Kashfa Nyingine nne nzito Zinakuja

Kashfa Nyingine nne nzito Zinakuja

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
ZITTO+PX.jpg


Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto amesema baada ya kukamilisha shughuli ya ufisadi wa Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo Sh306 bilioni zilichotwa, kamati yake sasa inaelekeza nguvu katika kashfa nyingine nne.

Zitto alisema kamati yake itatumia mwezi huu na Januari kupitia ripoti nne ambazo zina masilahi kwa Taifa, ikiwamo ya utoaji wa vibali vya kuagiza na kuingiza sukari nchini.

Alisema ufisadi katika utoaji wa vibali hivyo ni mkubwa kuliko sakata la escrow... "Hili linagusa moja kwa moja maisha ya wananchi, wamiliki wa viwanda na uzalishaji. Tayari tumewaita Bodi ya Sukari tujadiliane kwa kina kuhusu suala hili," alisema.

Mbali na suala la sukari, alizitaja ripoti nyingine kuwa ni ya uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari na mikataba ya gesi.

"Baada ya kazi ya PAC, tunapumzika, kwani kama unavyojua kazi ilikuwa ngumu, wiki mbili nilikuwa silali. Kwa kuwa tuna ratiba ya wiki mbili. Kwa Desemba na Januari tutaanza kuzifanyia kazi," alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Wiki iliyopita, Bunge lilijadili ripoti ya PAC kuhusu ufisadi katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuhitimishwa kwa kuweka maazimio manane yakiwamo ya kuitaka Serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wengine wakuu huku likitaka pia uchunguzi uendelee kwa wote waliotuhumiwa kupokea fedha hizo kwa njia moja au nyingine.

Kauli ya Zitto inakuja wiki moja baada ya wamiliki wa viwanda vya sukari vya Kagera, Mtibwa na Kilombero kutishia kuvifunga kutokana na kuviendesha kwa hasara.

Wamiliki hao walisema watafunga viwanda hivyo kutokana na Serikali kushindwa kuzuia uagizwaji wa sukari nchini kinyume cha taratibu.

Mkurugenzi wa Viwanda vya Kagera na Mtibwa, Seif Seif alisema uagizaji wa sukari kutoka nje unafanyika kwa ushirikiano wa wafanyabiashara wakubwa na vigogo serikalini kinyume cha makubaliano na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya viwanda.

"Tulikubaliana kwamba Serikali iwe inaagiza tani 100,000 kutoka nje lakini sukari inayoingizwa sokoni ni zaidi ya tani hizo. Sukari tunayozalisha katika viwanda vyetu ipo na haina pa kwenda," alisema Seif na kuongeza:

"Leo ukipita katika maduka utakutana na sukari ya kila aina, wafanyabiashara wanaoagiza wanawatumia vigogo serikalini kuingiza sukari wapendavyo, tena bila kulipa kodi," alisema Seif.

Kutokana na hali hiyo, Seif alisema wamelazimika kupunguza wafanyakazi 2,000 na kubakiwa na 5,000 katika Kiwanda cha Kagera, Kilombero imepunguza 3,000 na wamebaki 6,000 huku Mtibwa ikiondoa wafanyakazi 3,000.

"Hali ni mbaya, si kama Watanzania wanavyofikiri. Tukifunga kabisa Watanzania wengi watakosa ajira kama ambavyo mnaona wengine wamekosa, hatuwezi kuendelea kufanya biashara ya hasara ambayo Serikali inaihalalisha," alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Sukari Kilombero, Balozi Ami Mpungwe alisema: "Hali ni mbaya, tunaona kuliko kuendelea na hali hii ni bora tusimame kuzalisha sukari.

"Serikali kama kweli ina dhamira ya kuvifufua na kuviendeleza viwanda vyetu vya ndani ni lazima kuvilinda na kupiga marufuku uagizwaji holela wa sukari kutoka nje."


Chanzo: Mwananchi Decemba 2, 2014
 
Kama mnalitafuta joka basi huyu escrow ni yai tena moja tu!


polepole.jpg

Humphrey Polepole
hatupaswi kufurahia kushughulika na matokeo bali uhodari wetu wa kuzuia mabalaa.

Kama ambavyo Watanzania wengi wiki hii na siku chache zinazokuja mijadala yao imegubikwa na sakata la Akaunti ya Escrow na tuhuma za ukwapuaji wa mabilioni ya pesa za Watanzania na mimi nitumie fursa hii kujadiliana nanyi kuhusu nafasi ya Katiba katika kuzuia ubadhirifu wa mali ya umma.

Kwa namna ninavyoona mambo yanakwenda Watanzania tusipokuwa makini tutakuwa watu wa matukio, watu wanaoendeshwa kwa matukio, kama tukikubali hali hiyo itakuwa jambo baya sana kwa taifa letu. Matukio kama haya huwa ni matokeo ya chanzo fulani, matukio haya huwa ni chanzo cha udhaifu wa mifumo yetu ya udhibiti pahala fulani. Kwa sababu haiwezekani jambo likishatokea ndio tuulizane ilikuwa kuwa vipi, nafuatilia mjadala wa Bunge ninaona kila anayezungumza ama anasema mtu au taasisi fulani alipaswa kujua.

Haya mambo hayakufanyika kwa kutumia mbinu za kijasusi, mbinu ambazo hutumia intelijensia ya hali ya juu kiasi kwamba hata kama ulikuwa mlinzi anayelinda lango lakini mtu akapita katika lango hilo pasina kuonekana. Jambo linaloendelea kujadiliwa bungeni wala halikutokea kwa kificho au kutumia intelijensia ya hali ya juu kufanya wanaotuhumiwa kutenda wasijulikane kwa namna yoyote, la hasha.

Hii inanipeleka katika hoja nyingine kwamba, unapoona katika nchi yenye utawala wa sheria, mchana kweupe mambo makubwa na ya kutisha hasa yale yenye nasaba na ubadhirifu wa mali ya umma yanafanyika mchana kweupe basi hatupaswi kusubiri kuona mawingu kujua mvua itanyesha.

Ninayaandika haya kwa maana ya kujifunza, hata kama tungepata Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri wazuri kiasi gani, kama mifumo ya utawala wa nchi haijashonwa vema na kwa umadhubuti kikatiba kazi yao njema ingeishia katika jitihada zao za kibinadamu na kukosa usaidizi wa mifumo na taasisi za kikatiba. Binadamu kwa asili amekuwa kiumbe ambaye bila kujitungia kanuni huwa ni msumbufu kabisa, hata kama binadamu ni mwema kiasi gani, iwapo ataishi katika mazingira yasiyo na kanuni basi wema wake utakuwa hatarini kughiribika.

Katika ulimwengu wa leo utaratibu wa kuenenda katika jamii na Taifa lolote lile ni Katiba na sisi tumeamua kuandika Katiba Mpya na Bora. Ni Katiba Mpya na Bora ndiyo pekee inaweza kuwa silaha ya mwisho kuliangamiza joka ambalo limekuwa likitaga mayai kama vile Epa, Majengo ya Benki Kuu, Richmond na haya ni mayai ambayo tumeyaokota kweupe, bado hatuna hakika ya mayai ambayo joka ameyataga kwenye mashimo, vichakani na mayai ambayo joka huenda akayataga hivi karibuni tena. Sumu ya joka ni Katiba Mpya ambayo inatuwezesha wananchi kutumia mamlaka yetu kuiwajibisha Serikali, Bunge na Mahakama. Nchi ambazo zilipuuza kushughulika na joka kikatiba zimeishia kuwa mataifa yaliyoshindwa "failed states". Tusikubali kufika huko.


Kama mnalitafuta joka basi huyu escrow ni yai tena moja tu!


Matukio ya escrow na Katiba

Nitumie pia fursa hii kutoa rai yangu kwa Watanzania kwamba, kuwa na Katiba Bora na inayotungwa na wananchi ndiyo mwarobaini wa kuziba mianya ya ubadhirifu katika Taifa letu. Kuwa na Katiba Bora ndiyo itakuwa salama yetu katika kuona wale tuliowapa dhamana wanawajibika haraka iwezekanavyo pindi tuhuma za ubadhirifu zinapotokea katika maeneo na mamlaka yao.

Sikiliza na usome pia, kwa namna ambavyo mjadala wa sakata hili umejipambanua katika Bunge letu la Jamhuri je, unadhani, viongozi wetu hawa watadiriki kwenda kutunga masharti makali na magumu ya kuwawajibisha viongozi wanafanya ubadhirifu wa mali ya umma, ilhali wao wenyewe ni viongozi wa umma wakati huo?

Nikuoneshe kidogo Rasimu ya Warioba ilisema hivi katika suala la Maadili na Miiko ya Viongozi na Watumishi wa Umma, akiwa katika kazi za ofisi au kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine, atahakikisha kwamba mwenendo wake: hauruhusu kutokea mgongano wa masilahi kati ya masilahi binafsi na maslahi ya utumishi wa umma; hauhatarishi masilahi ya umma kwa ajili ya masilahi binafsi; au haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi. (2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kusimamia utekelezaji wa masharti yanayohusu kanuni za uongozi wa umma. (3) Wadhifa wa "Kiongozi wa umma" kama ulivyotumika katika Sehemu hii utajumuisha viongozi wa kuchaguliwa (hii inamaanisha Rais, makamu wa rais, wabunge, madiwani n.k) na kuteuliwa (Mfano, mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za Serikali n.k) kama watakavyoainishwa kwenye sheria za nchi.

 
Hizo za Sukari Pinda anahusika moja kwa moja, kwani kawapa marafiki au watu waliokaribu naye hiyo kazi ya kuagiza sukari na kuahidiwa "Msaada wa hali na mali mwakani" pinda anajisahau sana sijui kwa nini? yakimfika shingoni ndo anaomba msaada wa kusaidiwa asiwajibishwe.

Hiyo ya Gas!!!!
 
Kama JK ni msikivu avunje Baraza LOOOOTE
Hizo za Sukari Pinda anahusika moja kwa moja, kwani kawapa marafiki au watu waliokaribu naye hiyo kazi ya kuagiza sukari na kuahidiwa "Msaada wa hali na mali mwakani" pinda anajisahau sana sijui kwa nini? yakimfika shingoni ndo anaomba msaada wa kusaidiwa asiwajibishwe.

Hiyo ya Gas!!!!
 
Udhaifu wa serikali unasababisha nchi kuonekana dampo la kila kitu toka nje haijashindwa kuzuia il a inawezekana kuna maslahi ya watu binafsi
 
Watanzania ni wepesi kusahau na wagumu kukumbuka yaliyopita, EPA, Richmond, Tokomeza, , Ulimboka, Bomba la gesi, Escrow, vijisent, n.k. Walishasoma tabia ya watanzania walivyo na wanaitumia vema tabia hii ya watanzania kujineemesha. Itatubidi sasa tuache kucheza na makatibu, mawaziri na mawaziri wakati wa matukio yanayoligharimu taifa, badala yake tuhamie kwa baba mwenye nyumba labda itasaidia ingawa inaweza kuwa ghali kwetu.
 
Watanzania ni wepesi kusahau na wagumu kukumbuka yaliyopita, EPA, Richmond, Tokomeza, , Ulimboka, Bomba la gesi, Escrow, vijisent, n.k. Walishasoma tabia ya watanzania walivyo na wanaitumia tabia hii watanzania vizuri sana.
news is seven days wonder-Bill Clinton
 
Back
Top Bottom