Kashfa ya makontena ya samaki toka japan?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya makontena ya samaki toka japan??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jambotemuv, Jul 27, 2011.

 1. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  "Polisi walinda maghala ya samaki wenye mionzi
  Na Moshi Lusonzo
  27th July 2011B-pepeChapaMaoni
  Askari polisi wakilinda malori yaliyopakia samaki wanaohofiwa kuwa na mionzi ya nyuklia, yakiwa yamehifadhiwa ndani ya kampuni ya Alpha Krust ya jijini Dar es Salaam jana.Serikali imeamua kuweka ulinzi mkali katika maghala ya kuhifadhia samaki ya Kampuni ya Alpha Krust ili kuhakikisha samaki hao wanaohofiwa kuathiriwa na mionzi ya nyuklia hawatolewi kinyemela."

  Wadau, hivi serikali yetu na mamlaka zake hawakujua makontena haya yaja Tz? Iweje yameruhusiwa kuingia na hata samaki kuanza kusambazwa na sasa twaanza kuchachamaa eti tunachunguza ubora wake? Hivi kweli Tanzani tuna uhaba wa samaki mpaka tuagiziwe toka Japoni? Tutegemee nini hapa kwa wandugu?
   

  Attached Files:

 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mbona hawana protective gears?!!
  Umasikini huu utatuua!
   
 3. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hapo ndo ujue yote hii yawezakuwa changa la macho tu. Si ajabu hawakusudii kuchukua hatua yoyote ya maana zaidi ya kuonyesha picha ili kupunguza makali ya maswali bungeni. Hatimaye majibu yanakuja kama yale ya karatasi za kura Tunduma?
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naishangaa serikali inavyofanya jitihada kubwa ku Import kuliko kuexport wakati baadhi ya vitu twaweza na tunazalisha wenyewe kama hili la samaki ni hatari tupu ilobaki ni kumwomba MUNGU atunusuru mwaka 2015 na serikali hii ambayo ni sumu kwa raia
   
 5. gwino

  gwino JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nafikiri Mh. Wenje atakuwa amewashtua usingizini ingawa haisadii ki2 kwani tayari samaki hao wapo mtaani
   
 6. Researcher

  Researcher Senior Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Maskini askari wetu, yaani na intelijensia yao yote wameshindwa kutambua kwamba kama kuna mionzi hata hapo walipo watadhurika?
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Serikali imetakiwa kutoa 'statement' kesho. Hata hivyo waziri wa uvuvi na mifugo Dr Mathayo katoa summary ya kustua sana bungeni.

  Kasema waingizaji ni kampuni ya Alpha Krust ya jijini Dar es Salaam, na walipata vibali vyote toka kwa TDFA na TBS!
  Nashindwa kuelewa inakuwaje mpaka dakika hii mkurugenzi wa TDFA na yule TBS wako kazini? Kwa maelezo ya waziri wameweza kupata samaki baadhi laki kuna kiasi hazikupatikana. Kwa maneno mengine watu wameshakula samaki wenye mionzi ya nuclear.

  Na hii kampuni ya Alpha Krust ya watu gani hasa? Who is behind Alpha na walishaleta chakula tena Tanzania?
  Kwa wanaofuatilia situation ya Ocean Road, wagonjwa wa cancer wanaongezeka sana na inawezekana tumekuwa tunalishwa sumu kwa muda huku tukiridhika kwa kuona nembo ya TDFA na TBS!
   
 8. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu mbona hiyo ndo kawaida Bongo? Huko Morogoro tulimuuzia kwa bei ya kutupa mwarabu kiwanda cha mafura MOPROCO na baada ya hapo tukaanza kulishwa uchafu toka nje kwa jina la mafuta Moproco. Kiwanda kikawa hakikamui tena kutoka mazao ya ndani bali waagiza uchafu toka nje na kubandika lable. Ukifunua ndoo harufu inakupalia. Ajabu ikifika sabasaba bado TBS wanawapa ushindi wa ubora wa bidhaa. Zinakuwepo sampuli za kufikishwa kwa mkemia ambazo ni tofauti na bidhaa ziwafikao walaji. Hata hili la samaki wa Japan usijeshangaa majibu yakawa ya samaki wa Mwanza. Only in Bongo land!!
   
 9. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi
  Haha haaa haaaa
   
 10. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Katika hili kuna zaidi ya hicho kinachosemwa mionzi ! kuna mtu ameomba rushwa kwa muda mrefu sana from this company but this time ndo ameamua kuchomekea hii ishu ya mionzi ..tusiwe wepesi sana wakucomment (-) hakuna cha mionzi wala nini...
  Digging more info nikiwa kamili nitawaletea .... All the docs are there hakuna longolongo
   
 11. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,736
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Mzee, As part of corporate social responsibility we are expectinmg the compnay represenatative to have something to tell Tanzanian, and prove that the fish are not from JAPAN FUKOSHIMA. Rember that we have lost trust to our authorities such that even if you can produce a lot of documents as far as the fish are from Japan nobbody will fell free from radiation. We are anstonished that even the goverment is taking too long to have something to say about this. If i would be part of the coy i would have suggested that we returning all the cargo back to japan or we destroying it for future bussiness. Dont you see it is bad image for Tanzania worlwidw that you reckless such that you have allowed such kind of think to happen, think about diplomat working in tanzania using our hotels, do you think they are taking thsi isuues as we think we people with small brains.
   
 12. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145

  Its true mkuu, samaki wamekuwa "processed" Japan Dec 2010 na tsunami ilitokea 11 March 2011, so no link kati ya hao samaki na radioactive compounds!!! Pia during neclear power explosion in Japan, it was not easy for someone to engage on fishing in that area. Pia agencies za Japan before any shipment huwa wanatoa health certificates ambazo zinacertify that the food is fit for human consumption with relevant tests reports!!
  Hii ni sabotage tu kwa hii kampuni.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  samaki watoke japan mpaka tanzania hivi inaingia akilini kweli? wakti **** mito, maziwa na bahari?

  Kazi kwenu.
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Badala ya kuwaharibu hao samaki wao wanawalinda
   
 15. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  wamedhulumiana nini?...........au wanakomoana?......Tujuze mkuu!!! au wametoka Mbweni JKT 'MBUZI BEACH'?
   
 16. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndio mana most of the wazungu hukandamiza maharage tu mana hizi nyama nyama bongo hazinauhakika wa usalama labda uchinje au kuvua mwenyewe. Serikali haina uwezo hata wakuwapima hao samaki kama wana mionzi ndo mana ngoma umeambiwa ni inahisiwa kuwa hatari wao wanakata viuno sijui wanapata wapi samaki wao au hata familia na ndugu zao hawawajali. kweli binadamu wa bongo ni selfish.
   
Loading...