Kashfa za Mkurugenzi Muhimbili

Kashfa za Mkurugenzi Muhimbili

iwe isiwe kuna tatizo ccm. mbona kila anaeteuliwa ni mzigo ? ukianzia mawaziri kina wasira hadi wakuu wa mikoa hadi makabuti wakuu hadi wakuu wa wilaya hadi wakurugenzi. nipe watano tu walio safi nikurushie vocha sasa hhivi
siasa we endelea nayo tu, hiyo vocha watumie wenye kutaka

Mie nabaki na mada kwamba mfumo mzima wa utendaji Tanzania ni mbovu

na wapinzani wamecopy hayohayo ndio maana issues ndogo tu lazma ziamuliwe kwa vurugu, mifarakano na vitisho
 
huyo mama ana tengenezewa zengwe tu.....kwanza kafanya makubwa kuliko mkurugenzi yoyote walitangulia, ni wivu tu.nipashe waseng..... sana wanatumiwa kumchafua mkurugenzi
 
huyo mama ana tengenezewa zengwe tu.....kwanza kafanya makubwa kuliko mkurugenzi yoyote walitangulia, ni wivu tu.nipashe waseng..... sana wanatumiwa kumchafua mkurugenzi

Kwa faida ya wana JF ungeweka hapa record ya mafanikio yake. Itasaidia sana
 
Hawa waandishi wana matatizo gani?
Bilioni 12 na hivyo viposho visivyozidi hata milioni ishirini kuna uhusiano gani?

Inaonekana gazeti linatumiwa kumchafua .....
 
KWA hiyo mkurugenzi WA ATCL akiiba ndo WA muhimbili pia aige?huyu kwani kanunua GARI used kaleta risiti ya GARI MPYA? posho kajilipa kwa rate iliyo sahihi je wapi kajilipa posho kwa rate isiyo sahihi.aheri ya Mimi punguani kuliko wewe unayejiona una akili lakini MZUSHI!hapa leta facts kanunua GARI bei sio halali !yani dollar elf TATU au tano unaona nyingi KWA safari za nje?hovyo kabisa !nenda bandarini uliza posho ya siku moja ya mkurugenzi akienda nje ni dollar ngapi ! iwap o DED wa halmashauri ya wilaya anatembelea GARI LA mil 180 cha ajabu kwa yeye kununuliwa GARI mnalomtuhumu ni nini? sema upasuke ila ndo mshashindwa majungu yenu! kama wewe unavuta Mimi nalipuliza! kwani wanaodai madeni wapo muhimbili tu?pita of c za serikali ujue? au unadhani posho ya safari haikuwa budgetted? au ndo nyinyi mlokuwa mnamuwekea vigingi enzi hizo?sasa kapata madaraka mnagwaya? Dr Marina mpambanaji tangu anasoma muhimbili!
What is your problem..!?
 
Kwani yeye Njelekela ana tofauti gani na wabadhirifu wengine wa serikali yetu? Mnashangaa kitu gani. Ndiyo mfumo wao. Dawa ni kuindoa serikali dhaifu na legelege madarakani ije iliyo imara. Kula mama as if hakuna kesho. Mbona wenzio pamoja na malalamiko ya EPA but ipo Ecrow ya bil 200.
 
Kwa faida ya wana JF ungeweka hapa record ya mafanikio yake. Itasaidia sana

mfano mmja hyo mama ameiondoa bank ya nmb kwenye compound ya muhimbili kitu ambacho wakurugenzi wa nyuma walishindwa....tangia sarungi waziri wa afya.sababu ya kuiondoa nmb hapo ilitakiwa muda maana
kulikuws na longolongo....mama yeye kafanya kweli..uliziazaidi utajua
 
Hawa waandishi wana matatizo gani?
Bilioni 12 na hivyo viposho visivyozidi hata milioni ishirini kuna uhusiano gani?

Inaonekana gazeti linatumiwa kumchafua .....
nipashe wsnatumiwa sana siku hizi kutoa habari feki
 
Jamani kweli naamini mawaziri mizigo hata malalamiko hawasikii!! Do Tanzania ni zaidi unvyoijua
 
Ccm nayo inalazimisha uongozi badala yakupambana na kero unapambana na Ukawa ngoja tuone..
 
mfano mmja hyo mama ameiondoa bank ya nmb kwenye compound ya muhimbili kitu ambacho wakurugenzi wa nyuma walishindwa....tangia sarungi waziri wa afya.sababu ya kuiondoa nmb hapo ilitakiwa muda maana
kulikuws na longolongo....mama yeye kafanya kweli..uliziazaidi utajua

Hilo nalo ni la kujivunia kweli? Linahusiana vipi na huduma za Afya au maendeleo ya mgonjwa hospitalini hapo?
 
Hilo nalo ni la kujivunia kweli? Linahusiana vipi na huduma za Afya au maendeleo ya mgonjwa hospitalini hapo?

ukweli ni kwamba anatengenezewa zengwe tu, hata hivyo muhimbili kidogo kuna afadhali ndiyo kasoro zipo.ila kuna mabadiliko makubwa kafanya mkurugenzi huyu
 
mgoni huyo anashusha bonge la ghorofa mbz sasa asile ili iweje nani akule
 
mfano mmja hyo mama ameiondoa bank ya nmb kwenye compound ya muhimbili kitu ambacho wakurugenzi wa nyuma walishindwa....tangia sarungi waziri wa afya.sababu ya kuiondoa nmb hapo ilitakiwa muda maana
kulikuws na longolongo....mama yeye kafanya kweli..uliziazaidi utajua
Huu mfano haujakaa sawa... issue ilikuwa nini kuhusu NMB.

She has been hard working during MEWATA campaigns hatukusikia ufisadi, may be kaiga. Ingawa story imekaa kimajungu.
 
Ndgu mie kwa vitendea kazi cna pingamizi lolote kuhusu kw nn visinunuiwe na kwa nn wizara siingizwe kweye brn ili kubresha afya na hakuna maendeleo pasipo uhakika wa afya bora na imara?

Ila kuhusu gari tusimwonee mama wa wtu bure coz hlo ni mali ya mnh akistaafu leo cio mali yake itabaki kuwa ya mhmbili na bajeti likuwepo na idara zliipitiha bila shaka na kuku walikula , tenda bodi lipitia specification, wazabuni walishindanshwa na bila shaka toyota ndo aliweka ghrama hyo ndogo na akapewa zabni. Swali sasa hapa marina ana kosa lipi? Kumbukeni magari haya kila taasisi yamejaa dar tuache majungu wakuu!



kashfa za ufujaji na matumizi mabaya ya fedha zinazomhusu mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya taifa muhimbili zimeendelea kuibuliwa, wakati tanuru la kuchomea taka likiwa halijapatiwa ufumbuzi.

Licha ya hospitali hiyo kuwa taabani kifedha, kukosa vitendea kazi na wataalamu, mkurugenzi mtendaji dk.marina njelekela, anatuhumiwa kufuja fedha kwa kujilipa posho nyingi kinyume cha sheria.

Vyanzo vya kuaminika ndani ya hospitali hiyo, vimeiambia nipashe jumapili kuwa, licha ya njelekela, kununua gari aina ya toyota land cruiser v8 kwa sh. Milioni 207, fedha zilizolipwa kwa kampuni ya toyota tanzania kupitia hundi namba 117781 ya pv p3-13-001697 ya mei mwaka huu.

“tangu mkurugenzi huyu ameingia muhimbili, amekuwa akikiuka kanuni za fedha, baada ya kuona watu wanamshtukia anamtumia katibu muhtasi wake kuchukua fedha za posho za safari anazozipanga mwenyewe akijua kuwa hazina tija,” kilidokeza chanzo kimoja.

Baadhi ya fedha zilizodaiwa kuchukuliwa na mkurugenzi huyo ni kupitia hundi yenye namba 97543 (pv-13-000100) ambayo njelekela alijilipa dola 5,355 (sawa na sh. Milioni 8.8) na 3,780 (sh. Milioni 6.2) kwa wakati mmoja.

Chanzo hicho kilieeleza kuwa, wakati mkurugenzi huyo akidaiwa kufanya safari zisizo na tija, hospitali ina deni la zaidi ya sh. Bilioni 12 linayojumuisha madeni ya wazabuni na stahiki za wafanyakazi hasa madaktari na wauguzi.

Aidha vyanzo vimeeleza kuwa baadhi ya safari alizofanya zilistahili kufanywa na madaktari na si mkurugenzi.

“huu ni ufisadi na ubinafsi, mfano mwaka huu amekwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa taasisi ya watoto akalipwa dola za kutosha, je yeye ni daktari wa watoto, basi hata angekuwa mjumbe wa chama cha madaktari wa watoto tusingelalalamika lakini hayuko kote,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“hakuishia hapo alikwenda mkutano wa kimataifa wa chama cha madaktari wa figo na ini, akavuta dola za kutosha tena , hivi yeye ni daktari wa figo na ini? Huku ni kuchukua majukumu ya wengine na kuacha kazi ya ukurugenzi…”kililalamika.

Tangu aingie muhimbili amefanya safari zaidi ya 34 kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya idara ya fedha ya hospitali hiyo ambavyo vilihoji imeleta matunda gani? Wapashaji wetu wakizungumzia zaidi ubadhirifu walisema dk.njelekela amekuwa akijilipa posho za kujikimu ambazo wengine wakisafiri wananyimwa.

“februari 17, mwaka huu kupitia hundi na. 97523 alijilipa dola 2100 (sawa na shilingi milioni 3.5) fedha za safari iliyoanza februari 28 hadi machi 3 mwaka huu ,” kilieleza chanzo hicho.

Pia kilibainisha kuwa wafanyakazi hawajalipwa fedha za nauli kutoka agosti mwaka jana hadi sasa na wanadai sh. Milioni 247.3

chanzo kingine kilisema watumishi wa muhimbili kwa miaka miwili hawajalipwa posho za wafanyakazi zikiwamo mapato ya mfuko wa bima ya afya (nhif), yanayotokana na kutoa huduma kwa wateja wa mfuko huo.

“wakati deni hilo kubwa na madai ya wafanyakazi yakikwama kulipwa hospitali ina changamoto lukuki huwezi kuamini haina mita za kupima kiwango cha oksejeni anayopewa mgonjwa anayepumua kwa mashine (oxygen gauge) ambazo ni muhimu kwa wodi ya watoto wanaolazwa kila mara kwa kushindwa kupumua.

Chanzo kingine kilisema wagonjwa hujinunulia dripu na glovu na hakuna mashuka wala vyandarua vya kutosha mawodini.

Gazeti hili liliwasiliana na dk njelekela ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo lakini alijibu kwa jeuri kuwa anayetakiwa kuzungumzia madai hayo ni afisa uhusiano wa hospitali na sisi yeye.

Hata hivyo, mwandishi alipomwambia kuwa tayari amewasiliana na ofisa huyo na kujibiwa kuwa yupo nairobi, kenya na asingeweza kushughulikia habari hizo, mkurugenzi njelekela alisisitiza aendelee kuulizwa afisa uhusiano.

Awali gazeti hili, lilipowasiliana na mkuu wa kitengo cha uhusiano hospitalini hapo, aminiel aligaesha, ambaye alikuwa ametumiwa maswali ya tuhuma hizo , alisema kuwa yupo nje ya nchi hivyo si busara kuyajibu.

Wiki iliyopita tulichapisha taarifa kuhusu kuharibika kwa tanuru la kuchomea taka na kusababisha mabaki ya miili ya binadamu , dawa na vifaa tiba kuchomwa kwenye shimo la taka.

Pamoja na uongozi kuahidi kuwa unashughulikia tatizo hilo ili wiki hii tanuru hilo liweze kuanza kazi, lakini hadi jana nipashe ilifuatilia suala hilo iliambiwa bado linashughulikiwa


chanzo: Nipashe jumapili
 
Jukumi la kuhakikisha hospitali ina vitendea kazi ni la nani?

Mapato ya muhimbili yanaingia kwenye ac ya muhimbili direct au hazina (ambao watatoa mgao kwa muhimbili?)

Jukumu lankuajiri wataalam ni la muhimbilia au??

Gari alinunua bika kibali au kulikuwa na kibali? Aliamka tu asubuhi akanunua gari au ilikuwepo kwenye bajeti?

Wanataka safari apangiwe na nani???

Na kama alisafiri nje ya nchi kuna ajabu gani kulioa dola?

Je wangapi walikuwa hiyo safari wakaikosa?

Stahili za wafanyakazi wanalipa muhimbili au serikali.kupitia wizara ya afya?(au muhimbili wana utaratibu tofauti na serikali?

Nanukuu baadhi ya safari zinapaswa kufanywa na madaktari...kwa hiyo kuna uwezekano baadhi ya madaktari na wahasibu wameamua kupika majungu badala ya kuhudumia wagonjwa/kufanya malipo?

Mapato ya mfuko wa afya wanalipa muhimbili au mfuko wa afya?

Manunuzi ya vifaa yanafuata taratibu gani? Msd hawahusiki?

Nawewe njelakela hizo safari wape na wenzio unaona wanataka kukutoa macho?

Na hakikisha stahili za watumishi zinalipwa maana hao kwa kuchonga ndo wenyewe


Na vifaa viwepo hospitali..... tena wewe hapo wananunua dripu temeke hadi canula(spelling) mgonjwa ananunua....xray akapige kwa dr massawe pale apeleke majibu
muhimbili inajitegemea kwa asilimia kubwa na mdio maana hata ajira zake unaomba direct pale
 
Mwacheni huyu mama apumue aisee! FastJet kila uchao iko angani hata kwa safari ambazo zingefanywa na maafisa Wa ngazi ya chini kwenye wizara mbona hamjapiga kelele? Nasikia harufu ya mfumo dume hapa! Muhongo na Werema wamepiga mabilioni ya kutosha mmenyamaza, mwacheni Dr. Marina naye ale kwa urefu Wa kamba yake!!!

Mama nampendaga huyo! Alivyotulia sasa!! Mama yuko vizuri!
 
mfano mmja hyo mama ameiondoa bank ya nmb kwenye compound ya muhimbili kitu ambacho wakurugenzi wa nyuma walishindwa....tangia sarungi waziri wa afya.sababu ya kuiondoa nmb hapo ilitakiwa muda maana
kulikuws na longolongo....mama yeye kafanya kweli..uliziazaidi utajua

Mkuu, nadhani wakuu amkawewe na chakii wanamaanisha record ya kiutendaji hasa afya, pili NMB office ilikuwa katika compound ya chuo na si Hospitali.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom