Kashfa nzito Muhimbili

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]06 FEBRUARY 2012[/h][h=3][/h]

*Kitengo cha Figo chahujumiwa
*Vifaa vyahamishiwa hospitali binafsi
*Rais Kikwete aingizwa mkenge

Na Mwandishi wetu

VIFAA vinavyotumika kupima ugonjwa wa figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), vinachukuliwa kinyume cha sheria na kwenda kutumika katika hospitali binafsi. Majira Jumapili limeelezwa.

Vifaa hivyo vilivyoko katika Kitengo cha Figo MNH ni pamoja na filta (Filter) ambapo mtoa taarifa anaeleza kuwa, kinapelekwa katika Kliniki ya Kidney iliyopo Msasani Beach jijini Dar es Salaam kiwanja namba MSN/BLM/1118.

Chanzo kutoka katika kliniki hiyo kinaeleza, Dkt. Linda Ezekiel ambaye ni mmiliki wa kliniki hiyo pia Mkuu wa Kitengo cha Figo Muhimbili amekuwa akichukua kifaa hicho na kukitumia katika kliniki yake huku akiwaelekeza wagonjwa anaokutana nao Muhimbili kwenda kutibiwa katika kliniki yake.

Alipopigiwa simu ili kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizi awali Dkt. Ezekiel hakupokea lakini baada ya muda mchache alipiga na kuzungumza kwa jazba huku akimtaka mwandishi kumpelekea ushaidi ndani ya nusu saa.

“Ninaomba uniletee ushaidi ndani ya nusu saa kama mimi natumia filter za Muhimbili kwenye Kliniki yangu, na nitapiga simu ndani ya dakika 5 ili niongee na mhariri wako," alisema ambapo pamoja na kuahidi hivyo, Dkt. Ezekiel hakupiga tena simu.

Kitengo cha Figo Muhimbili kinajumuisha maabara, kliniki na idara inayoshughulika na kusafisha damu ya wagonjwa wa figo matibabu ambayo kitaalamu yanaitwa Haemodialysis.

Mwandishi wa habari hizi alifika kliniki hapo na kujifanya amepeleka mgonjwa kutoka Iringa ambapo alimuliza muuguzi wa kliniki hiyo bei za huduma.

Bila kujua kama anazungumza na mwandishi, muuguzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Kamisache alisema, kumuona daktari huyo bingwa gharama yake ni sh. 50,000 na dialysis hutozwa kwa sh. 255,000 na sindano sh 120,000 ambapo huduma hiyo hutolewa Muhimbili bure.

Mama Kimisache alimwambia 'mteja wake' kliniki hiyo inamilikiwa na Dkt. Ezekiel wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Chanzo cha Majira Jumapili kilieleza kuwa Dkt. Ezekiel alipata mashine nne za kusafishia figo kutoka moja ya hospitali za Apollo nchini India kwa bei ya chini kwa masharti ya kununua vifaa mbalimbali vya kuendeshea mashine hizo pia kupeleka wagonjwa kwao kwa msaada wa serikali.

“Unajuwa serikali yetu tangu tupate Uhuru haikuwahi kupata msaada kama huo au kuwa na bajeti ya kuweza kununua mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo," kilieleza chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, pamoja na Muhimbili kuwa na mashine saba aina ya GAMBO za kusafishia damu zilizopatikana baada ya Chuo Kikuu cha Bergen, Norway kuipa serikali msaada, mpaka sasa zinazofanya kazi ni tatu ambapo nne zimeharibika hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa.

Kitengo cha Figo Muhimbili kilifunguliwa na Rais Jakaya Kikwete Novemba 2, 2009 kikiwa na mashine zilizoelezwa kuwa mpya na za kisasa aina ya Gambo AK SAB kutoka Norway, hata hivyo chanzo hicho kinaeleza kuwa mashine hizo sio mpya ambapo nne hazifanyi kazi mpaka sasa.

Siku ya uzinduzi wa kitengo hicho Rais Kikwete aliwatangazia wagonjwa wa figo nchini kuwa, mashine hizo zitaanza kufanya kazi mara moja lakini zilianza kufanya kazi Mei 12, mwaka jana.

"Ucheleweshwaji wa makusudi ulikuwa unafanywa kwa makusudi ili wagonjwa wenye matatizo ya figo waende Msasani" kilieleza chanzo hicho.

Akitakiwa kueleza sababu za mashine hizo kutotumika kwa muda mrefu pia kuharibika kwa mashine nne Muhimbili hapo, Dkt. Ezekiel alijibu kuwa, hawezi kuongea lolote kuhusu suala hilo.

"Wewe andika unavyoona sawa, ila mimi siwezi kuongea chochote kuhusu suala hilo. Mimi nitaongea na Ofisa habari wetu Muhimbili," alijibu Dkt. Ezekiel.

Mmoja wa madaktari Muhimbili katika Kitengo cha Figo alisema, yapo mambo mengi yanayotendeka Muhimbili na kuongeza kuwa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) isiishie kuwachunguza wanasiasa pekee, ifanye kazi pia Hospitalini hapo.

"Kwa muda mrefu katika kitengo hiki huduma imekuwa sivyo inavyopaswa kuwa, taarifa za wagonjwa kuelekezwa Msasani nilizisikia lakini siwezi kuthibitisha nadhani PCCB wanaweza kufanya kazi hiyo," alisema dokta huyo.


Hata hivyo, taariza zilidai kuwa, Katibu wa Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni ana hisa katika Kliniki hiyo ambapo Februari 2 mwandishi wa habari hizi alimtafuta ili kupata ukweli, alipopigiwa simu alijibu anaendesha gari na kwamba, atapigia baadaye lakini hakufanya hivyo.

Jana mwandishi wa habari hizi alimpigia tena simu Bi. Nyoni ili kutoa ufafanuzi, alijibu kuwa yupo kwenye kikao.

Mwandishi alitembelea kitengo hicho Muhimbili na kukutana muuguzi ambaye aliekiri kuwa, baada ya uzinduzi uliofanywa na Rais Kikwete, ilichukua muda mrefu kuanza kwa huduma hizi.

"Sijui miaka miwili sijui zaidi lakini mimi sina uhakika, huduma hizi zilichelewa ikilinganishwa na muda ilipozinduliwa," alisema muuguzi huyo.



 
Muhimbili needed to be privatised, and stop few greedy people to benefit from the few Money GVT invested
 
jamani huyu Blandina Nyoni kwanini wanamshindwa??????????
mwekeni pembeni na vifaa vya figo virudishwe waliohusika washtakiwe
hata akiachia ngazi kamateni na mali zake zote
 
Serious huyu mama yuko kila sehemu, what's wrong with her, JK kwanini hauwatumi UWT wakamwangalia huyu mama, anaweza kuwa demerge kwako na CCM.
 
muda mwengine soma af toa hoja kwa kufupisha,ona sasa umeachiwa thred yako.watu hawana muda wa kusoma wewe
 
Ajabu nini ka mawaziri wanapaki magari ya gvt kwenye bar,kwa nini ma Dr.Wasifanye uhamisho wa vifaa,nchi haina mwenyewe hii,chukua chako mapema.
 
Watanzania HATUNA BUDI kuwaondoa mafisadi wote waliopo madarakani. Wafadhili wetu wameshasema: Kama hamtaki kutatua matatizo yenu, basi msije kwetu. Pesa zetu ni za kutatua matatizo yetu, tunayo LUKUKI!

Hivi kweli tunashindwa KULINDA KURA ZETU zisiende kwa CCM, tuwang'oe hawa mafisadi ifikapo 2015? Kwanza ninadhani Kikwete anaweza kulivunja Bunge, Uchaguzi Mkuu ukaja mapema zaidi. Si wanataka kutoka nje ya Bunge kwa kuwa wanapinga kitendo chake cha kukutana na CHADEMA Ikulu kuzungumzia suala la Katiba Mpya, ambao wao wanaona eti ina maslahi makubwa kwa CHADEMA?

Duuuu! Uzalendo KWISHNEY!

Mimi nilidhani sababu ni ya maana zaidi!

Akina Mama Nyoni waondolewe! Wazungu wameshatuchoka! Anna Abdallah alimfukuza mwanzilishi wa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Dr. Uma Grob. Yaani ufisadi NJE NJE! Kisa? Kwa kuwa Dr. Uma alikuwa anadhibiti ULAJI wa pesa zilizokuwa zinatoka Uswisi kusimamia MOI.
 
hEBU chunguzeni mjue link ya huyo Dr. na kigogo mmoja hapo wizarani, mtashangaa
 
Kumbe kuna mengi ndani ya mgomo huu. Hivi huyo Dr. Ezekiel anaweza kugoma kweli? Nchi hii inahujumiwa kulia, kati, kushoto, nyuma na mbele. Vifaa vya alipakodi ndivyo vinatumika kuwanyonya walipa kodi! Masikini Tanzania yangu.
 
Wizara ya afya ipo wapi? Funga hiiyo hospitali ASAP! tutaweza kupambana na hawa wapungawazi wanaoifilisi nchi bila huruma. Kibaya zaidi ni Watanzania wangapi wanaweza hizo gharama. Hivi mijitu mingine ipoje?
 
Back
Top Bottom