TBS amkeni Magari USED ya Japan nayo Balaa si Samaki wa TFDA pekee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBS amkeni Magari USED ya Japan nayo Balaa si Samaki wa TFDA pekee

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHOST RYDER, Jul 25, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  TBS amkeni Magari USED ya Japan nayo Balaa si Samaki wa TFDA pekee

  Asubuhi ya leo nimefuatilia mahojiano kati ya Mkurugenzi wa TFDA Ramadhan Msuya na Idhaa ya Kiswahili ya BBC inayotangaza kutoka Nairobi akiwatahadharisha umma wa Watanzania kujiepusha na sehemu ya shehena ya samaki wa kusindika waliosambaa kwa wauzaji wa rejareja kutoka Nchini Japan.

  Samaki hawa hasa wanaotoka katika Miji ya Kobe na eneo jirani na ufuo wa kinu cha Nyuklia cha fukushima wanadaiwa kuwa na vinasaba vya mionzi ya Nyuklia ambayo ni hatari kwa afya ya Binadamu.

  Sehemu kubwa ya shehena hii imezuiliwa katika maghala na TFDA huku sehemu ya shehena hii tayari inavinjari katika Mini-market zilizochipuka kama uyoga katika viunga vya miji mbalimbali ya Tanzania.

  Ashkum si matusi, jana kidogo nami niingie mkenge kwa kutaka kunasa mkebe mmoja wa samaki wa Kopo wakati nafanya manunuzi Super Market, kwa bahati nzuri waziri wa mambo ya Ndani akanitolea nje vibaya…Haya hilo limepita salama

  Swali langu na hofu ya watanzania wengine Ilikuwaje sehemu ya shehena hiyo ikapenya katika mamlaka husika hadi TFDA nao waanze kuisaka katika masoko? Wahusika wanayo majibu sahihi.

  Katika mahojiano hayo Msuya alilikwepa swali la mwandishi aliyetaka kujua inakuwaje Tanzania Nchi yenye fuo nyingi na maeneo mengi ya kuwezesha uvunaji wa Samaki kuendelea kuagiza samaki kutoka Japan, alikwepa swali hilo kwa kusema kuwa '' tupeni nafsi TFDA tushughulike na majukumu yetu na kuwa hili jingine ni nje ya uwezo wa TFDA''
  Kinachogomba hapa ni kusambaa kwa mionzi hii kutokana na kuvuja kwa kwa kinu cha fukushima kufuatia tetemeko la Ardhi na Tsunami katika ukanda huo wa miji ya KOBE Nchini Japan.

  Miji ya KOBE inasifika sana kwa maarufu kwa kuwa na utitiri wa YARD za magari yaliyokwishatumika yanayouzwa katika nchi nyingi za Dunia ya tatu na Tanzania ikiwa ni soko mahiri sana kwa wafanyabishara wa Kijapan ambao sasa wamefungua matawi mengi katika jiji la Dar na Mwanza kwa kuwatumia mawakala wao.

  Kwa mtaji huo haishii tu kwa kuwatolea macho samaki hao na tukayafumbia macho magari haya ambayo Yard nyingi ni biashara za watumishi wenye mamlaka.


  My TAKE:
  • Tusiishie tu kupigia kelele minofu ya samaki, magari ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kutunza mionzi isiyokufa kwa zaidi ya miaka 100, utafiti wa kisayansi unathibitisha hili.
  • Kenya wameanza jitihada hizi magari yote kutoka Japan yatakuwa yanapimwa Bandarini kabla ya kukanyaga ardhi ya kubaini kiwango cha mionzi kufuatia malalamiko mengi ya matatizo ya kiafya kwa watumiaji wa magari kutoka Japan kufuatia kadhia la fukushima. Endapo yatabainika kuwa contaminated yataharibiwa ama kurudishwa Japan.
  • Japan pia kupitia The Japan Export Vehicle Inspection Centre (JEVIC) wamethibitisha kupokea malalamiko hayo na kuwa watafanya uchunguzi huo kupitia International Maritime Dangerous Goods Code and International Atomic Energy Agency's safety standards.
  • JEVIC tayar wameingia mkataba na TBS ya Kenya ijulikanayo kama Kenya Bureau of Standards (Kebs) lakini hapa kwetu TBS kimya mpaka tufe tuishe na magari haya ya bei chee. Uchunguzi Nchini Kenya umeanza toka mwezi Mei na unayahusisha pia magari yanayoingia Nchini humo kutokea Dubai.

  • JEVIC imethibitisha kuwa uchunguzi wa haraka umebaini magari 10 kati ya 5000 yamebainika kuwa yamebeba mionzi hii baada ya kuvuja kutoka kinu cha Fukushima.
  Madhara ya haraka unayoweza kuyahisi kama umeshaukwaa Mkoko kutoka KOBE na haukuyajua haya ni kupata kizunguzungu mara kwa mara, maumivu ya kifua na kichwa muda mfupi tu unapowasha AC ya gari wakati unaendesha.

  Vipi imekugusa hii Mdau, Chukua tahadhari wakati TBS bado wapo katika usingizi mzito.

  ADIOS
   
 2. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo la Tanzania ni serikali legelege ndo chanzo cha matatizo mengi na makubwa mno! Ni wasiwasi wangu juu ya TBS! Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya bidhaa fake mfano Dawa baridi za binadam, vyakula. Simu, n.k Yawezekana tbs bado wanatumia vifaa ya miaka ya 80's ambavyo kimsingi haviwezi kutambua madhara ya bidhaa husika ama huenda hakuna wataalam kwenye kitengo cha upimaji, Lakini pia huenda kitengo kikawa kimegubikwa na rushwa na hongo ili kuwakata kidomodomo zaidi ya hapo nahisi ni undugunization umetawala hivyo hakuna wa kumnyeshea kidole mwenzie! Bila ya kung'oa hii serikali legelege tutaangamiza taifa! MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
 3. P

  Penguine JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  You have made a very important alert Kiongozi! Nafikiri hiyo ndiyo maana sahihi ya kuwepo kwa JF. Endapo magari hayo yatakuwa na shida hiyo, shida tunayo kweli.

  Thank u 4this useful post kwa kweli mwe!
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Serikali legelege kama hii inaweza kufikiri katika direction hii kweli? Thanks for the alert but ahhhhhh .
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Itabidi mnaoweza mnunue vifaa vya kubaini mionzi, nikumbuka Fizikia yangu ya miaka ya 70 vilikuwa vikiitwa "geiga mula" counter. kabla ya kununua gari au chochote cha mashaka unakitumia!
   
 6. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili ni jambo la muhimu sana kuzingatia ,Hata kama tumechelewa kiasi gani ,Ipo fursa ya kuwaokoa wale wachache ambao hawajaathirika.Wakati ni huu zuia janga la athari za mionzi ya nuklia hapa Tanzania.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  dah!pale utakapopanda daladala iliyoathirika na mionzi!
   
 8. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Tatizo la tanzania, kukishakuwa na tetesi ya bidhaa ambayo inamadhara kwa afya ya binadamu, kwa maana hiyo ni haramu kuingia nchini, basi hiyo hugeuka kuwa ni deal kwa TFDA and TBS officials, kwani uingizaji wake utabidi uingizwe kwa kupitia back door which translates to whealth to the people tuliowaamini kulinda afya zetu watanzania. Mimi nimepoteza imani na TFDA na TBS siku nyingi sana, ninachokifanya ni kula vyakula asilia, na bidhaa nyingine nanunua tu huku ninajua kuwa ninaumia kwani havina ubora unaostahili. Muuzaji mmoja akanionyesha nembo ya TBS, nikacheka sana, nikamwambia this doesnt mean any thing to me!!!. Sisi watanzania ni kama watoto wa mitaani, hatuna wa kututetea wala kulinda afya zetu. Kitu ambacho kina potential health effect basi hugeuka mradi kwa hawa maofisa>>
   
 9. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tatizo jingine ni Watanzania wenyewe tunapenda sana short cut na huwa hatukubali kushindwa kitu wala kukubali ushauri wa Kitaalam, kwa kuwa tu nafsi yako imeridhika uko radhi kutumia mbinu yoyote lengo lako litimie.

  Mchezo huu ndio umekuwa ukitia mwanya kwa wenye mamlaka kuwa na sababu ya kutukamua kutokana na ujuaji na ujuha wetu, mfano mzuri ni zoezi la sasa linaloendelea la Utoaji wa leseni Mpya, Vigezo masharti na taratibu zote zipo wazi lakini Mbongo atajiuliza taratibu zote hizi za nini wakati nikimega fungu kidogo tu vyote hivi inakuwa hadithi ya funika Kombe.

  So wataendaji wenye njaa nao wameukumbatia mchezo huu kwa hiyo mambo saaafi tu. Wkati tunabadili passport Mpya pale Uhamiaji ungefika zile siku za kwanza mpaka raha unapata huduma kwa uharaka na bila malipo ya uchochoroni, Nenda leo sasa wapenda shortcut walivyovuruga mfumo utachoka na roho yako.
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,319
  Likes Received: 5,644
  Trophy Points: 280
  umeonaaaa eeeh!!!
   
 11. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Heshima Kwako Mkuu..
  Uko sawa kabisa, issue yoyote ikishakuwa banned au illegal ndo unakuwa mtaji kwa wenzetu tulowapa dhamana ya kulinda afya zetu. Hii inasononesha sana hasa ukizingatia ya kuwa hizo mali/hela hawatazikwi nazo sana sana watakuwa answerable on the judgement day.
   
 12. rachi

  rachi New Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiukweli hoja hii nitam sana ndugu yangu kiukweri mi binafsi nami nimekuwa na wasiwasi na kitengo hiki cha TBS kiasi kwamba nahisi rushwa imewaganda ktk vichwa vyao ama hawako makini kabisa wakati mwingine naona bora hiki kitengo kinge futwa au kubadirishwa watendaji wake maana bidhaa nyingi zinaingia madukani zikiwa feki,nasema si watendaji wazuri nibora kifutwe au wabadilishwe watendaji ninasababu muhimu ili kunusuru uhai wetu nahisi TBS haipo.
   
Loading...