Ilani za CHADEMA na ACT Wazalendo kwa upande wa uchumi hazifafanui namna pato la ndani ya nchi (GDP) litakavyokuwa linaongezeka mwaka hadi mwaka kutoka figures za sasa. Pia hazitaji watakuwa wanakusanya mapato (kodi na mapato yasiyo kodi) kiasi gani ili kuwezesha wananchi tuweze kupima hayo mambo wanayohaidi kama yanatekelezeka kwa sababu pesa ndio msingi wa utekelezaji wa ahadi za kiuchumi zinazotolewa. CHADEMA na Lissu wao kila kitu wanadai kinawezekana na watafanya kuanzia afya, elimu, makazi, ajira, mishahara mikubwa ikiambatana na nyongeza lakini hakuna mahali wanapoonyesha namna watakapopata fedha hizo. Kwao hakuna financial constraints.
Zitto yeye na ACT Wazalendo walau wao amekuwa wajanja na ilani yao inaonyesha wapi watapata fedha za kutekeleza jambo moja moja kutoka kila chanzo chake. Lakini wamekwepa aspect muhimu niloizozileza hapo juu.
Wanapaswa kwanza kueleza matarajio (projection) ya ukuaji wa uchumi kila mwaka kwa miaka yote mitano, GDP ya kila mwaka kwa figures ili iweze kujulikana kwa uhakika chini ya sera zao pato la nchi litakuwaje. Pato la nchi ndio msingi wa mapato ambayo serikali itakuwa inakusanya kwa njia ya kodi na yasiyo ya kodi. Pia walipaswa waeleze makusanyo yao ya kodi yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka na pia mapato ya ndani ya serikali kwa ujumla yatakuwa asilimia ngapi ya GDP kila mwaka. Wataje pia kwa figures (projections) watakuwa wanakusanya shilingi ngapi kila mwaka
CHADEMA na ACT Wazalendo wanapaswa watueleze (projections) watatumia shilingi ngapi kati ya makusanyo hayo ya kila mwaka kulipa mishahara hiyo mikubwa wanayoahidi na pia kulipa madeni ambayo watapaswa kuendelea kulipa. Baada ya hapo tutaweza kujua kiasi cha mapato kinachobakia kwa ajili ya kutekeleza hayo mambo makubwa wanayoahidi na watukukotolee matumizi yote kuanzia afya, elimu bure, mikopo ya elimu ya juu, maji, nyumba, viwanda, masoko nk ambavyo hasa CHADEMA wamekuwa wakidai watafanya. Kwa dunia ya sasa data zote za kiuchumi zunatabirika tena kwa figures hivyo hakuna sababu ya wao kueleza maneno matupu bila kuweka figures.
Pia ACT Wazalendo katika ilani yao niliyoisoma Mwanahalisi online (extract) kwani sijabahatika kupata kitabu kizima, wanadai kuwa mwaka wa tano makusanyo ya kodi yatakuwa asilimia 25 ya GDP. Ukiangalia makusanyo ya sasa ya kodi kwa uwiano wa GDP ni asilimia 12.9. Ni vigumu kuwa wao ACT watakuwa na muujiza wa kuongeza uwiano huo mara mbili hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka mitano tu. Ukiangalia nchi kama Kenya yenye uchumi mzuri, wao makusanyo yao kwa mwaka 2018 yalikuwa asilimia 15.09 kwa uwiano wa GDP. Wastani wa uwiano wa makusanyo ya kodi kwa GDP kwa nchi za Africa kwa mwaka 2019 ilikuwa asilimia 17.2. Hivyo utaona wanachoeleza ACT Wazalendo sio rahisi kufikiwa kwa miaka mitano tu.
Kwa mujibu wa ilani ya ACT Wazalendo waliyoiwasilisha, kodi zitakuwa kubwa sana kuliko kodi za sasa hivyo wananchi wajiendae kulipa zaidi ikiwa watashinda. Chini ya CHADEMA kwa haya matamko yao, uchumi utaporomoka sana na inflation itakuwa juu.
Ila kuna jambo moja tu katika ilani ya ACT Wazalendo ambalo linatekelezeka na ni jambo zuri nalo ni namna watakavyotatua tatizo la maji. Wamesema kuwa kwa kila lita ya mafuta (fuel) watatoza kodi maalum kama inavyofanywa kwa ujenzi wa barabara na uenezaji umeme vijijini (REA). Jambo hilo litapelekea tatizo la maji kutatuliwa.