Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 588
- 1,698
Habari wakuu,
Subira yavuta heri, hatimae Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe amepeleka pendekezo la jina la waziri mkuu kwa awamu ya Tano anayoiongoza. Rais amempendekeza Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu ambae anahitajika kuthibitishwa na bunge kwa kura za siri kabla ya kutangazwa rasmi.
Majaliwa anapendekezwa kuwa waziri mkuu baada ya kumaliza kutumikia Unaibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa serikali ya awamu nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Majaliwa ambae kazaliwa Desemba 22, 1960 pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani hadi mwaka 2009. Pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.
Kadhalika, Majaliwa amekuwa Mbunge wa Ruangwa tangu 2010, alisomea Ualimu Chuo cha Ualimu Mtwara na Mafunzo ya JKT alifanyia kambi ya Makutopora mkoani Dodoma. Pia alisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia aliwahi kuwa Katibu wa Chama cha Walimu Singida. Majaliwa alisoma elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mnacho mwaka 1970 mpaka 1976 na baadae akajiunga na shule ya sekondari Kigosensera mwaka 1977.
Baada ya wabunge kupiga kura, alithibitishwa na bunge baada kupata kura nyingi zaidi za ndio hivyo kuwa waziri mkuu wa awamu ya tano.
Wabunge 394
Wabunge waliosajiliwa 369
Wabunge wanaotakiwa kufika akidi 184
Wabunge waliopo na kupiga kura 351
Kura zilizoharibika 2 (0.06%)
Kura za Hapana 91 (25.9%)
Kura za Ndio 258 (73.5%)
Personal Details
Salutation: Hon.
Surname: Majaliwa
First Name: Kassim
Middle Name: Majaliwa
Date of Birth: 22 Dec. 1960
Marital Status: Married
Sex: Male
Mobile Number: (+255) 785 205 910
Email: majaliwa.kasimu(at)yahoo.com
Address: P.O.Box 51, Ruangwa
Education Background:
Primary Education: 1970 -1976 Mnacho Primary School
CSEE: 1977-1980 Kigonsera Secondary School
- 1991 - 1993 Mtwara Teachers College
Bachelors Degree 1994 - 1998 University of Dar es Salaam
PGDP 1999 - 1999 Stockholm University
Other Trainings:
-
Experience
2010 - 2015 Member of Parliament
2006 - 2010 District Commissioner
2001 - 2006 Reginal Secretary (PS - CWJ)
2001 - 2001 District Commissioner (PS - CWJ)
1988 - 2000 PS - Moec (Instructor)
1984 - 1986 TD - Lindi Council (Teacher)
Hobbies: Soccer
Attachments
Last edited by a moderator: