu sasa. Haipo CCM kuna dola.

Kufikiria kutoa uhai wa mtu mwingine kwa namna yoyote ile ni kiwango/hatua ya Mwisho kabisa kuelekea kufilisika hata uwezo wa ubongo kufanya kazi. Maana yake ubongo umeshindwa kufikiri njia mbadala, umeamua kutoa suluhisho la "kuua". Ubungo uliopooza (paralyze) ndio haufanyi kazi tena.

Mbunge wa CCM, (ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais) Abdallah Bulembo anasimama bungeni,kwa sauti na madoido na kumtuhumu Zitto Kabwe (kwa usaliti?) na anasema Zitto Kabwe hapaswi kurejea nchini, auwawe huko nje ya nchi. Spika wa bunge yupo kimya na wabunge wa CCM wanashangilia.

Kinachotia kinyaa zaidi ni mama anayejiita 'mtumishi wa Mungu' Gertrude Rwakatare (ambaye pia no mbunge wa kuteuliwa na Rais) anapiga makofi pembeni ya Bulembo na kushangilia kauli za kuua binadamu, na baadae atahubiri haki, mshikamano na utulivu kwenye jamii, na ataeleweka, watanzania ni wepesi kuwamudu.

Serikali ya awamu ya tano inajinasibu kufanya maendeleo makubwa ya kiuchumi yenye kugusa watu, kwanini wapambe wa serikali hii, viongozi wake wanakataa kukosolewa? Kwanini wasijitokeze kwa wananchi na kusema maendeleo hayo, wananchi wawashangilie?

Serikali ambayo imejenga SGR, inajenga SGHEP, ikaleta ndege zaidi ya 11, imeleta umeme kila kijiji, imepeleka Maji kila familia nchi nzima, imejenga barabara, imetengeneza Meli, viongozi wake wanaogopa kukosolewa? Hadi hadharani wanasema wanaikosoa serikali yao wanapaswa kuuwawa?

Serikali ambayo imewalipa 'cash' wakulima wa Korosho, ikawalipa 'cash' wakulima wa Pamba, wakulima wa Mbaazi, dengu wanafurahia bei ya bidhaa zao, soko la nje limefunguka, kwenda India kupeleka mazao ni rahisi, inaogpa kukosolewa? Au wanayotupa simulizi ni ya uongo?

Kama huwezi kutetea Hoja zako, huwezi kuitetea serikali yako na umeshindwa kuitetea CCM hadharani (huna hoja) unataka na ambao wanaweza kuikosoa serikali wanyamaze kimya? Wakifanya majukumu yao ya kuikosoa serikali mnakasirika? Mnatamani kuwaua? Mmekuwa watu wa hovyo!

Mwenyekiti wa UVCCM ni mjumbe wa NEC, mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, mjumbe wa mkutano mkuu Taifa. Huyu anawajibu wa kumshauri mwenyekiti wa CCM Taifa kuhusu masuala ya sera za vijana, ajira, uchumi, usalama, Amani na utulivu. Kwa akili hizi, atafanya hayo?

Kheri James anaagiza vijana wake wawashambulie, kuwajeruhina kuwaua viongozi wa upinzani ambao wanatoa maoni yao yenye kupingana na serikali ya CCM. Haya ni Mawazo ya mwenyekiti wa vijana wa CCM Taifa hadharani. Sirini Je? Mnajadiliana kuhusu kuwaua wapinzani wenu kisiasa?

Huyo ambaye mnapanga kumuua, mnadhani hana familia, ukoo, marafiki? Kwamba mnaweza kumuua mtu kwa sababu haipendi CCM na ninyi mkaendelea kuwa salama tu? Hamjui kuna nguvu kubwa katika kulipiza kisasi? Mtamwaga damu zenu nyingi kuliko hao wapinzani. Kaeni kwa kutulia.

Polisi wametulia kimya. Wanasikia yote yanayoendelea. IGP yupo kimya. Hapo anasubiri mwanasiasa wa upinzani asimame, aseme kama huyu Bulembo (wamkamate na kumpa mashtaka ya ugaidi, uchochezi au uhujumu uchumi). Tunaishi kwenye nchi iliyoharibika sana. Imeharibiwa na CCM kwa kiwango KIKUBWA.

Godbless Lema, mwaka 2017 alikamatwa na kuwekwa mahabusu ya gereza la Kisongo, ARUSHA kwa zaidi ya miezi 4 kwa kosa la kutoa simulizi bungeni, yenye kuhusu ndoto ambayo ilimuonesha JPM atafariki. Kosa! Ndoto ikapewa mashtaka ya uchochezi. Maajabu! Awamu hii ya Awafu mwenye nguvu.

Mwaka 2017, ikulu DSM, wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya Madini (Tanzanite na Almasi), Rais Magufuli alitoa tuhuma za Usaliti kwa "mtu/watu" na akasisitiza wasaliti wanachofanywa kwa mbinu za kiaskari. Alisema "wamedukua" maongezi ya huyo mtu na Mwanyika na wamegundua usaliti wake.

Usaliti wake ni upi mtu huyo ambaye hakutajwa? (wengine tunajua nani alikuwa akizungumziwa) usaliti wake ni kuomba nyaraka (documents) za mikataba ya BARRICK na Serikali. Huu ndio usaliti? Kwamba mtanzania hapaswi kufahamu yenye kuhusu nchi yake kwenye mikataba? Ni kosa la jinai? Dhambi?

Ok! Siku hiyo, saa chache baadae, Tundu Lissu akitoka bungeni kwenda nyumbani kwake, saa saba mchana, Jua kali, alishambuliwa kwa risasi nyingi na risasi 16 ziliingia katika mwili wake. Waliomshambulia Tundu Lissu kwa risasi hadi sasa hawajawahi kujulikana. Inashangaza.

Sasa tunaona viongozi wa CCM wakisema hadharani bila hofu kuhusu kuwaua wapinzani, wakosoaji wa serikali, wanaharakati wa haki za binadamu. Wakiwapa majina mabaya kwanza, wasaliti. Ili jamii ikubali kwamba wapinzani hao kwa sababu ya wao kukataa kusimama na CCM ni usaliti.

CCM imefilisika. Hawajui kukubali katika kutokubaliana pia ni demokrasia? Sio lazima kila kitu kama taifa wananchi mkubaliane. Ndio maana katika uchaguzi mkuu wa 2015 kuna watanzania zaidi ya milioni 6 hawakumchagua Magufuli aliyekuwa mgombea wa CCM. Hawa watanzania bado wapo. Mnawaua wote?
Kweli damu ya mtu ni mbaya wameanza kuropoka hadharani .Swali fikirishi nini chanzo cha mauaji ya kimyakimya ambayo nadhani yamezalisha watu wasiojulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kidogo kidogo mambo yanaanza kuwekwa wazi.

Na bila shaka wabunge wa CCM inawezekana ndio walioomba hata Mh Tundu Lissu auliwe katika vikao vyao vya siri (Kama wameweza kusema katika kikao cha bunge na nchi zima imeshuhudia, na rekodi zipo kwenye Hansard za Bunge).
Kweli damu ya mtu ni mbaya wameanza kuropoka hadharani .Swali fikirishi nini chanzo cha mauaji ya kimyakimya ambayo nadhani yamezalisha watu wasiojulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom