Kasuku na Changudoa

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,109
Reaction score
53,630
Mwanadada mmoja mrembo
alienda mjini kufanya
shopping,akapita mahali flani
akaona muuzaji mmoja anauza
kasuku elfu 25....akaamua kuulizia:
Dem:"Mambo."
Muuzaji:"Poa sista...nikusaidie
nini?"
Dem:"Nilikuwa naulizia
tuh...inaonekana huyu kasuku
wako ni special maana unamuuza
kwa bei ghali!"
Muuzaji:"Huyu kasuku huongea
ndio maana namuuza kwa hio
bei."
Yule dem akaamua kumjaribu pale
pale...akamuuliza kasuku,
"Mmmh..hebu niambie leo
nakaaje?...mi najiona
nimetoklezea!"
Kasuku akajibu:"Unaonekana
kama Changudoa..."
Dem akakasirika na
kusema,"Siwezi kumnunua
kasuku huyu maana ni mshenzi
ana tabia mbaya na za
kipumbavu!!"
Muuzaji akamwambia yule dada
asubiri kiasi...akamchukua kasuku
na kuenda nae nyuma ya
duka,akamzamisha ndani ya
beseni lililojaa maji kwa dakika
kadhaa...kisha akamtoa na
kumwambia,"Pumbavu ukirudia
kuongea ushenzi mbele ya wateja
kama yule dada nitakuzamisha
tena na safari hio hadi
ufe...mshenzi wewee!!"
Aliporudi akamkuta yule
mwanadada bado yupo
akamwambia,"Dada samahani
kwa tatizo hilo...naomba umuulize
tena kasuku swali lolote."
Dem akauliza:"Nikirudi nyumbani
kwangu na mwanamume mmoja
utafikiriaje?"
Kasuku:"Kwa kweli nitafikiria
huyo ni MUME WAKO."
Dem:"Nikirudi na wanaume
wawili?"
Kasuku:"Hapo itakuwa MUME
WAKO na KAKA YAKO."
Dem:"Je nikirudi nyumbani na
wanaume watatu?"
Kasuku:"Hao watakuwa MUME
WAKO,KAKA YAKE MUME WAKO na
KAKA YAKO."
Dem:"Vipi je nikirudi nyumbani na
wanaume wanne?"
Kasuku:"Aarggh!..Kudadeki!!! Lete
hilo beseni la
maji....nilishakwambia huyu dada
ni Changudoaaaaaa..!!!"
 
Hivi hapa CC imeshakuwa hivi wajameni?

Hawa member wa jukwaa hili leteni maoni yenu hapa;

Arushaone
Filipo
Madame B
Preta
Asprin
Bishanga

Na member wengine wa jukwaa hili hebu naombeni maoni yenu maana Mi binafsi naona kama thread hii ya huyu member Bulldog; Ningefurahia pale jukwaa la Jokes!

Mabadiliko ndani ya jukwaa hili muhimu wadau!

Toeni maoni yenu!
 
Last edited by a moderator:
Madame B; Yani kwa kweli hili jukwaa lenu Mi natamani sana ifanyiwe marekebisho kwani hata maneno mengi hayapaswi hata kusikika katika glob kama hii yetu ila member toka Glob hii ya FACEBOOK wamehamia jukwaa hili na hawanaga hekima hata kidogo! Mi inaniboa sana!


Umeona eeeee LiverpoolFC:glasses-nerdy:
 
Last edited by a moderator:
Heheheheh! Mkuu leo naona jukwaa limekaa kikasuku kasuku.

Karibu jukwaa la dini tumwimbie Bwana.

CC: Zion Daughter
 
Last edited by a moderator:
Heheheheh! Mkuu leo naona jukwaa limekaa kikasuku kasuku.

Karibu jukwaa la dini tumwimbie Bwana.

CC: Zion Daughter
Mchumba & mtumishi mwenzangu mie nishatangulia huko na nimeanza mapambio...Neno linasema ulimi(ukasuku) ni kiungo kidogo lakn madhara yake ni makubwa sana Yak 3..Ukimaliza kuwahamasisha nakusubiri uombee sadaka.
 
Mi nitahamia kwenye jukwaa la mapenzi & urafiki huko kuna changamoto sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…