Uchaguzi 2020 Kasoro za kiuchumi katika ilani za CHADEMA na ACT-Wazalendo

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
461
500
Ilani za CHADEMA na ACT Wazalendo kwa upande wa uchumi hazifafanui namna pato la ndani ya nchi (GDP) litakavyokuwa linaongezeka mwaka hadi mwaka kutoka figures za sasa. Pia hazitaji watakuwa wanakusanya mapato (kodi na mapato yasiyo kodi) kiasi gani ili kuwezesha wananchi tuweze kupima hayo mambo wanayohaidi kama yanatekelezeka kwa sababu pesa ndio msingi wa utekelezaji wa ahadi za kiuchumi zinazotolewa. CHADEMA na Lissu wao kila kitu wanadai kinawezekana na watafanya kuanzia afya, elimu, makazi, ajira, mishahara mikubwa ikiambatana na nyongeza lakini hakuna mahali wanapoonyesha namna watakapopata fedha hizo. Kwao hakuna financial constraints.

Zitto yeye na ACT Wazalendo walau wao amekuwa wajanja na ilani yao inaonyesha wapi watapata fedha za kutekeleza jambo moja moja kutoka kila chanzo chake. Lakini wamekwepa aspect muhimu niloizozileza hapo juu.

Wanapaswa kwanza kueleza matarajio (projection) ya ukuaji wa uchumi kila mwaka kwa miaka yote mitano, GDP ya kila mwaka kwa figures ili iweze kujulikana kwa uhakika chini ya sera zao pato la nchi litakuwaje. Pato la nchi ndio msingi wa mapato ambayo serikali itakuwa inakusanya kwa njia ya kodi na yasiyo ya kodi. Pia walipaswa waeleze makusanyo yao ya kodi yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka na pia mapato ya ndani ya serikali kwa ujumla yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka. Wataje pia kwa figures (projections) watakuwa wanakusanya shilingi ngapi kila mwaka

CHADEMA na ACT Wazalendo wanapaswa watueleze (projections) watatumia shilingi ngapi kati ya makusanyo hayo ya kila mwaka kulipa mishahara hiyo mikubwa wanayoahidi na pia kulipa madeni ambayo watapaswa kuendelea kulipa. Baada ya hapo tutaweza kujua kiasi cha mapato kinachobakia kwa ajili ya kutekeleza hayo mambo makubwa wanayoahidi na watukukotolee matumizi yote kuanzia afya, elimu bure, mikopo ya elimu ya juu, maji, nyumba, viwanda, masoko nk ambavyo hasa CHADEMA wamekuwa wakidai watafanya. Kwa dunia ya sasa data zote za kiuchumi zunatabirika tena kwa figures hivyo hakuna sababu ya wao kueleza maneno matupu bila kuweka figures.

Pia ACT Wazalendo katika ilani yao niliyoisoma Mwanahalisi online (extract) kwani sijabahatika kupata kitabu kizima, wanadai kuwa mwaka wa tano makusanyo ya kodi yatakuwa asilimia 25 ya GDP. Ukiangalia makusanyo ya sasa ya kodi kwa uwiano wa GDP ni asilimia 12.9. Ni vigumu kuwa wao ACT watakuwa na muujiza wa kuongeza uwiano huo mara mbili hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka mitano tu. Ukiangalia nchi kama Kenya yenye uchumi mzuri, wao makusanyo yao kwa mwaka 2018 yalikuwa asilimia 15.09 kwa uwiano wa GDP. Wastani wa uwiano wa makusanyo ya kodi kwa GDP kwa nchi za Africa kwa mwaka 2019 ilikuwa asilimia 17.2. Hivyo utaona wanachoeleza ACT Wazalendo sio rahisi kufikiwa kwa miaka mitano tu.

Kwa mujibu wa ilani ya ACT Wazalendo waliyoiwasilisha, kodi zitakuwa kubwa sana kuliko kodi za sasa hivyo wananchi wajiendae kulipa zaidi ikiwa watashinda. Chini ya CHADEMA kwa haya matamko yao, uchumi utaporomoka sana na inflation itakuwa juu.

Ila kuna jambo moja tu katika ilani ya ACT Wazalendo ambalo linatekelezeka na ni jambo zuri nalo ni namna watakavyotatua tatizo la maji. Wamesema kuwa kwa kila lita ya mafuta (fuel) watatoza kodi maalum kama inavyofanywa kwa ujenzi wa barabara na uenezaji umeme vijijini (REA). Jambo hilo litapelekea tatizo la maji kutatuliwa.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,397
2,000
Mkuu ndio maana nyuzi zako hazina wachangiaji. Inaonekana mweupe sana kwenye masuala ya uchumi. Na muhimu unapaswa kufanya comparative reading kabla haujaja hapa kukosoa unaposema haiwezekani kisa tu average ya Afrika ni 17.2 ina maana hata REA tunaosikia wamecover vijiji 90% kupata umeme isingewezekana kisa tu average ya sub sahara ipo chini ya hapo? Au ulikua unamaanisha nini?

Alafu hakuna inflation kisa spending itakua juu, kazi ya BOT itakua nini?. Monetary policy zinabadilika kulingana na hali ya uchumi wakiona pesa inakua nyingi kwenye mzunguko basi tools zinatumika ili kucontract uchumi.

Pia ukifanya uchambuzi acha biasness, unaposema kodi zitaongezwa mbona huongelei impact yake kwenye makusanyo ya serikali ili watu wapime faida na hasara.

Alafu kitu kingine kuonyesha ulivyo mtupu kiuchumi eti unaeleza kuwa kivipi GDP itapanda ilihali hapo umekiri ACT wana solution ya kumaliza tatizo la maji kupitia tozo ndogo. Je umepiga hesabu kwamba kila mtanzania akipata access ya maji na hasa huko vijijini wakawekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji kuepuka risk ya mazao kukosa mvua n.k je umepiga hesabu ya faida yake? Je umepiga hesabu ya muda waaotumia akina Mama kusaka maji wangeutumia kufanya ujasiriamali wangeingiza shingapi? Je umejiuliza cost za kununua maji hta mjini kma hyo pesa ingetumika kwingine isingekuza vipato vya wananchi? Embu chukua tu kipengele cha maji alafi kipigie hesabu ya spillover effect kwa opportunity cost ya gharama za maji kuwekezwa kwenye mambo mengine alafu ndio urudi hapa kukosoa ripoti.

Uchambuzi wako una makosa lukuki embu rudi kajipange upya.
 
Naomba jibu hoja kwa hoja nimewataka muweke projections zenu kama GDP growth, nk lakini nawe unataka mimi nifanye ambacho ulipaswa kufanya wewe. Hebu jibu kipengele kwa kipengele kwa sababu hili ni jukwaa la hoja sio matusi.
Kuhusu kukiri suala la maji ndio ukomavu wa kukubali ukweli sio ushabiki.
 
Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,446
2,000
Ilani za CHADEMA na ACT Wazalendo kwa upande wa uchumi hazifafanui namna pato la ndani ya nchi (GDP) litakavyokuwa linaongezeka mwaka hadi mwaka kutoka figures za sasa. Pia hazitaji watakuwa wanakusanya mapato (kodi na mapato yasiyo kodi) kiasi gani ili kuwezesha wananchi tuweze kupima hayo mambo wanayohaidi kama yanatekelezeka kwa sababu pesa ndio msingi wa utekelezaji wa ahadi za kiuchumi zinazotolewa. CHADEMA na Lissu wao kila kitu wanadai kinawezekana na watafanya kuanzia afya, elimu, makazi, ajira, mishahara mikubwa ikiambatana na nyongeza lakini hakuna mahali wanapoonyesha namna watakapopata fedha hizo. Kwao hakuna financial constraints.

Zitto yeye na ACT Wazalendo walau wao amekuwa wajanja na ilani yao inaonyesha wapi watapata fedha za kutekeleza jambo moja moja kutoka kila chanzo chake. Lakini wamekwepa aspect muhimu niloizozileza hapo juu.

Wanapaswa kwanza kueleza matarajio (projection) ya ukuaji wa uchumi kila mwaka kwa miaka yote mitano, GDP ya kila mwaka kwa figures ili iweze kujulikana kwa uhakika chini ya sera zao pato la nchi litakuwaje. Pato la nchi ndio msingi wa mapato ambayo serikali itakuwa inakusanya kwa njia ya kodi na yasiyo ya kodi. Pia walipaswa waeleze makusanyo yao ya kodi yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka na pia mapato ya ndani ya serikali kwa ujumla yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka. Wataje pia kwa figures (projections) watakuwa wanakusanya shilingi ngapi kila mwaka

CHADEMA na ACT Wazalendo wanapaswa watueleze (projections) watatumia shilingi ngapi kati ya makusanyo hayo ya kila mwaka kulipa mishahara hiyo mikubwa wanayoahidi na pia kulipa madeni ambayo watapaswa kuendelea kulipa. Baada ya hapo tutaweza kujua kiasi cha mapato kinachobakia kwa ajili ya kutekeleza hayo mambo makubwa wanayoahidi na watukukotolee matumizi yote kuanzia afya, elimu bure, mikopo ya elimu ya juu, maji, nyumba, viwanda, masoko nk ambavyo hasa CHADEMA wamekuwa wakidai watafanya. Kwa dunia ya sasa data zote za kiuchumi zunatabirika tena kwa figures hivyo hakuna sababu ya wao kueleza maneno matupu bila kuweka figures.

Pia ACT Wazalendo katika ilani yao niliyoisoma Mwanahalisi online (extract) kwani sijabahatika kupata kitabu kizima, wanadai kuwa mwaka wa tano makusanyo ya kodi yatakuwa asilimia 25 ya GDP. Ukiangalia makusanyo ya sasa ya kodi kwa uwiano wa GDP ni asilimia 12.9. Ni vigumu kuwa wao ACT watakuwa na muujiza wa kuongeza uwiano huo mara mbili hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka mitano tu. Ukiangalia nchi kama Kenya yenye uchumi mzuri, wao makusanyo yao kwa mwaka 2018 yalikuwa asilimia 15.09 kwa uwiano wa GDP. Wastani wa uwiano wa makusanyo ya kodi kwa GDP kwa nchi za Africa kwa mwaka 2019 ilikuwa asilimia 17.2. Hivyo utaona wanachoeleza ACT Wazalendo sio rahisi kufikiwa kwa miaka mitano tu.

Kwa mujibu wa ilani ya ACT Wazalendo waliyoiwasilisha, kodi zitakuwa kubwa sana kuliko kodi za sasa hivyo wananchi wajiendae kulipa zaidi ikiwa watashinda. Chini ya CHADEMA kwa haya matamko yao, uchumi utaporomoka sana na inflation itakuwa juu.

Ila kuna jambo moja tu katika ilani ya ACT Wazalendo ambalo linatekelezeka na ni jambo zuri nalo ni namna watakavyotatua tatizo la maji. Wamesema kuwa kwa kila lita ya mafuta (fuel) watatoza kodi maalum kama inavyofanywa kwa ujenzi wa barabara na uenezaji umeme vijijini (REA). Jambo hilo litapelekea tatizo la maji kutatuliwa.
Niliwahi kuuliza hapa na nikasema kama T Lisu hana nafasi na kwa kuwa chadema wanajinasibu kuwa wana wasomi basi waje watwambie vyanzo vya mapato vitakuwa vipi ili hayo yatimie.

Je walishasema serikari imekopa sana kwa hiyo deni la taifa limekuwa kubwa, sasa tulitaka kujua je wao hawatakopa ili kuliongeza hilo deni?
Hiyo nyongeza ya mishahara na kuilipa fidia na mapungufu ya upandishwaji mishahara pesa itatoka wapi kwa kuwa walisema watashusha kodi?

Yaani huyu jamaa anawaingiza watu chaka vibaya saana.
 
  • Thanks
Reactions: RMC

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,397
2,000
Naomba jibu hoja kwa hoja nimewataka muweke projections zenu kama GDP growth, nk lakini nawe unataka mimi nifanye ambacho ulipaswa kufanya wewe. Hebu jibu kipengele kwa kipengele kwa sababu hili ni jukwaa la hoja sio matusi.
Kuhusu kukiri suala la maji ndio ukomavu wa kukubali ukweli sio ushabiki.
Mkuu kubali umechemka, GDP estimations huwezi fanya kwa ilani wakati bado hujajua macro economic effects za sera ya ilani zako.
Labda nikupe elimu, CHADEMA ikishinda uchaguzi ile ilani inakabidhiwa kwa serikali ambapo Kupitia tume ya mipango ndio wanatengeneza mpango wa taifa wa miaka 5. Ambapo ilani inageuzwa kuwa workable objectives za kiuchumi.

Mpango unaingizwa bungeni na ukipitishwa ndio bajeti zote za serikali zitatengenezwa kupitia huo mpango wa taifa. Kwahiyo Ilani ni blueprint tu au executive summary/Proposal ya unachotaka kufanya ila methodology zote na milestones zitachambuliwa kwa upana na hizo document nlizokutajia hapo juu.

Mfano soma ilani ya CCM uk wa 11-19 wameelezea hali ya uchumi 2020-25 ila sijaona projection ya GDP popote. Wameahidi ajira million 8 ila sijaona projection ya GDP au GNI kwa miaka hii 5 sababu ilani ni summary tu ila ikishapelekwa kufanyiwa kazi kila kipengele kinaundiwa work plan yake.

Sasa basis ya kusema CHADEMA iweke GDP projections unazitoa wapi? Kuna template ya pamoja?
Niliwahi kuuliza hapa na nikasema kama T Lisu hana nafasi na kwa kuwa chadema wanajinasibu kuwa wana wasomi basi waje watwambie vyanzo vya mapato vitakuwa vipi ili hayo yatimie.

Je walishasema serikari imekopa sana kwa hiyo deni la taifa limekuwa kubwa, sasa tulitaka kujua je wao hawatakopa ili kuliongeza hilo deni?
Hiyo nyongeza ya mishahara na kuilipa fidia na mapungufu ya upandishwaji mishahara pesa itatoka wapi kwa kuwa walisema watashusha kodi?

Yaani huyu jamaa anawaingiza watu chaka vibaya saana.
 
RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
461
500
Mkuu kubali umechemka, GDP estimations huwezi fanya kwa ilani wakati bado hujajua macro economic effects za sera ya ilani zako.
Labda nikupe elimu, CHADEMA ikishinda uchaguzi ile ilani inakabidhiwa kwa serikali ambapo Kupitia tume ya mipango ndio wanatengeneza mpango wa taifa wa miaka 5. Ambapo ilani inageuzwa kuwa workable objectives za kiuchumi.

Mpango unaingizwa bungeni na ukipitishwa ndio bajeti zote za serikali zitatengenezwa kupitia huo mpango wa taifa. Kwahiyo Ilani ni blueprint tu au executive summary/Proposal ya unachotaka kufanya ila methodology zote na milestones zitachambuliwa kwa upana na hizo document nlizokutajia hapo juu.

Mfano soma ilani ya CCM uk wa 11-19 wameelezea hali ya uchumi 2020-25 ila sijaona projection ya GDP popote. Wameahidi ajira million 8 ila sijaona projection ya GDP au GNI kwa miaka hii 5 sababu ilani ni summary tu ila ikishapelekwa kufanyiwa kazi kila kipengele kinaundiwa work plan yake.

Sasa basis ya kusema CHADEMA iweke GDP projections unazitoa wapi? Kuna template ya pamoja?
Unafahamu kuwa nchi hii mwaka 2011 tulitengeneza mpango wa miaka kumi na tano na ndani yake ikatengenezwa mipango mitatu ya miaka mitano mitano? Mipango wa tatu wa miaka 5 unaanza 2021 . hivyo hadi mwaka 2025 kuna mpango mezani tofauti na unavyosema labda uniambie mkiingia nyinyi mnaubomoa na kutengeneza wenu upya.

Kama hadi mpaka muingie madarakani ndio mfanye projection mbona ACT Wazalendo wamesema watakusanya uwiano wa kodi kwa GDP asilimia 25 mwaka wa tano9? Kama unaweza kufanya projection ya mwaka mmoja wa mwisho kwa nini miaka minne ya mwanzo usiifanye.

Kwanza nikufahamushe kuwa Tume ya Mipango iliishavunjwa na majukumu yake yanafanywa na Wizara ya Fedha.

Unawezaje kuzungumza kwa uhakika kuwa utalipa mishahara mikubwa, na mambo mengine makubwa yanayihitaji fedha nyingi halafu unajitetea hapa kuwa huwezi kufanya projection za mapato?
Mbona tumeambiwa na serikali ya CCM kuwa miwaka 2020/21 uchumi utakua kwa asilimia 5.5 je sio projection hiyo? Na kutokana na hiyo huwezi kujua GDP kwa kipindi hicho itakua kiasi gani? Unaweza kabisa ukafanya hata horizon ya miaka kumi ya ukuaji wa uchumi na mambo yasiwe tofauti sana.

Mnawapa watanzania matumaini hewa halafu unatafuta technicality za kukwepa kuthibitisha hicho mnachoahidi.

Makusanyo ya sasa ya mapato na matumizi hasa ya mishahara na kulipa madeni yalipaswa yawe basis ya mnachoahidi maana unafahamu baada ya kulipa vitu hivyo kinachobaki ni kiasi gani.
 
Kwa hiyo serikari ikishindwa ku compere na ilani basi ilani hiyo inakuwa ni mfu na haitekelezeki sio?
Kwa mana hiyo ilani ya chadema inaweza isitekerezeke kama wanavyo tuaminisha kwenye majukwaa.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,397
2,000
Kwa hiyo serikari ikishindwa ku compere na ilani basi ilani hiyo inakuwa ni mfu na haitekelezeki sio?
Kwa mana hiyo ilani ya chadema inaweza isitekerezeke kama wanavyo tuaminisha kwenye majukwaa.
Ilani inatekelezeka ikishaingizwa kwenye mpango wa taifa na baadae bajeti ya serikali kuu/halmshauri n.k sasa huko ndio inapangiwa jinsi gani itatekelezeka.

Hiki mnachohoji hata Ilani ya CCM haionyeshi kivp ajira million 8 zitakuja au GDP itapaa kiasi gani ila wakishaandaa mpango wa taifa wa 2021-25 ndio watavunja kipengele kwa kipengele inabaki kazi ya serikali kutembea ndani ya huo mpango.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,397
2,000
Unafahamu kuwa nchi hii mwaka 2011 tulitengeneza mpango wa miaka kumi na tano na ndani yake ikatengenezwa mipango mitatu ya miaka mitano mitano? Mipango wa tatu wa miaka 5 unaanza 2021 . hivyo hadi mwaka 2025 kuna mpango mezani tofauti na unavyosema labda uniambie mkiingia nyinyi mnaubomoa na kutengeneza wenu upya.

Kama hadi mpaka muingie madarakani ndio mfanye projection mbona ACT Wazalendo wamesema watakusanya uwiano wa kodi kwa GDP asilimia 25 mwaka wa tano9? Kama unaweza kufanya projection ya mwaka mmoja wa mwisho kwa nini miaka minne ya mwanzo usiifanye.

Kwanza nikufahamushe kuwa Tume ya Mipango iliishavunjwa na majukumu yake yanafanywa na Wizara ya Fedha.

Unawezaje kuzungumza kwa uhakika kuwa utalipa mishahara mikubwa, na mambo mengine makubwa yanayihitaji fedha nyingi halafu unajitetea hapa kuwa huwezi kufanya projection za mapato?
Mbona tumeambiwa na serikali ya CCM kuwa miwaka 2020/21 uchumi utakua kwa asilimia 5.5 je sio projection hiyo? Na kutokana na hiyo huwezi kujua GDP kwa kipindi hicho itakua kiasi gani? Unaweza kabisa ukafanya hata horizon ya miaka kumi ya ukuaji wa uchumi na mambo yasiwe tofauti sana.

Mnawapa watanzania matumaini hewa halafu unatafuta technicality za kukwepa kuthibitisha hicho mnachoahidi.

Makusanyo ya sasa ya mapato na matumizi hasa ya mishahara na kulipa madeni yalipaswa yawe basis ya mnachoahidi maana unafahamu baada ya kulipa vitu hivyo kinachobaki ni kiasi gani.
Mkuu mpango wa miaka 5 lazima upitishwe bungeni so kupitia hii ilani ya CCM ya sasa kuna mambo yanaongezwa kwa mpango. N dio maana hta uliona Mchumi Mkuu wa wizara ya fedha alikutana na private sector ili kukusanya maoni yawe incorporated kwenye mpango wa 2021-2026!! Kwahiyo hata serikali ikibadilika bado kuna room ya kuconsolidate ilani mpya kwenye huo mpango wa miaka mitano.

2. ACT wamefanya projection which is fine lakini sio kwamba ni lazima kwenye ilani. Huwa unaweka summary na mpango tu ila yote hayo yanakua extended kwenye mpango wa taifa,sera za uchumi, mabadiliko ya sheria na kanuni, bajeti za serikali n.k so kuna room ya kuandaa projections other than ilani otherwise itakua na page elfu 10!! Na kma ni udhaifu basi pia upo ilani zote mpka CCM maana sijaona projection yeyote ndani ya ilani yao.
3. Which takes us to the third point..... Serikali ya CCM imeproject?? Sasa serikali ya CCM ndio CCM? Kazi za wizara zisigeuzwe ndio kazi za CCM!! wao kazi ya chama ni kuisimamia serikali yake tu sio serikali kusimamia CCM!!. Hata serikali ya ACT au CHADEMA itaproject tu maana wana tools mfano BOT na wizara za fedha kuweza kutoa ripoti ya muelekeo wa uchumi. Sasa usigeuze kazi za wataalamu eti ndio CCM hivyo upinzani waje na yao!! It's funny! Unless ungeenda kusoma bajeti kivuli maana mdee aliweka projections mule za mapato na matumizi!! Najua hujasoma sababu ya uvivu ndio maana unakuja kutoa biased analysis humu.
 
Toka mwanzo unakwepa hoja za msingi ndio maana unaishia kukashifu. Gist ya argument yangu sio details ya mipango yenu ya kutekekeza yale mliyoahidi kwenye ilani. Nillikuwa ĺ projections za pato la taifa ( GDP), uwiano wa kodi na mapato yasiyo kodi kwa GDP , mapato kwa figures, kwa sababu kwa yale mlioahidi kuyafanya hata wa rough estimation ni matrilioni ya shilingi yatahitajika . Ukilinganisha trend ys mapato na matumizi na mSasa kwa trend ya ukuaji wa uchumi ambayo ni predictable ndio maana miaka 20 iliyopita tuliweza kypanga kuwa
Mkuu mpango wa miaka 5 lazima upitishwe bungeni so kupitia hii ilani ya CCM ya sasa kuna mambo yanaongezwa kwa mpango. N dio maana hta uliona Mchumi Mkuu wa wizara ya fedha alikutana na private sector ili kukusanya maoni yawe incorporated kwenye mpango wa 2021-2026!! Kwahiyo hata serikali ikibadilika bado kuna room ya kuconsolidate ilani mpya kwenye huo mpango wa miaka mitano.

2. ACT wamefanya projection which is fine lakini sio kwamba ni lazima kwenye ilani. Huwa unaweka summary na mpango tu ila yote hayo yanakua extended kwenye mpango wa taifa,sera za uchumi, mabadiliko ya sheria na kanuni, bajeti za serikali n.k so kuna room ya kuandaa projections other than ilani otherwise itakua na page elfu 10!! Na kma ni udhaifu basi pia upo ilani zote mpka CCM maana sijaona projection yeyote ndani ya ilani yao.
3. Which takes us to the third point..... Serikali ya CCM imeproject?? Sasa serikali ya CCM ndio CCM? Kazi za wizara zisigeuzwe ndio kazi za CCM!! wao kazi ya chama ni kuisimamia serikali yake tu sio serikali kusimamia CCM!!. Hata serikali ya ACT au CHADEMA itaproject tu maana wana tools mfano BOT na wizara za fedha kuweza kutoa ripoti ya muelekeo wa uchumi. Sasa usigeuze kazi za wataalamu eti ndio CCM hivyo upinzani waje na yao!! It's funny! Unless ungeenda kusoma bajeti kivuli maana mdee aliweka projections mule za mapato na matumizi!! Najua hujasoma sababu ya uvivu ndio maana unakuja kutoa biased analysis humu.
Acha kupotosha hoja yangu, rudi usome vizuri thread yangu ya mwanzo kuhusu kasoro za kiuchumi.

Mimi nilichotaka sio CHADEMA au ACT kuelezea mipango ya kibajeti, najua hiyo inafanywa kila mwaka na kupelekwa bungeni kupitishwa na serikali iliyopo mdarakani. Nilichohoji ni projections za macroeconomic indicators muhimu ambazo sasa ndio zitatoa mwanga kama hicho mnachowaahidi watanzania kinatekelezeka.

Projections za Macro economic indicators kwa miaka mitano nilizowataka mziseme ninarudia kuzitaja: ukuaji wa GDP kila mwaka , GDP ya kila mwaka, uwiano wa kodi kwa GDP, uwiano wa mapato ya ndani (kodi na yasiyo kodi) kwa GDP kwa kila mwaka na mapato kwa figures . Mkiamua kuziweka sidhani kama hata page moja itamalizika.

Mpango wa maendeleo wa miaka mitano huwa kila mwaka unavunjya katika mpango wa mwaka mmoja mmoja ili utekelezwe kulingana na uwezo wa kibajeti wa mwaka husika hivyo mkichaguliwa najua mtakuwa mnapeleka mipango ya kiutekelezaji bungeni lakini suala la kutaja projections muhimu za macro economic indicators nilizozitaja hapo juu hazihitaji kusubiri muingie serikalini.

Uwezo wa kiuchumi wa nchi huwa haubadiliki ghafla kwa sababu tu wapinzani wameingia madarakani bali huwa ni matokeo ya mikakati na mipango ya muda mrefu ambayo matunda yake yanaweza yasiwe yamesababishwa na hao walio madarakani wakati huo. Projections za mapato zitasaidia watanzania waweze kujua kama kweli hayo mnayowaahidi watanzania kama vile majengo ya wamachinga kila mji, makazi bora kwa watanzania, elimu bure, mikopo ya wanafunzi, maji, viwanda, fidia, mishahara mikubwa, afya n.k yatatekelezeka kwa sababu wote tunajua kinachobakia kwa makusanyo haya ya sasa ambayo baada ya kulipa mishahara na madeni.

Mwisho hiyo mipango ya miaka mitano mitano iliyotekelezwa tangu 2011 sio kuwa ilikuwa inazuka tu, ina connection na Dira ya Taifa ya mwaka 2000 ambayo ilielekeza tunataka kuwa taifa la namna gani mwaka 2025, hivyo mipango na mikakati mbalimbali ilipangwa kuanzia wakati huo kama vile porvety reduction strategy, MKUKUTA I & II, n.k. HIvyo wanachofanya CCM wanatembelea mule mule ili kuweza kufanikisha hiyo Dira ya Taifa ambayo ina malengo matano .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom