KATAVI: Mwanafunzi abakwa na kuuawa akienda shule

KATAVI: Mwanafunzi abakwa na kuuawa akienda shule

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,303
MWANAFUNZI wa kike mwenye umri wa miaka 14 ameuawa kikatili baada ya kubakwa kwa zamu na mwendesha pikipiki maarufu ‘bodaboda’ kisha akachomwa kisu ubavuni na sehemu zake za siri kunyofolewa wakati akienda shule akiwa amefuatana na mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka 11.

Mwanafunzi huyo alikuwa akisoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Vikonge katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, sambamba na mdogo wake wa kiume ambaye alikuwa akisoma darasa la nne kwenye shule hiyo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema kuwa tukio hilo la kikatili lilitokea juzi Jumanne saa moja asubuhi umbali wa kilometa moja na nusu kutoka shuleni hapo.

“Asubuhi hiyo ya tukio, marehemu akiwa ameongozana na mdogo wake wa kiume huku wakielekea shuleni walikutana na mwendesha pikipiki maarufu ‘bodaboda’ ambaye alikuwa hawamfahamu na kuwaambia kwamba atawapa lifti. Marehemu alipopanda mwendesha bodaboda alimzuia mdogo wake wa kiume asipande ambapo aliondoka akiendesha pikipiki hiyo kwa kasi isiyo ya kawaida huku kaka wa marehemu akiikimbilia bila mafaniko.

Aliongeza kuwa mdogo wa marehemu alipoamua kutembea kwa miguu kuelekea shuleni baada ya kuchoka kuifukuza pikipiki hiyo, ghafla aliiona pikipiki ile iliyombeba dada yake ikiwa imeegeshwa karibu na kichaka kando ya barabara inayoelekea shuleni kwao na akaipita.

Kamanda Nyanda alisema kaka huyo wa marehemu alienda shuleni hapo na kuhudhuria darasani kama kawaida hadi ilipofika saa nane na nusu alianza safari kuelekea nyumba pasipo kumtafuta dada yake.

“Kaka wa marehemu bila shaka kutokana na umri wake kuwa bado mdogo baada ya kufika shuleni hakushughulika kumtafuta dada yake, aliingia darasani na kuendelea na masomo kama kawaida na baada ya muda wa masomo yaani saa nane na nusu alianza safari ya kurejea nyumbani bila kumtafuta dada yake,” alieleza Kamanda Nyanda.

Aliongeza kuwa baada ya mtoto huyo kufika nyumbani wazazi wake walishtuka kumuona akiwa pekee yake ndipo walipomuhoji alikomuacha dada yake ndipo alipowasimulia kila kitu.

“Wazazi wa marehemu baada ya kupata maelezo hayo walipatwa na mashaka hivyo walimtaka mdogo wa marehemu awapeleke kwenye eneo alipoina pikipiki iliyombeba dada yake ikiwa imepakiwa karibu na kichaka. Mtoto huyo aliwaongoza wazazi wake ambao walikuwa wamefutana na majirani zao hadi kwenye eneo la tukio, walishtuka kuona kuwa kuna nyasi zilikuwa zimelala ndipo walipoona mwili wa marehemu ukiwa umechomwa kisu ubavuni huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.


Chanzo: Habari Leo
 
Damu ya mtu hua haiendi bure,R.I.P mtoto

Mtenda kosa atakamatwa tu
 
Haya maisha yamevaa Combat, yaani kila MTU anatembea na Kadi ya kifo.
Ila huwezijua anayekupeleka kwenye tukio.

Trust Nobody.

Mungu akuweke mahala salama binti.
 
Kule kuna watu wanaitwa wahutu...wale warundi wakioletwa na Nyerere...wanaroho mbaya sana..mtaniamin akiamatwa utasikia ni mhutu..Sina maana ya kuwatenga lakin hawa watu wana tabia tofaut kabisa na watz walio weng
 
Hapo adhabu ya kunyongwa haijaondolewa!! Je, ikiondolewa?
 
Rip Mwanafunzi wa kike,samahani madakatari sehemu ya kike inanyofolewaje?
 
Hivi hadi hili nalo la ukatili alofanya dereva toyo linastahili watu wa haki za binadamu waje wamtetee huyo dereva '?
napendekeza wananchi wenye hasira kali waachiwe wamnyooshe kidogo.
 
mbona huu mkasa kama ni revenge ? kama ni nia ya kutimiza tamaa za mwili wake mbona baada ya kufanya hivo alimuuwa huyu mtoto asiye na hatia ? hakika kuna jambo nyuma ya pazia, upelelezi ukikamilika itafahamika.
r.i.p binti
 
inauma sana pole wazazi kwa kuondokewa na mpendwa wenu,manyang'au kama hayo yafaa yafungwe maisha yanapo patikana
 
Mambo haya yanasikitisha sana. Huyo mtenda kosa atakamatwa tu muda si mrefu.Jamii yetu ina mchanganyiko wa watu, wengine ni hatari. Ulinzi kwa watoto uwe jukumu la kila mmoja wetu. RIP Mtoto!

R.I.P Mtoto
====
Kuna utaratibu umeanzishwa na shule moja ya kutwa ya serikali ya sekondari huko Chamwino Dodoma, utaratibu huo unanipa mashaka juu ya walimu pamoja na baadhi ya wazazi wanakusudia nini! Ni shule ya mchanganyiko.

Hiko hivi:
Wanafunzi wanaenda shule asubuhi...wanarudi nyumbani mchana kama saa nane hivi..kwenye saa tisa 'alasiri' wanarudi tena shule na kurudi muda wa saa kama kumi na mbili na robo jioni. Kisanga kinaanza pale ambapo, wanafunzi hawa wanalazimishwa pia kurudi shuleni mida ya saa moja na robo usiku na kurudi saa nne usiku nyumbani tena bila uangalizi wa aina yoyote kutoka kwa wazazi ama walimu. Lengo la kwenda kule usiku ni kwa ajili ya masomo.

Karibu na shule ile kuna 'kilinge' cha walevi na kadhalika. Mkaguzi/ama msaidizi wa mkurugezi wa shule za sekondari wa wilaya hii sina hakika ana taarifa hizi.
 
Watu lama hao kwenye jela za ulaya wakiingia tu wanatolewa utumbo na wenzao. Inasikitisha sana.
 
Mtoto wa darasa la nne akaipita piki piki iliyomteka dada yake ikiwa imepaki pembeni akaenda shule akapiga kimya hakumwambia yeyote na akarudi nyumbani bila ya kumwambia yoyote yule shule!!! ..kwa kawaida tukio la aina hii hata mtoto wa Nursery School ws miaka 4 angesema tu shule kama si kwa walimu basi kwa wenzake vipi yeye wa miaka karibia 10 ashindwe??.. amini usiamini huyu mtoto ni mjinga sana!!
 
Back
Top Bottom