Kashfa nyingine nzito kwa Polisi Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa nyingine nzito kwa Polisi Arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 20, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,600
  Likes Received: 415,734
  Trophy Points: 280
  Kashfa nyingine nzito kwa Polisi Arusha

  na Violet Tillya, Arusha

  [​IMG] WAKATI wakazi wa Arusha wakiwa bado na kumbukumbu ya machungu ya kupotelewa na wenzao watatu waliouawa na Jeshi la Polisi kwa kufyatuliwa risasi za moto kwenye vurugu za kisiasa zilizotokea Januari 5 mwaka huu, Jeshi la Polisi mjini hapa limekumbwa na kashfa nyingine nzito kwa askari wake mmoja aliyekuwa amevaa sare za jeshi hilo kumfyatulia risasi ya shingoni dereva teksi mmoja na kumjeruhi vibaya.
  Dereva huyo amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Selian mjini hapa.
  Taarifa za tukio hilo zimeeleza askari huyo ambaye polisi bado wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, alifika katika eneo la Shivaz Kaloleni majira ya saa 10 usiku ambapo dereva teksi huyo huegesha gari lake hapo na kumtaka ampeleke katika Kituo cha Polisi cha Ngarenaro baada ya makubaliano ya kulipwa shilingi 3,000.
  Imeelezwa mara baada ya kufika karibu na kituo hicho, askari huyo alimwamuru dereva huyo kusimama na alimtaka ampatie shilingi 7,000 ili ampe noti ya shilingi 10,000.
  Wakati dereva huyo aliyetambulika kwa jina la Jamal Abdul (32) akijaribu kutoa noti hiyo ya shilingi 10,000, askari huyo aliyekuwa ametoka nje ya gari hilo ghafla aliikoki silaha hiyo na kumfyatulia risasi moja iliyompata sehemu ya shingo na kutokeza upande wa pili na kumjeruhi pia katika bega la kushoto.
  Aidha, kwa mujibu wa maelezo ya dereva huyo aliyekuwa akiongea kwa taabu hospitalini hapo, alisema anamtambua mtu huyo kuwa ni askari polisi na kwamba mara baada ya kukumbwa na masahibu hayo aliamua kufika katika kituo hicho cha polisi Ngarenero kuomba msaada.
  Alisema chakushangaza mara baada ya kufika kituoni hapo askari waliokuwa zamu siku hiyo waligoma kumfungulia mlango na kumtaka aende kituo kikuu cha polisi mjini kwa ajili ya kupata msaada zaidi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,600
  Likes Received: 415,734
  Trophy Points: 280
  Ukizoea kula mzoga wa mtu utaendelea vivyo hivyo...............
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Again.....yale yale
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yooooooooooooooooooooooooo....................................mayoooooooooooooooooooooooooooooh twafwa kama ishu yenyewe ni hivyo may be kulikua na jambo jingine walibishana
   
 5. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Labda alitaka kuvamia kituo cha polisi kama polisi wanavyo jitetea! Watanzania twafa!

  Jana nilimsikia waziri wa habari na michezo Nchimbi kuwa amani na utulivu iliyomo nchini imesababishwa na waaandishi wa habari. Tanzania kuna amani na utulivu? Waziri huyu mbona amewaka pasipo aibu?
   
 6. 2my

  2my JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lol jaman pole zake huyo dereva tax ila mbona ht sababu ya kumjeruhi kijana wa wa2 sioni km ni kubwa kivile?au kulikuwa na lingine?duh arusha ina mambo mara baba kung'ata kidole cha mkewe na kuuwa watoto wake wanne na yeye kujinyonga jamani tunaenda wapi?
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  au kulikuwa na taarifa za "kiintelijensia" hapo, ndio maana akampiga risasi?
   
 8. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Sasa na hapo akitokea askofu kulaani kitendo hicho mashehe watakuja juu.....?!!!
   
 9. m

  msham Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du> Tumwombee huyo derava apone kwanza, kisha tuanze libeneke lingine na huyo mtuhumiwa
   
 10. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sababu za "kiintelijensia"ila haya mambo yana mwisho wake.
   
 11. Abigree

  Abigree Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhan kulikua na taarifa za kiintelejinsia hapo
   
 12. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Serikali na vyombo vinavyohusika visipo chukua hatua madhubuti kwa askari, vita kati ya wananchi na polisi hapa Arusha haviko mbali kama vitendo hivi vitaendelea.

  Kwanza askari wengi kwa sasa wanapangisha nyumba uraiani, hivyo usalama wao utakuwa duni.
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  duh...huu sasa ni uuaji!!
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  20th January 2011
  Polisi adaiwa kumpiga risasi dereva teksi Arusha
  Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linadaiwa kukumbwa na kashfa nyingine, baada ya askari wake mmoja kumpiga risasi ya shingoni dereva wa teksi na kumjeruhi.
  Askari huyo ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi hilo huku akiwa na bunduki aina ya SMG, alimpiga dereva huyo risasi sehemu ya shingoni
  Dereva huyo, Jamal Abdul (32), amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospital ya Selian jijini hapa.
  Taarifa za tukio hilo zimeeleza kuwa askari huyo ambaye polisi bado wanafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, alifika katika eneo la Shivaz, Kaloleni Jumatatu wiki hii majira ya saa 10:00 alfajiri, ambako dereva taksi huyo huegesha gari lake namba T.976 AGZ aina ya Toyota Mark II saloon, na kumtaka ampeleke katika kituo cha Polisi cha Ngarenaro, baada ya makubaliano ya kulipwa Sh. 3,000.
  Imeelezwa kuwa baada ya kufika karibu na kituo hicho, askari huyo alimwamuru dareva huyo kusimama na alimtaka ampatie Sh. 7,000 ili ampe noti ya Sh. 10,000.
  Wakati dereva huyo akijaribu kutoa noti hiyo 10,000 ,askari huyo aliyekuwa ametoka nje ya gari hilo, ghafla aliikoki bunduki na kumfyatulia risasi moja iliyompata Abdul sehemu ya shingo na kutokeza upande wa pili na kumjeruhi pia katika bega la kushoto.
  Kwa mujibu wa maelezo ya dereva huyo aliyekuwa akiongea kwa taabu hospitalini hapo, anamtambua mtu huyo kuwa ni askari polisi na kwamba baada ya kukumbwa na masahibu hayo, aliamua kwenda katika kituo cha polisi Ngarenero, kuomba msaada.
  "Chakushangaza mara baada ya kufika kituoni hapo, askari wa waliokuwa zamu siku hiyo waligoma kunifungulia, mlango na kunitaka niende kituo kikuu cha polisi mjini kati kwa ajili ya kupata msaada zaidi," alisema Abdul.
  Alisema wakati akiwa na askari huyo wakielekea Ngarenaro, cha kushangaza kila wakati askari huyo alikuwa akiwasiliana na watu kadhaa kwa simu muda wote.
  Inadaiwa kuwa baada ya askari huyo kumpiga dereva huyo, alipora gari hilo na kuelekea eneo la Mbauda, ambapo alifanya tukio la uporaji wa fedha katika kituo kimoja cha mafuta akiwa na wenzake.
  Habari zaidi zilieleza kuwa baada ya tukio hilo la uporaji, askari huyo na wenzake waliondoka na gari hilo, lakini waliligonga gari aina ya Toyota Hiace eneo la Mbauda na kuamua kulitelekeza gari hilo na kutokomea kusikojulikana wakiwa na mfuko wa fedha.
  Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa mfuko huo ulikuwa ukidondosha fedha barabarani, huku askari huyo na wenzake wakiendelea kukimbia wakiwa wamevaa sare za polisi na SMG.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Thobias Andengenye, alisema kuwa taarifa juu ya tukio hilo amezipata na wanafanya uchunguzi.
  "Tutatoa taarifa juu ya tukio hilo, bado tunafanya uchunguzi kubaini ni askari gani alihusika na tukio hilo, maana inawezekana pia siyo askari bali majambazi waliamua kuvaa sare ili kujifanya polisi," alisema Andengenye.
  Hata hivyo, familia ya Abdul waliokutwa wodini hapo, ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walilalamikia Jeshi la Polisi kwa kushindwa kutoa ushirikiano juu ya tukio hilo, japo wanakiri kuwa baadhi ya viongozi wa jeshi hilo, wamefika hospitalini hapo kumjulia hali majeruhi huyo.

  CHANZO: NIPASHE
   
 15. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #15

Loading...