Shida sio ugali, shida ugali unakula na nini..
Kweli ugali unakosa madini mengi tu.
Lakini ugali hauliwi pekee yake, ugali unaenda na mboga gani!!
Juzi kati nimeenda kwa mama ntilie ugali ule ni mtamu, mboga standard mpaka nikamuuliza kwa buku jero hupati hasara kweli!?
Ugali laini,
Dagaa wametiwa nazi
Maharage nazi
Mboga za majani
Na nyama
Mboga zoote quality, si mpenzi saana wa ugali, ila ile nilikula ugali mchana kwa siku 5 mfululizo