Kashfa - Naibu Waziri Janeti Mbene ameanza kutumia madaraka yake vibaya


Mkuu Pasco namkumbuka huyu waziri aliamrisha uvunjwaji wa jengo binafsi katika sehemu nyeti ya ardhi pembezoni mwa fukwe ya barabara (ocean road beach area) na mkabala wa kiwanja cha gofu cha Gymkana. Aliwapa wamiliki binafsi wote notisi ya kuwataka kuhama na mkono wa sheria ungelifika na hakuna cha kuusimamisha. Lakini tangu kipindi hicho, inaonekana ule mchakamchaka na kuendelezwa kwa umakini sambamba na maneno ya Rais umerudisha nyuma juhudi za waziri kushughulikia uvamizi wa maeneo na upangiwaji pia uvamizi umeendelea kama tabia.

Vitendo vya uporaji wa ardhi kupitia rushwa vimekuwa vikiongezeka kwa kasi na kuwa tatizo tete kwa Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla. Kiuhalisia kwa wananchi wa kawaida hakuna mabadiliko. Waziri yupo kimya. Mambo yanaenda kama kawaida. Hakika kuna watu wananufaika sana kutokana na hali hii ya kuachiliwa mambo kwenda mrama. Ila tujiandae na majibu ya kuwajibu wajukuu wetu kwa nini Dar Es Salaam hakuna sehemu ya wazi ya watoto kucheza. Sidhani kama wataridhika na jibu kuwa tumejenga ofisi za serikali za mitaa!
 
Mtoa mada hapo amejichanganya sioni wapi Naibu Waziri Mbene anahusika ukisoma barua ya manispaa ya Kinondoni ya 04/05/2010 kwenda Kwa Shomari. Tuache kufanya mambo kisiasa na upotoshaji usio wa lazima. Wewe unachuki binafsi huyu mama wizara yake haihusiki kabisa na suala hili. Yeye wala hilo sio jimbo lake. Acheni hizo za kulete wachafu nyie
 
mie nina mashaka na mleta uzi, kajiunga 30 septermber 2012, ina maana lengo lake lilikuwa ni kuweka post hii au?? au umetumwa kumchafua naibu waziri wa fedha?? jipange mkuu, usilete uzi za uzushi hapa, waziri awaamuru manispaa kumbomolea mtu au kumwamisha mtu?? kwani hiyo manispaa hain master plani ya eneo husika?? haijui ianalopaswa kufanya mpaka waziri wa fedha awaingilie?? isitoshe kunawezekana kubadili matumizi ya ardhi husika sheria ya ardhi ya mwaka 1999, no.4 imeainisha hilo
 
igwana123 acha uongo mleta mada hakuweka barua ya tarehe 04/05/2010. Ameweka barua ya tarehe 17/06/2010 kutoka manispaa ya kinondoni ikijibu barua ya Shomari ya tarehe 04/05/2010 ambapo alikuwa ameomba kupimiwa eneo lililopo Masaki. Hata hiyo, Mh. Mbene anahusika tuu kama M/Kiti wa mtaa Masaki.

Ukisoma barua ya tarehe 30/12/2010 inatoka ofisi ya serikali ya mtaa wa Masaki na imesainiwa na Mh. Mbene mwenyewe ikimtaarifu Shomari kuondoka kwenye eneo la wazi. Maajabu ni kwamba katika eneo hilo hilo la wazi, Manispaa ya Kinondoni ilimwandikia Shomari kuwa ni sehemu ya barabara kwa mujibu wa mchoro wa Mipangomji namba 1/499/169. Kwa hiyo Mh. Mbene na ofisi yake ya mtaa anadhani ni eneo la wazi wakati manispaa inasema ni eneo la barabara.

Lakini pia kuna barua muhimu ya tarehe 15/09/2011 kutoka kwa Kaimu Katibu wa Waziri, Wizara ya Ardhi kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuhusiana na mgogoro kati ya Shomari na Jaspreet Kaur ambayo inataka maelezo ya kina kuhusiana na huu mgogoro. Barua inasema hata Waziri mwenyewe alistaajabu juu ya huyu Jaspreet Kaur na ana interests gani kwenye hili eneo wakati manispaa ya Kinondoni tayari imeshasema kuwa ni eneo la barabara?

Huyu Mkurugenzi wa manispaa alipeleka ufafanuzi aliotakiwa na waziri?
Na huyu Jaspreet Kaur ni nani?
 
Last edited by a moderator:
Ciello badala ya kujadili hoja unaanza kujadili mleta hoja kajiunga lini. Kwani kuna ubaya gani kujiunga na JF kwa ajili ya kuweka post tuu? Sheria za JF zinakataza? Mbona wewe umejiunga juzi tarehe 7 September 2012 na hatusemi? Tena ulivyojiunga ulianzisha thread na kusema kuwa umeamua "kujitosa kuwa miongoni mwa magreat thinkers". Kuwa great thinker then.

Hata kama matumizi ya eneo husika yalibadilishwa na sheria ya ardhi ya mwaka 1999, how come then Jaspreet Kaur alimilikishwa hilo eneo tokea mwaka 1995? Unataka kuniambia kuwa hiyo sheria ili-apply retrospectively?
 
Last edited by a moderator:
mkuu EMT halikuwa dhumuni langu kumjadili mleta uzi, ila nilitaka kuweka angalizo kusijekuwa ni illmotive behind the accussations, migogoro ya arhdi na ishu nyingi za ardhi ni very sensitive na watu hawatakiwi kujudge basing on one side claims and evidence, ardhi ni miongoni mwa maswala tete katika nchi yetu, nasema haya si kwakufikiri bali niko uwandani nayashuhudia haya even sometimes binafsi nakutana na ishu kama hizi katika utendaji wangu wa kazi
 
Last edited by a moderator:

Soma attachments za barua kwenye post namba 75 hapo. Halafu Mzee wa Masaki tuelezee step by step nini kiliendelea baada ya waziri wa ardhi kumtaka mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni kutoa maelezo. Ulipokea majibu yoyote kutoka kwa waziri au mkurugenzi wa manispaa? Ni kweli ulifungua kesi mahakamani? Unaweza kuwepo nakala za hukumu yenyewe hapa?
 
Last edited by a moderator:


Ndambonyiliva, inaonyesha umeandika kwa masikitiko makubwa kuhusu tukio hili. Lakini ni lazima Watanzania tufike mahali tubadilike kimitazamo na fikra, enzi ya kumaliza matatizo kwa kusema Mungu atawalipa ndilo lililotufikisha hapa tulipo sasa, Watanzania wengi tunazidi kupoteza mali zetu halali kuwa kuendelea kusema hili namwachia Mungu na wale wenye tamaa kuendelea kujichukulia mali na haki za wengine. Ni wakati sasa kuacha kufikiria hivyo na kupambania haki zetu.

Namshauri Bw. Shomari aende ngazi nyingine ikibidi kuomba ushauri wa kisheria kutoka kwa wanasheria ili aweze kupatiwa haki yake. Waziri hayuko juu ya sheria tatizo ni hilo tu kuwa watu wanawatishia wengine kwa kuchukua udhaifu wa mfumo wetu wa sheria.

Namshauri aende vituo vya haki za binadamu wanaweza kumsaidia wanasheria watakaosimamia haki yake, huyo Naibu waziri pia anatishia kuona kama jamaa atakimbia na kuacha akiona amekomaa atakimbia mwenyewe. Kwanza angeweza kumshtaki tu hata sasa kwa kumdhalilisha yeye na familia yake.

Hata humu JF nadhani kuna wanasheria wazuri tu, ni muhimu kusadia vitu kama hivi kama kweli tunauchungu na maisha ya Watanzania wenzetu, tukianza na huyu mmoja ndiyo mwazo wa kubadili mifumo yetu ya kibabe kwa wenye dhamana ya vyeo.

Please nawaombeni watanzania enzi ya kumwachia Mungu mambo ya yaende Tanzania imepita watu hawajali hilo hata kama wanakesha makanisani kumwomba Mungu. Sasa wimbo uwe haki yangu haipotei bure nitaipigania hadi kufa na siyo kumwachia Mungu akulipe. Shituka ewe Mtanzania.
 
Ama kweli hujafa hujaumbika...
Huwa naamini hakuna viumbe wenye roho mbaya kama wanawake...
Sipati picha ndo awe mama wa kambo flani lazima madogo wafe njaa

Futa kauli au kuwa specific kwa Janeth Mbene! Your mom is a woman, your wife/gf is a woman, your sista is a woman too!!

Labda una bad experience ya wanawake, ila me benafsi sina thats why I love them most!!! Nawaheshimu sana
 

Mambo mazito haya kama ni ya kweli!!! Siamini macho yangu. Time will tell!!!
 

Hata mimi nakubaliana na wewe lakini tukumbuke pia kuwa ardhi kwa Tanzania ni mali ya Umma na Raisi ndiyo kapewa mamlaka ya kuisimamia kama mdhamini mkuu, yawabasi kama ilipopimwa na kutengwa kuwa ya barabara na je yule kwa wakati huo alikuwa akiishi pale alifidiwa? Kumbuka pia kuna hoja imesemwa humu Shomari alikaribishwa na akawa analima bustani, je Serikali ya Mtaa ilipoona inahitaji eneo lake imemfidia na kumtafutia mahali pengine? Maswali ni mengi majibu hakuna, hii inadhihirisha Wakubwa wana manufaa na jambo hili.
 
nawe kwa umbea umezidi,..mambo ya chadema unajifanya unayajua,ya serikali za mitaa wewe,ikulu wewe,..nyinyi ndio usalama wa ccm
 
Shomari ana history ya kuvamia maeneo ya wazi,kwa muda mrefu sana.Mbagala walimtimua,akavamia pale salender pia wakamtimua.Pale Masaki pia alipavamia.mimi namjua Shomari toka akiwa mdogo,nnamjua mama ake na ukoo wake,shomari Bibi zake wote upade wa baba au mama akuna aliyewai ishi masaki ata kwa siku moja!Mama ake mzazi mpaka nnaandika haya muda huu anaishi Kigogo na ndugu wengine wa shomari.
 
Very healthy CV. I wonder if what has been written here about her is true, considering the capacity building she has been doing for the less priviledged!!
 
Very healthy CV. I wonder if what has been written here about her is true, considering the capacity building she has been doing for the less privileged!!
 
Asante Tumtemeke. Jamani wana JF hakikisheni mnapoweka mada hapa jamvini mmezifanuia utafiti. Sasa watu wamemtukana mama wa watu matusi makubwa kumbe ni mambo ya uongo!! Hii haipendezi hata kidogo. No research no right to post anything here!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…