Kashfa za Mkurugenzi Muhimbili

Kashfa za Mkurugenzi Muhimbili

Kuna dalili za ukweli wa haya mambo japo mtoa maada na mwandishi ametoa hii habari kwa mtindo wa majungu na wivu wa madaraka. Ni skitiko kubwa kwa huu ufujaji na nadhani uchunguzi wa kina unahitajika...
 
Hizo safari Njelekela anamuiga bosi mkubwa pale magogoni au?

Tiba
 
Hayo ni majungu yanayotokana na wivu wa posho za safari, na wanaomfanyia fitna ni waliokosa hizo safari sasa wanamtumia mwandiahi wa nipashe ambaye naye anatumika kama kasha la kubebea sumu asiyojua.

Anayetoa siri ya hizo namba za hundi bila shaka ni muhasibu au wanaohusika na maswala ya fedha. Bila hivyo mwandishi angepata wapi hizo namba za hundi.

We mwandishi nenda kamuulize Mhusika anayetuhumiwa usiandike stori za upande mmoja.

Usiendelee nitarudi hapa kuleta uhusiano wakimapenzi na mmoja wa wah wizara ya afya huku kijana mmoja wa moi akiendelea kufa bilakujijuwa

Nipemuda nifungue kwanza niko na swaumu Bado

Mod ihold hii thread mpaka ramadhani

Baadae nitakwambia nani anamlinda usitahamakki
 
Hata kama ni ukweli au uongo, huyu ni mkurugenzi acha naye asafiri ni malupu lupu ya mkurugenzi mbona JK anatumia 55 bn/= za safari? Mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake. Ha haaaaaaaa
 
kwa anayejua taratibu za manunuzi na malipo ya posho serikalini ataelewa hapa kuna kutafutana! hakuna pesa inatpka hovyo kwa eti mtu kuamua yeye mwenyewe bila kuwa iliombwa ktk bajeti !alipokuwa mewata michango kibao alisimamia na kufanya vizuri sana kufanikisha kazi zake!si mlizoea wakurugenzi kutoka maeneo flaniflani sasa ametoka sio huko !mwacheni achape kazi!hana mamlaka ya kufanya hayo mnayompakazia!
 
kwa anayejua taratibu za manunuzi na malipo ya posho serikalini ataelewa hapa kuna kutafutana! hakuna pesa inatpka hovyo kwa eti mtu kuamua yeye mwenyewe bila kuwa iliombwa ktk bajeti !alipokuwa mewata michango kibao alisimamia na kufanya vizuri sana kufanikisha kazi zake!si mlizoea wakurugenzi kutoka maeneo flaniflani sasa ametoka sio huko !mwacheni achape kazi!hana mamlaka ya kufanya hayo mnayompakazia!

Ufisadi upigwe vita kokote but Story ilivyowekwa kuna harufu ya kuchafulia kwa majungu. Report ya CAG inasemaje kuhusu mnh
 
haya ni majungu ya ipp siajabu amenyimwa kitalu, hizo posho mbona za kawaida sana,
 
mwenzeu alikuja kutafuta pesa.
sasa hivi anajichotea fedha,waliokosa ndio roho zinauma,ila Mungu yupo!.kwani ataondoka nazo?,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
kweli wakubwa nina shemeji yenu yupo pale huyo mama tangu aje kuna matatizo kweli .hamna majungu hapo yote ni kweli,wanamadai mengi sana na mara nyingi hana kauli nzuri na walio chini yake,sio vizuri kutetea kitu ambacho hukijui vyema.
 
kwa anayejua taratibu za manunuzi na malipo ya posho serikalini ataelewa hapa kuna kutafutana! hakuna pesa inatpka hovyo kwa eti mtu kuamua yeye mwenyewe bila kuwa iliombwa ktk bajeti !alipokuwa mewata michango kibao alisimamia na kufanya vizuri sana kufanikisha kazi zake!si mlizoea wakurugenzi kutoka maeneo flaniflani sasa ametoka sio huko !mwacheni achape kazi!hana mamlaka ya kufanya hayo mnayompakazia!

ACHA UPUNGUANI WEWE
BORA KUDESA KULIKO KU CREAM

NENDA KAULIZE KULICHOMPELEKA MAHAKAMANI DIR WA ATCL

NISAIDIE KUJUA ALINUNUAJe MAGARI. 26.kwa hela Ya used car Dubai nakupeleka receipt ya gari za new car frm japan

Shame
 
Nimesema na narudia tena sitakusema zaidi naombanimalize mfungo
 
Huu ni udaku, kwa Mkurugenzi wa Hospitali kubwa ya Muhimbili hivyo ni vijisenti.
 
Kashfa za ufujaji na matumizi mabaya ya fedha zinazomhusu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili zimeendelea kuibuliwa, wakati tanuru la kuchomea taka likiwa halijapatiwa ufumbuzi.

Licha ya hospitali hiyo kuwa taabani kifedha, kukosa vitendea kazi na wataalamu, Mkurugenzi Mtendaji Dk.Marina Njelekela, anatuhumiwa kufuja fedha kwa kujilipa posho nyingi kinyume cha sheria.

Vyanzo vya kuaminika ndani ya hospitali hiyo, vimeiambia NIPASHE Jumapili kuwa, licha ya Njelekela, kununua gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 kwa Sh. milioni 207, fedha zilizolipwa kwa kampuni ya Toyota Tanzania kupitia hundi namba 117781 ya PV P3-13-001697 ya Mei mwaka huu.

“Tangu Mkurugenzi huyu ameingia Muhimbili, amekuwa akikiuka kanuni za fedha, baada ya kuona watu wanamshtukia anamtumia katibu muhtasi wake kuchukua fedha za posho za safari anazozipanga mwenyewe akijua kuwa hazina tija,” kilidokeza chanzo kimoja.

Baadhi ya fedha zilizodaiwa kuchukuliwa na mkurugenzi huyo ni kupitia hundi yenye namba 97543 (PV-13-000100) ambayo Njelekela alijilipa Dola 5,355 (sawa na Sh. milioni 8.8) na 3,780 (Sh. milioni 6.2) kwa wakati mmoja.

Chanzo hicho kilieeleza kuwa, wakati mkurugenzi huyo akidaiwa kufanya safari zisizo na tija, hospitali ina deni la zaidi ya Sh. bilioni 12 linayojumuisha madeni ya wazabuni na stahiki za wafanyakazi hasa madaktari na wauguzi.

Aidha vyanzo vimeeleza kuwa baadhi ya safari alizofanya zilistahili kufanywa na madaktari na si mkurugenzi.

“Huu ni ufisadi na ubinafsi, mfano mwaka huu amekwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa taasisi ya watoto akalipwa Dola za kutosha, je yeye ni daktari wa watoto, basi hata angekuwa mjumbe wa chama cha madaktari wa watoto tusingelalalamika lakini hayuko kote,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Hakuishia hapo alikwenda mkutano wa kimataifa wa chama cha madaktari wa figo na ini, akavuta dola za kutosha tena , hivi yeye ni daktari wa figo na ini? Huku ni kuchukua majukumu ya wengine na kuacha kazi ya ukurugenzi…”kililalamika.

Tangu aingie Muhimbili amefanya safari zaidi ya 34 kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya Idara ya Fedha ya hospitali hiyo ambavyo vilihoji imeleta matunda gani? Wapashaji wetu wakizungumzia zaidi ubadhirifu walisema Dk.Njelekela amekuwa akijilipa posho za kujikimu ambazo wengine wakisafiri wananyimwa.

“Februari 17, mwaka huu kupitia hundi Na. 97523 alijilipa Dola 2100 (sawa na Shilingi milioni 3.5) fedha za safari iliyoanza Februari 28 hadi Machi 3 mwaka huu ,” kilieleza chanzo hicho.

Pia kilibainisha kuwa wafanyakazi hawajalipwa fedha za nauli kutoka Agosti mwaka jana hadi sasa na wanadai Sh. milioni 247.3

Chanzo kingine kilisema watumishi wa Muhimbili kwa miaka miwili hawajalipwa posho za wafanyakazi zikiwamo mapato ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), yanayotokana na kutoa huduma kwa wateja wa mfuko huo.

“Wakati deni hilo kubwa na madai ya wafanyakazi yakikwama kulipwa hospitali ina changamoto lukuki huwezi kuamini haina mita za kupima kiwango cha oksejeni anayopewa mgonjwa anayepumua kwa mashine (oxygen gauge) ambazo ni muhimu kwa wodi ya watoto wanaolazwa kila mara kwa kushindwa kupumua.

Chanzo kingine kilisema wagonjwa hujinunulia dripu na glovu na hakuna mashuka wala vyandarua vya kutosha mawodini.

Gazeti hili liliwasiliana na Dk Njelekela ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo lakini alijibu kwa jeuri kuwa anayetakiwa kuzungumzia madai hayo ni Afisa Uhusiano wa hospitali na sisi yeye.

Hata hivyo, mwandishi alipomwambia kuwa tayari amewasiliana na ofisa huyo na kujibiwa kuwa yupo Nairobi, Kenya na asingeweza kushughulikia habari hizo, Mkurugenzi Njelekela alisisitiza aendelee kuulizwa afisa uhusiano.

Awali gazeti hili, lilipowasiliana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Hospitalini hapo, Aminiel Aligaesha, ambaye alikuwa ametumiwa maswali ya tuhuma hizo , alisema kuwa yupo nje ya nchi hivyo si busara kuyajibu.

Wiki iliyopita tulichapisha taarifa kuhusu kuharibika kwa tanuru la kuchomea taka na kusababisha mabaki ya miili ya binadamu , dawa na vifaa tiba kuchomwa kwenye shimo la taka.

Pamoja na uongozi kuahidi kuwa unashughulikia tatizo hilo ili wiki hii tanuru hilo liweze kuanza kazi, lakini hadi jana NIPASHE ilifuatilia suala hilo iliambiwa bado linashughulikiwa


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Ni kawaida kwa serikali yetu kukosa pesa za kutengeneza x ray lakini za safari huwa hazikosekani hata siku moja
 
Iwe isiwe kuna tatizo Muhimbili

iwe isiwe kuna tatizo ccm. mbona kila anaeteuliwa ni mzigo ? ukianzia mawaziri kina wasira hadi wakuu wa mikoa hadi makabuti wakuu hadi wakuu wa wilaya hadi wakurugenzi. nipe watano tu walio safi nikurushie vocha sasa hhivi
 
ACHA UPUNGUANI WEWE
BORA KUDESA KULIKO KU CREAM

NENDA KAULIZE KULICHOMPELEKA MAHAKAMANI DIR WA ATCL

NISAIDIE KUJUA ALINUNUAJe MAGARI. 26.kwa hela Ya used car Dubai nakupeleka receipt ya gari za new car frm japan

Shame

KWA hiyo mkurugenzi WA ATCL akiiba ndo WA muhimbili pia aige?huyu kwani kanunua GARI used kaleta risiti ya GARI MPYA? posho kajilipa kwa rate iliyo sahihi je wapi kajilipa posho kwa rate isiyo sahihi.aheri ya Mimi punguani kuliko wewe unayejiona una akili lakini MZUSHI!hapa leta facts kanunua GARI bei sio halali !yani dollar elf TATU au tano unaona nyingi KWA safari za nje?hovyo kabisa !nenda bandarini uliza posho ya siku moja ya mkurugenzi akienda nje ni dollar ngapi ! iwap o DED wa halmashauri ya wilaya anatembelea GARI LA mil 180 cha ajabu kwa yeye kununuliwa GARI mnalomtuhumu ni nini? sema upasuke ila ndo mshashindwa majungu yenu! kama wewe unavuta Mimi nalipuliza! kwani wanaodai madeni wapo muhimbili tu?pita of c za serikali ujue? au unadhani posho ya safari haikuwa budgetted? au ndo nyinyi mlokuwa mnamuwekea vigingi enzi hizo?sasa kapata madaraka mnagwaya? Dr Marina mpambanaji tangu anasoma muhimbili!
 
mmezoea wakurugenzi wachaga..na wala msingesema!!!wacha na mtoto wa kingoni naye ale..majungu matupu.:llama:
 
Back
Top Bottom