Kasusura sasa kutandikwa bakora.....!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Justine Kasusura aliyeshitakiwa kwa kosa la wizi wa fedha dola za kimarekani milioni mbili ( 2ml.) akiwa mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group ameshindwa katika rufaa yake aliyokata katika mahakama kuu ya Tanzania. Kasusura aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya wizi akiwa mlinzi wa kampuni hiyo alikata rufaa katika mahakama kuu kupinga adhabu hiyo, lakini rufaa yake hiyo iligongwa mwamba ambapo sasa adhabu hiyo ya miaka 30 jela itaambatana na viboko 6...
 
Hiyo ni adhabu ya mwizi. Kwa kuwa aliiba na kuzubaa na pesa yote humu humu nchini akiwahonga mandata akiwemo mkubwa wa mandata wa wakati ule. Wacha apate haki yake. Atajuta kwa nini aliiba kitita hicho na kukichezea bila mpangilio.
 
Huyu jamaa alizimaliza pesa zake zote kwa kuwahonga mapolisi.....aliisahau mahakama.....sasa mtu mzima kama yeye kupigwa stiki 6??? na hiyo itakua daily au??? kama daily nampa Pole...
..Hapana mkuu daily wataua...nadhani siku atakayokuwa akimaliza kifungo chake iwe ni salamu kwa wadau wengine na mai wife wake pia...
 
Sitetei wizi wa aina yeyote ile lakini kati ya wezi wajinga duniani na Kasusura yumo, mtu umeiba dola mil.2 badala ya kuchukua single ticket unakwenda kujificha Mbeya halafu baada ya siku mbili unaanza kutanua baa za vichochoroni na vimada huo kama si ukichaa ni nini, acha ale hizo mvua 30 ni saizi yake.
 
Hiyo ni adhabu ya mwizi. Kwa kuwa aliiba na kuzubaa na pesa yote humu humu nchini akiwahonga mandata akiwemo mkubwa wa mandata wa wakati ule. Wacha apate haki yake. Atajuta kwa nini aliiba kitita hicho na kukichezea bila mpangilio.

Mchukia Fisadi:

Hii paragraph sijaielewa vizuri - haindani na jina lako!
 
Sitetei wizi wa aina yeyote ile lakini kati ya wezi wajinga duniani na Kasusura yumo, mtu umeiba dola mil.2 badala ya kuchukua single ticket unakwenda kujificha Mbeya halafu baada ya siku mbili unaanza kutanua baa za vichochoroni na vimada huo kama si ukichaa ni nini, acha ale hizo mvua 30 ni saizi yake.
..Unajua huwa najiuliza kama jamaa alikuwa amesepa na mzigo wote $ 2m. na hata kama aliamua kutanua bila ya kuwa na akiba ya busara kuwa endapo litabumburuka atajipoza vipi then hapo hata mimi namshangaa!! Tena dola zikiwa mpya 2m ni unene wa kipande cha sabuni tu!!:mmph:
 
Justine Kasusura aliyeshitakiwa kwa kosa la wizi wa fedha dola za kimarekani milioni mbili ( 2ml.) akiwa mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group ameshindwa katika rufaa yake aliyokata katika mahakama kuu ya Tanzania. Kasusura aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya wizi akiwa mlinzi wa kampuni hiyo alikata rufaa katika mahakama kuu kupinga adhabu hiyo, lakini rufaa yake hiyo iligongwa mwamba ambapo sasa adhabu hiyo ya miaka 30 jela itaambatana na viboko 6...
kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa, Mithali 1 : 7
kuusikiliza mwili na nafsi yako daima, mwisho wako ni wa aibu na mbaya sana,
laiti kama angeamua kuishi kwa kuitii torati ya Mungu kwa Musa na watu wote angejua kuwa kuiba ni dhambi, maana ilikuonya Kasusura, ''USIIBE'' maana mwizi hufa dhambini,
 
Back
Top Bottom